Lissu: Wakati wa Magufuli waandishi walikuwa wanaogopa kunihoji, kwa sasa wanaweza kunisogelea

Lissu: Wakati wa Magufuli waandishi walikuwa wanaogopa kunihoji, kwa sasa wanaweza kunisogelea

Uzima Tele

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2023
Posts
1,270
Reaction score
2,822
Ameyasema leo akihojiwa na Ngasa TV leo Dodoma akiwa njiani kuelekea nyumbani kwao Ikungi, Singida..

Akizungumzia utawala wa Rais Samia Suluhu, amesema moja ya mambo yaliyobadilika kidogo baada ya Mwendazake John P. Magufuli kufa, ni waandishi wa habari kuwa na ujasiri wa kumsogelea na kumhoji kama hivi..

Kabla ya hapo, ilikuwa ni hofu na woga wa kufunguliwa mashitaka au kufungiwa na TCRA..

Mtazame na fuatilia mahojiano hayo katika video hii hapa nchini..
 
Ameyasema leo akihojiwa na Ngasa TV leo Dodoma akiwa njiani kuelekea nyumbani kwao Ikungi, Singida..

Akizungumzia utawala wa Rais Samia Suluhu, amesema moja ya mambo yaliyobadilika kidogo baada ya John P. Magufuli kufa, ni vyombo vya habari mbalimbali na waandishi wao kuwa na ujasiri wa kumsogelea na kumhoji kama hivi. Kabla walikuwa wanamuogopa kama ukoma kwa sababu yeye huwa hakopeshi wala kuwalemba watawala.



Kabla ya hapo, ilikuwa ni hofu na woga wa kufunguliwa mashitaka au kufungiwa na TCRA.

Mtazame na fuatilia mahojiano hayo katika video hii hapa nchini.
 
kwny maridhiano kumsakama CHUMA ni azimio namba ngapi?
 
Hahah kuna TV moja nilisikia wanajitoa kwenye mahojiano. Wanasema “ yaliyozungumzwa hapa ni msimamo wa Tundu Lisu na si media”
 
Hahah kuna tv moja nilisikia wanajitoa kwenye mahojiano. Wanasema “ yaliyozungumzwa hapa ni msimamo wa tundulisu na si media”
Ni Clouds TV & Radio juzi kati kwenye kipindi Chao Cha 360°

Yaani wametaka wenyewe wahojiane, wakauliza maswali wenyewe walichotaka kukifahamu lakini mwisho wa siku wanasema, "huu si msimamo wa Clouds TV"

Si wangenuamaza tu?
 
Mkuu kumbuka kuna kurudisha mikopo. JPM alikopa mikopo ya kibiashara ya muda mfupi na riba kubwa. Sasa hiyo mikopo inatakiwa kurejeshwa na miradi yoote mikubwa aliyoanzisha kuanzia ununuzi wa midege, SGR, bwawa la umeme n.k hakuna hata mmoja umeweza kurudisha hata shilingi. Mambo siyo rahisi kama tudhanivyo.

Sema watu wengi ni wajinga, wanadhani ukikopa hakuna kurejesha au Burundi ndiyo watarejesha hiyo mikopo ya Jiwe.

Serikali inabidi itoe elimu zaidi
Mikopo mfano imejenga shule nyingi na hospital kila mahali

Lakini Afende sele aelewe mikopo ni madeni sasa yanalipwaje. Mkopo mfano ya sehemu y kwanza ya reli Magu alikopa kwa riba ya juu sana 8% kwa miaka 6 mkopo wa $1.5 B mi kama billion 600 kwa kila mwaka je pesa hizi za kulipa zinatoka wapi? Lakini reli bado haijaisha hizo pesa zinatoka wapi?. Pesa za bwawa zitoke wapi.

Utaratibu wa kutaifisha pesa za wafanyabiashara, kuteka matajiri na kuchukuwa pesa za maduka ya pesa haziwezi kuwa endelezi badala yake inabidi kuwe na mifumo mizuri.

Watanzania waliowengi ni wajinga mama anatakiwa afanye kazi asiwasikilize hawa wapuuzi aina ya afande sele magufuli aliacha hazina ikiwa nyeupe kwa miradi yake ya kipumbavu ambayo MPAKA leo haijaleta faida mfano mandege ya ATC ni hasara tupu na bora alikufa maana hela alishamaliza kwenye kihenge tukawa hatukopesheki tena the only solution aliyoiyona ni kuanza kuteka matajiri na kukwapua hela za watu mbaya zaidi akaingilia MFUMO wa mahakama wa kununua haki (plea bargain) na ili kuondoa ukosoaji akaterorize taifa yoyote aliyemkosoa alikiona cha mtema kuni leo hii Huyo selemani msindi ingekuwa enzi za belzebuul magufuli angeshakuwa misitu ya bigwa au tungi Morogoro huko analiwa na funza hicho ki tv uchwara cha mtandaoni kingepigwa bomu na kuuwawa watu wake mwacheni mama afukie mashimo ya mwehu yule wa chato.

Umerogwa wewe, kwahiyo zile za kwenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni zilikuwa za mungu wenu pia?

Kwamba wakati jpm anaingia aliikuta reli ya kigoma imeishia dodoma na yeye ndo akaileta dar es salaam?!!!! Nilikuwa sijajua hili.

Sijajua afande sele ana nini na baadhi ya marais fulani fulani hivi maana nilishawahi kumsikia katika mahojiano ya radio kipindi fulani hivi (kabla jpm hajafariki) akimponda mno kikwete. Alikuwa anasema kuwa kikwete hakufanya lolote katika kipindi chake na kwamba jpm aliikuta nchi ikiwa haina mradi wowote ule na hivyo kila mradi alioufanya jpm ameuanzisha mwenyewe. Leo anasema jpm aliiendeleza vema miradi aliyoikuta. Sasa sijui miradi ipi na sijui iliachwa na mkapa au nyerere?!!!!

Alipofariki jpm, afande sele ni mmojawapo kati ya watu kadhaa wachache waliofanya jitihada za kutaka kuiaminisha jamii kuwa jpm aliuawa, na bila aibu, huruma wala shukrani alimlenga kikwete moja kwa moja.

Leo amemvaa mama, akisema hakuna mradi wowote unaoendelea. Anayasema haya huku tulio binadamu wa kawaida (tusio na chuki, hila, ukanda au udini) tunajua, kusikia na kuona maendeleo ya miradi km madaraja (eg wami linafunguliwa hivi karibuni, lile la iringa etc); viwanda vinaonekana na kuendelea kujengwa; mabarabara; hilo bwawa walilokuwa wanajifichia haters ukweli umeanikwa live kuwa limeendelea hadi 67%; mashule maalum (ukiacha haya madarasa yanayoongezwa) yanajengwa mikoa mingi tu n.k. Tatizo la tozo (ukweli na kuelewa vs uwingi na ukubwa wake) lipo lakini ni vipi linamfanya afande huyu adanganye?!!!!!! Ni dhahiri ana kitu, very unhealth, na baadhi ya maraisi.

Sijajua chanzo cha hili ni nini au inawezekana kule kubadilika kwake kumemuathiri maana nasikia alibadili na siku hz ni mlokole................

Hivi unajua kuwa mpaka leo ike 1.5 tr bado haijulikani iko wapi?

Hakuna mauaji ya raia kutoka kwa watu wasiojulikana

Kinachowaumiza wala sio tozo bali ni chuki zenu binafsi dhidi ya Rais aliyopo madarakani ndio maana mnajitia upofu,Ni kweli wakati wa Magu hakukuwepo na tozo lakini watu wengi walidhulumiwa fedha zao kinguvu na wengine kupotezwa sasa wewe unaona bora wananchi wote tuchangie au wachache wadhulumiwe kwa kuchukuliwa fedha kinguvu huku wakiziakiwa kwa kuitwa mafisadi?

Kwahiyo Mo naye alikuwa drug dealer halafu wameshindwa kucheza movie vizuri yao vizuri eti katekwa nyala! Unazungumzia nchi kupata heshima wakati ndio alivuruga diplomasia! Na kutosafiri ni kutokana labda na sababu zake binafsi lakini haikuwa na maana yoyote kwa nchi,binafsi nikipima kati ya wema na ubaya naona ubaya ulikuwa mwingi sana sawasawa na kulisifu jambazi liliyopata utajiri kwa kutoa roho za watu na kupora fedha na mali zao.

Unaongea hoja zaidi ya tatu Kwa pamoja...

Hoja ya kwanza ... Umuhimu WA kukopa....

Hoja ya pili ..ufisadi wa pesa zilizo kopwa...

Hoja ya Tatu ..alivyokopa Magufuli ilikuwa sawa...


Ntakujibu hoja moja hapo ya tatu..

Ilikuwaje sawa?wakati hata taarifa Tu haikuwa sahihi...tulikuwa hatuambiwi tunakopa wapi na kiasi gani Kwa matumizi gani ...kuficha ficha ndo kunapelekea ufisadi ambao huwezi hata kuujua...

Twende na hoja no 2...Je kweli Magufuli alidhibiti ufisadi?..
Wewe unajua gharama halisi za ujenzi wa airport ya chato?..bajeti Yake ?ilitangazwa wapi?Bunge lipi la bajeti lilipitisha?kampuni iliyojenga ilitokea wapi? Huo mfano mmoja tu

Yani unataka wote tumuamini Magufuli huyu ambaye anawalaumu wananchi kwa kuchagua mbunge wa upinzani ndio maana hawezi kuwajengea barabara halafu kwenye mkutano huo huo anapaza sauti na kusema "maendeleo hayana vyama."?

Tuna imani na FSG mitano tena
 
Back
Top Bottom