Suala la ufisadi linachanganya sana, hivi ukikuta dukani soda inauzwa 200 badala ya 600 utakataa kwa sababu ni bei ndogo? Baadae mtu anakuambia yule muuzaji ni chizi kwa hiyo una makosa kununua soda kwa being hio, kwani we ndie uliyemweka yule chizi kuuza dukani.
Eti RA alinunua viwanda kwa bei ndogo hivyo ni fisadi, kwahiyo angekataa angesema niongezeeni bei, hii ni ndogo sana!!! Watu wanaenda mbali eti auwawe!!! Kosa no kunua kwa bei ndogo au kuuza???
Hamjui kuna vingine hata hiyo bei ndogo vilikosa vimekuwa stoo ya popo, badala ya kumshukuru angalau amenunua viwanda vilivyo uwawa na serikali ya ujamaa. Hivyo hamvisemi, kuna kiongozi anaweza kukwepa lawama za kufa kwa viwanda kuanzia Nyerere aliyepewa msaada na wachina na warusi lakini vikafia mkononi mwake, Mwinyi akavizika, Mkapa akavifufua kwa kuviuza angalau kwa bei yoyote, anaambulia matusi tu??