Fact ni kwamba, Lisu ni kiongozi mkuu namba 2 Chadema.
Maamuzi yote ya Chadema yanaamuliwa na kamati kuu na baraza kuu na yeye ni sehemu yake.
Lisu kwa nafasi yake yeye ndio mamlaka ya nidhamu mwenyekiti hana hayo mamlaka katiba haisemi hivyo.
Mkuu wa nidhamu wa Chama ndio hana nidhamu unategemea hawa watoto waliojaa kwenye mitandao nidhamu waipate wapi?
Narudia tena, huyu siyo Lisu ninayemjuwa mimi.
Mama anavyoamini yeye Mbowe aliyetoka jela siyo Mbowe wa zamani, na mimi naamini kwa dhati kabisa, Lisu niliyemjuwa kabla ya kupigwa risasi siyo Lisu huyu mropokaji, hana adabu na anajiona yeye ndio bora kuliko mtu yeyote, huyu na Magufuli tofauti yao ni vyama tu.