Kweli huu ni mwaka wa mageuzi wapi Kamala, Sarungi, Lubeleje, Malechela, Bendera, Mwapachu, Mshangama, Kimaro, Mzee wa Mchinga duuuu wameangukia pua wajameni nk. Mwakalebela kaanguka kwani kesi inayomkabili ni ya rushwa wakati wa kura za maoni ndio maana akaondolewa, lakini Mramba na Chenge kesi zao si za kisiasa na bado hukumu haijatolewa ila wakifungwa ubunge wao utasitishwa, shida ni wale waliowateuwa kuendelea kugombea ubunge kwenye majimbo haya hali wakijua hawa wamevunja sheria ana wanakesi, hasa la Mramba ni baya sana la kufisadi serikali.Kuhusu Selelii ni kutotulia kwake maana baada ya kushindwa alianza maneno na kuhamia CHADEMA, ila nina uhakika akienda kugombea pale Nzega kwa tiketi ya CHADEMA atashinda, Bashe anapendwa sana pale kama Selelii tu so huyu dogo hana ishu na CCM wameshalitema hili jimbo.
Hongera sana Rage na Mkhamia maana Simba tuliondokewa na wabunge wawili Lubeleje na Sarungi ila nyie mtaziba pengo. Nawapongeza vijana kadhaa kama January, Lusinge, Kizigha nk kwa kuwachapa wakongwe. Msisahau kuwa CHADEMA tumekuja kivingine mwaka huu.