Lissu unasema uongo kuhusu Jeshi la Akiba, umesahau au hujui?

Lissu unasema uongo kuhusu Jeshi la Akiba, umesahau au hujui?

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
245
Reaction score
314
Juzi nilimsikia intern wangu akidai mgambo ni intarahamwe na kuwa hakuna kitu kinaitwa jeshi la akiba. Nimpe benefit of doubt kuwa hajui au kasahau.

Ningependa nimumbushe tena kwa picha. Kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha JKT na jeshi la mgambo yeyote aliepitia JKT au mgambo ni askari wa akiba. Nchi ikiingia vitani anawajibika kuitika wito wa amiri jeshi mkuu. Ndivyo ilivyokuwa mwaka 1978 ambapo baadhi yetu ilitulazimu kwenda vitani.

Amiri Jeshi Mkuu alitangaza taarifa ya habari saa 2 usiku chini ya David Wakati kuwa wale wote tuliotoka JKT turudi jeshini. Binafsi nilipelekwa CHUI BRIGEDI tuliyoanzia matayarisho pale Old Shinyanga; Jukumu letu la kwanza ilikuwa kumfurusha Nduli na askari wake kutoka kiwanda cha sukari Kagera. Kiwanda kilikuwa kipya lakini ilitulazimu kukivunja kwa makombora! Ndipo tulipomfurusha akakambia na kuvunja daraja ili tusimfuate! Alishaanza kuonja joto ya JIWE.

Inashangaza Lissu hajui hili! Ninamuwekea picha za wapinzani wenzake wakiwa JKT na hakika hata wao kwa mujibu wa sheria ni askari wa akiba! Yuko hapa Zitto, Mdee na Bulaya! Je hawa nao ni ni Intarahamwe?

Yampasa Lissu na wenzke wajue jeshi la akiba tupo! Na sisi amiri jeshi mkuu akituambia tuingie barabarani wataweza? Maana anazungumza as if wao pekee ndio wanajua kuingia barabarani!

Hapa pia namwekea picha ya ambao hakika ndio Intarahamwe! Tena wa chama chake! Lissu atueleze hawa wa chadema ni jeshi gani? Hawa ambao Mbowe anapokea saluti ni Inatarhamwe haswaa! Lakini Lissu hawaoni

1599554407497.png
1599554431765.png
1599554447755.png
 
Lisu ni mtu wakuhurumia na anataka kupewa urais wa kuhurumiwa
 
Kwenye sheria mama za nchi hii (Tanzania) hatuna "uchafu" unaitwa mgambo. Na wala sio sahihi kulinganisha "mbwa" au ukitaka "mgambo" na Jeshi la kujenga Taifa yaani JKT.

JKT ni jeshi kamili na wana "brigadi yao! na wapo kwa mujibu wa sheria. Hizi takataka nyingine (mgambo)ni "njaa njaa za wanaCCM" kujitafutia kitoweo tu sio wanajeshi.
 
Kwenye sheria mama za nchi hii (Tanzania) hatuna "uchafu" unaitwa mgambo. Na wala sio sahihi kulinganisha "mbwa" au ukitaka "mgambo" na Jeshi la kujenga Taifa yaani JKT.

JKT ni jeshi kamili na wana "brigadi yao! na wapo kwa mujibu wa sheria. Hizi takataka nyingine (mgambo)ni "njaa njaa za wanaCCM" kujitafutia kitoweo tu sio wanajesh
i.
Na ndicho alichomaanisha Lisu
 
Juzi nilimsikia intern wangu akidai mgambo ni intarahamwe na kuwa hakuna kitu kinaitwa jeshi la akiba. Nimpe benefit of doubt kuwa hajui au kasahau...
Swali la Tundu lilikuwa jepesi sana ila Tatizo mataga wote mmeshindwa kumjibu!

Lissu ameuliza Jeshi la akiba limeanzishwa chini ya sheria gani?

Nasikitika kwenye utumbo wako wote hata hukasema jeshi la Mgambo limeanzishwa chini ya sheria gani ya nchi!
 
JPM ndio muongo hajui hata Nyerere ametawala miaka mingapi anasema 27
 
Back
Top Bottom