Lissu umeutumikia upinzani na kumwaga damu yako kwa gharama kubwa, upinzani uliokoa maisha yako, kulikoni?

Lissu umeutumikia upinzani na kumwaga damu yako kwa gharama kubwa, upinzani uliokoa maisha yako, kulikoni?

tripof

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
829
Reaction score
1,120
Kusema ukweli sitegemei Lissu atoe kauli alizozitoa kuwa CHADEMA siyo mama yake, ni kweli wote tunafahamu hivyo lakini angalia historia yako kwenye upinzani, na hadi ulipopigwa risasi.

Nadhani hakuna aliyeteseka na kupigania haki za watanzania kama wewe. Safari ya mapambano ni ndefu na ngumu ina "dynamics" nyingi. Wewe ni Nelson Mandela wetu usiogope mtu awe ndani ya chadema au kwingine popote,wasikilize wananchi wanasemaje. Fullstop.

Pia Soma
- Kuelekea 2025 - Lissu: CHADEMA ikiondoka kwenye misingi iliyonifanya nijiunge nacho, nitaondoka. CHADEMA siyo mama yangu wala dini yangu
 
Hakupigwa risasi kwa ajili ya chadema ni kwa ajili ya msimamo wake, manesi na madaktari waliookoa maisha yake hawana uhusiano na chadema, waliotoa ndege kumpeleka nairobi ni wana ccm, magumu aliyopitia si kwa sababu ya chadema, ila raha alizo enjoy ni kwa sababu ya chadema,
 
hakupigwa risasi kwa ajili ya chadema ni kwa ajili ya msimamo wake, manesi na madaktari waliookoa maisha yake hawana uhusiano na chadema, waliogoa ndege kumpeleka nairobi ni wana ccm, magumu aliyopitia si kwa sababu ya chadema, ila raha alizo enjoy ni kwa sababu ya chadema,
Nimesema alipigwa risasi kwa kupigania haki za wananchi akiwa chadema. bado unayo nafasi ya kuupigania umma ukiwa hapohapo, wasikilize watanzania.Ukweli mchungu
 
Lisu yuko sahihi. Hamuwezi kupanga jinsi ya kumkabili adui, halaf mmoja wenu anatoka kwenda kwa adui kumwambia mlichokipanga ili alipwe kimya kimya kwa kutoa siri za ndani.

Mtu mmoja anatumikia mabwana wawili kwa masilahi yake binafsi alaf Lisu anyamaze!

Kinana akishakuweka karibu yake ujue umekwisha.
 
Attachments

  • images (10).jpeg
    images (10).jpeg
    30.3 KB · Views: 1
  • images (9).jpeg
    images (9).jpeg
    39.9 KB · Views: 1
kusema ukweli sitegemei Lissu atoe kauli alizozitoa kuwa Chadema siyo mama yake,ni kweli wote tunafahamu hivyo lakini angalia historia yako kwenye upinzani,na hadi ulipopigwa risasi. Nadhani hakuna aliyeteseka na kupigania haki za watanzania kama wewe. Safari ya mapambano ni ndefu na ngumu ina "dynamics" nyingi. Wewe ni Nelson Mandela wetu usiogope mtu awe ndani ya chadema au kwingine popote,wasikilize wananchi wanasemaje. Fullstop.
Tatizo vyama pinzani havina maji ya kunywa mengi.......grass moja kira mtu atie domolake..........
 
Lissu anataka kumpanda kichwani Mbowe. Ninadhani Mbowe hawezi fanya kosa kwa msaliti kama Lissu. Amfukuze.
 
Kosa lilikuwa kumpa umakamu Mwenyekiti Lissu mtu mtata, ingawaje na Mbowe naye kuendelea kuwa Mwenyekiti wa milele ni kosa. Mlifanya kosa wenyewe kubadili katiba. Rudini kwenye uhalisia na misingi ya awali.Wote wawili waondoke chama kijengwe upya na kifanye mageuzi upya.
 
kusema ukweli sitegemei Lissu atoe kauli alizozitoa kuwa Chadema siyo mama yake,ni kweli wote tunafahamu hivyo lakini angalia historia yako kwenye upinzani,na hadi ulipopigwa risasi. Nadhani hakuna aliyeteseka na kupigania haki za watanzania kama wewe. Safari ya mapambano ni ndefu na ngumu ina "dynamics" nyingi. Wewe ni Nelson Mandela wetu usiogope mtu awe ndani ya chadema au kwingine popote,wasikilize wananchi wanasemaje. Fullstop.
Hakuna chama ambacho ni mama wa yeyote. CCM siyo mama kwa Rais Samia hata akiulizwa muda huu. Vivyo hivyo Chadema siyo mama kwa Mbowe, na wanachama wote.
Hili ni jibu kutoka kwa yeyote mwenye akili nzuri.
Kwani wewe chama chako kina thamani au umuhimu kama mama yako?
 
hakupigwa risasi kwa ajili ya chadema ni kwa ajili ya msimamo wake, manesi na madaktari waliookoa maisha yake hawana uhusiano na chadema, waliogoa ndege kumpeleka nairobi ni wana ccm, magumu aliyopitia si kwa sababu ya chadema, ila raha alizo enjoy ni kwa sababu ya chadema,
Unajisahaulisha si mlitaka apelekwe Mhimbili nyie ili........? Aliyeshikilia chupa ya damu wa CCM? Wakati hata maji hamuachiani acha wewe!
 
kusema ukweli sitegemei Lissu atoe kauli alizozitoa kuwa Chadema siyo mama yake,ni kweli wote tunafahamu hivyo lakini angalia historia yako kwenye upinzani,na hadi ulipopigwa risasi. Nadhani hakuna aliyeteseka na kupigania haki za watanzania kama wewe. Safari ya mapambano ni ndefu na ngumu ina "dynamics" nyingi. Wewe ni Nelson Mandela wetu usiogope mtu awe ndani ya chadema au kwingine popote,wasikilize wananchi wanasemaje. Fullstop.

Pia Soma
- Kuelekea 2025 - Lissu: CHADEMA ikiondoka kwenye misingi iliyonifanya nijiunge nacho, nitaondoka. CHADEMA siyo mama yangu wala dini yangu
Labda anatofautiana kimtazamo na wenzie kwenye chama ni haki yake
 
Back
Top Bottom