Pre GE2025 Lissu: Waliopinga maridhiano toka mwanzo wote wameshughulikiwa, sasa nami nashughulikiwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Lissu amesema akiwa Ubelgiji hawa ni watu wa kwanza kabisa kuonesha uongo wa maridhiano na waliupinga kwa nguvu zote, nao ni Msigwa, Wenje, Lema, na Gaston.

Kipinga kwao maridhiano hayo kumefanya wote wameshughulikiwa, Wenje amepiga uturn kubwa baada ya kuona wenzake wanashughulikiwa, Msigwa kaondoka na wengine wameacha kugombea.

Soma, Pia: Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini

Sasa nami nimeanza kushughulikiwa kwakuwa nilipinga maridhiano haya baada ya kuona tunadanganywa na nikatoka hadharani kusema maridhiano hayo hayapo.

=====

"Waliopinga huu uongo wa maridhiano kwenye kamati kuu ni Peter Msigwa, John Heche, Godbless Lema, Gaston Garubindi, Ezekia Wenje kabla hajapiga U-Turn baada yakuona wenzake wanashughulikiwa, hao ndo walikua mashujaa waku expose huu uongo wa maridhiano, mimi nilikuja mwishoni.! John Heche alikua mjumbe wa kamati ya maridhiano and he always came out and said Hapana, alinuniwa sana! Godbless Lema akiwa uhamishoni Canada alikataa." Mhe Tundu Lissu akiweka wazi watu waliopinga uongo wa maridhiano kwanzia Mwanzo!

 
Msigwa yuko wapi sasa baada ya kupinga maridhiano? Kwa hio Msigwa alikimbilia kule abako wanapinga kufanya maridhiani na CDM?
 
Msigwa alianza kwa kuunga mkono serikali katika suala la Ngorongoro lakini hakuchukuliwa hatua yeyote. Akaanza kumtupia madongo ya waziwazi Mwenyekiti wake ( inaelekea akipigwa tough ya chini chini na Lissu), hakuchukuliwa hatua. Nae kama anavyosema Lissu aliapa kuwa hatatoka CDM kwa namna yeyote ile. Kashindwa uchaguzi na sasa ni kada mkubwa wa CCM. Na kuna mtu mmoja wa CCM alisema wazi kuwa mazungumzo na Msigwa yalianza hata kabla ya uchaguzi. Haiwezekani kuwa CDM walimshughulikia baada ya kumstukia? Matendo yake baada ya kuondoka CCM yanathibitisha kuwa walikuwa sahihi. Unaweza ku imagine sifa ambazo CCM wangepata kama angehamia baada ya kushinda uchaguzi? Na tukumbuke Lissu hajasema lolote kuhusu usaliti wake.

Lema ametangaza kutogombea na amewasifu walioshinda. Kama aliacha kugombea kwa sababu ya figisu figisu za Mbowe basi ni mnafik mkubwa. Mimi nahisi amegundua opportunities za biashara Canada na ameamua ajikite zaidi kwenye biashara zake.

Heche kweli amekuwa kimya. Lakini sasa hivi yuko mdogo wake na anafanya vizuri tu.

Sikatai kuwa kuna watu walipinga mpango wa maridhiano. Lakini vile vile wako walio muunga mkono Mbowe. Katika demokrasia uamuzi wa wengi ndio unakuwa msimamo wa chama. Sasa kama hata kwenye hili anashindwa kuheshimu maamuzi ya wengi itakuwaje kwa wale watakaotofautiana nae akiwa Mwenyekiti?

Amandla...
 
😂😂😂
 

Sasa mpaka Mbowe anampa Samia tuzo ya Maridhiano huoni kuwa Mbowe alitumika kumsafisha Samia mbele ya umma na Jumuia ya kimataifa?-Chama kilinufaikaje na Mbowe kumpa Samia tuzo ya maridhiano ambayo kama kawaida yao CCM waliyaruka baadae?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…