List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Huyu bwana naona Dr Slaha kakurupuka kumtuhumu kama kawaida ya wapinzani. Hawafanyi homework ya kutosha na wanapenda cheap popularity.

Huyu jamaa alipinga sana IPTL na sote tunaelewa hilo Ngoja nitafute ile thread ya IPTL tuirudishe hapa.

Wananchama wapya wa JF naomba ikirudi (thread ya IPTL) muisome kwa makini muamue!
 
Asante SAM, nimechukua hii kutoa kwenye post yako ya IPTL:

Hii inamsafisha huyu mwananchi: Like James Rugemalira, Rutabanzibwa is from Kagera, but there the similarity ends. Rutabanzibwa is from an aristocratic clan and is the son of a former ambassador.

He studied in the US and the UK. He is a brilliant technocrat, dedicated to the development of Tanzania. Rutabanzibwa was Commissioner for Energy when the IPTL project was first launched. He knows there is no need for extra generating capacity and that even if there was, IPTL would be the most expensive, rather than the ‘least cost' provider.

But he is surrounded by pro-IPTL lobbyists in Tanesco, his Ministry, and the government, who are constantly trying to undermine him.

He knows that when investment projects are taken over by politicians, technocrats like himself are sidelined, and only wheeled out to endorse decisions, however crazy, that have already been made. Rutabanzibwa tries to convince the President that IPTL ‘is a disaster waiting to happen.' If the cost of IPTL is passed on to the consumer, Mkapa will not make many friends. Business and private consumers will face huge increases in electricity prices.

Donors will be incensed. Their dismissive attitude towards IPTL is on record. On the other hand, many heavyweights in the party and cabinet are in favour of IPTL. They try to convince the President that Rutabanzibwa is in the pay of the Bank and Songas. There will be another power crisis if IPTL is not added to the national grid, they argue.

What if the rains fail again? Demand for power is growing fast…. Rutabanzibwa puts his job on the line: ‘I promise you, Mr President, there will be no more power cuts between now and the next elections. If I'm wrong, I will resign.' Rutabanzibwa has made his calculations. The ‘El Niño' rains have struck East Africa.

The dams are full to overflowing. An extra 180 megawatts of donor-financed hydro will come on stream in less than a year. Tanesco's demand projections for electricity are way too high. The big mining companies are signing power supply agreements with Tanesco - and bringing in their own generators to run the mines. Benjamin William Mkapa does not know what to do.

Amueni, myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Kuna jambo kubwa litawatokea hawa wala rushwa kabla ya mwaka huu kuisha. Pressure ni kubwa mno. Kuna kila dalili ya kulazimishwa kurudisha walichochota. Huko aliko Mkapa sijui anawazaje kwa sasa. Kuna watu watakimbia nchi tusipokuwa makini. Wamewekwa kwenye kibano kikali tokea tupate uhuru. Na kama kuna ambayer anakadili kake naona atakuwa amekaweka pending kwa sasa.
 
Mara nyingi huwa tunasali na kuswali, tukiomba na kutoa dua zetu. Mara hizo nyingi wakati mwingine tunaingiwa na shaka kama mbinguni wanatusikiliza... Hata hivyo, maendeleo ya sasa yananifanya niamini kuwa Mungu husikia sala za waja wake. Tuombe tuvuke kwa amani kipindi hiki.. bado nina hofu niliyosema kwenye "Mko Tayari"?
 
Maandamano ndio njia sahihi ya kudhibitisha kuwa msimamo huu wa kutaka mafisadi washughulikiwe sio wa Slaa, Wanasiasa,waandishi wa habari na wasomi pekee kama Warioba anavyotaka kujenga picha ya aina hiyo(kupotosha)bali ni wa waTZ wote. Jambo hili limefanikiwa katika nchi nyingi naamini hata kwetu LITAFANIKIWA.Maandamano yatafanya hata ulimwengu wote ufahamu nini tunataka maana hadi sasa inaonekana kama vile ni misuguano ya kisiasa tu mbele ya macho yao.Mkjj asante kwa wazo zuri,hata hivyo usiwe na hofu ya uliyosema katika "Mko tayari?" Ni kweli wakitumia nguvu kutatokea madhara kwa watu wasio hatia, lakini jee,maumivu yake yanalingana na vifo,dhiki na umasikini wa kudumu wa Wanyonge? LAZIMA TUGEUZE FIKRA ZETU ZIWE KAMA ZA WAPIGANIA UHURU WALIVYO.Mpigania uhuru adhima yake sio yeye lazima kufaidi matunda ya nchi yake maana anajua lolote laweza kutokea,bali anataka wengine na vizazi vijavyo wayapate kula matunda ya nchi yao kama binadamu.Wakati wenyewe ni sasa.
 
Wazo la Mkjj, ni muafaka sana. Ningeshauri walifikishiwe mapema sana ikiwezekana kabla ya kikao cha leo watakachokifanya na waandishi wa habari ili tarehe itangazwe rasmi leo. Ikiwezekana weekend hii lets say jumapili ingekuwa vizuri zaidi. Wananchi wengi wanatamani kupata nafasi ya kuunga mkono jitihada hii. Na nianaamini maandamano hayo yataweza kuvunja rekodi. Na ingefaa yafanyike kabla JK hajarudi. ...Tatizo sijui kama watayaruhusu
 
Mzee Mwanakijiji mimi ninakuunga mkono kwa asilimia 1,000,000%. Maandamano makubwa ya kumuunga mkono Dr. Slaa ni muhimu ili kuonyesha jinsi sisi wenye nchi tulivyochoka na wababaishaji hawa Magaidi wa Kiuchumi.
 
There is somthing happening at Viwanja vya mnazi mmoja 29th Sep this Sat something to do with utawala bora and uwajibikaji wa viongozi just heard on eatv jana usiku.

Labda watu waandamane kwenda huko. Waandishi wa habari watakuwepo wengi. Ni wazo tu
 

Bravo Mwanakijiji naona wazo lako limepokelewa Nyumbani!Kama anavyozungumza Mheshimiwa hapo Juu,kutakuwepo na maandamano kesho,Jumamosi.
 


Safii Sanaaaaaaaaa! Kwa melezo hayo ni vizuri ametajwa katika orodha ya mafisadi na akienda mahakamani itasaidia kupata hizo ripoti za kitaalamu alizoshauri wanasiasa wakakataa!Na zaidi ya hayo tutapata kujua ni kina nani hao walioshinikiza mradi wa IPTL. Na baada ya hapo tutamhoji kwa nini hakuchukua jukumu la kujiuzulu kama maslahi ya umma yalikuwa hayajazingatiwa baada ya kushindwa kuwashawishi wanasiasa wakubalianae naye!
 
Bravo Mwanakijiji naona wazo lako limepokelewa Nyumbani!Kama anavyozungumza Mheshimiwa hapo Juu,kutakuwepo na maandamano kesho,Jumamosi.

maandamano hayo ni ya mada hii au ni ingine?

Sikitiko langu ni kuwa maandamano hayo hayakuhusisha mikoa mingine..inatakiwa maandamano yaandaliwe kwa nchi nzima, ..yaani kila mkoa unaandamana kivyake kwa siku moja, wakiangalia Dar mambo moto, wakienda Moro nako moto, ...hadi wazee wanakimbizwa hospitali kwa pressure...they have taken us for fools for so long...am itching to andamana!
 
Tunakushukuru Mkjj, kwa jitihada yako....Lowassa ni muhimu maelezo yake yapatikane, afadhari hata ya baadhi yasionekane lakini ya kwake yawepo, maana issue yake ni current (Richmond)na aliishinikiza kwa mabavu kuliko hata wengine.
 
Mimi nakumbuka huyu Bwana Rutabanzibwa alipinga sana dili la IPTL Shukrani kwa hiyo post FD na Sam, hivyo kwa suala la IPTL nitampa the benefit of the doubt, hiyo ya Tangold mhhh sijui...
 
Habari nilizozipata zinasema kwamba siku ile Dk Slaa anawaanika wazi Viongozi wanaodaiwa kuwa ni Mafisadi Timu za Yanga na simba muda huo huo zilikuwa zinafanya Mazoezi ktika viwanja Tofauti tofauti karibu na eneo hilo, nilipotafakari kwa kina nikagundua kwamba hapa kuna conspiracy ,lengo likiwa ni kudivert attention ya wananchi kwenda katika mpira

halafu tena wiki hii jumamosi Mheshimiwa Kabwe atakuwa Maeneo ya chuo kikuu akiunguruma , wananchi watapata fursa nyingine ya kumsikiliza Mheshimiwa lakini cha kushangaza ni kwamba Serikali siku hiyo hiyo imewaalika wanavichekesho wa kikundi Maarufu cha Ze Comedy, kikundi ambacho michezo yake inarushwa na Tv 5,
mgeni rasmi atakuwa ni Makamu wa raisi Dk Shein,watakuwa katika viwanja vya Mnazi MMoja.matukio haya yanaleta wasiwasi kwamba serikali inajaribu "kudilute" ajenda za wapinzani kwa kuwafanya wananchi wengi wasiende kuwasikiliza
 
Tena Ruta aliwahi kuwatimua hawa wa-malaysia wa IPTL na kuwaambia wawe "out of the country in the next available flight" lakini wazee wakatia guu.

Katika hili la IPTL Ruta anaonewa!
 
Hata yule bwana aliyelipukiwa na umeme majuzi wakati akiiba waya za umeme hai za TANESCO, hamkumbuki alisema kasingiziwa na kubebeshwa mkanda wa kiTANESCO ilhali ametoboka sehemu kibao mwilini kutokana na mlipuko huo?

Ukweli ni kwamba hata mwizi wa wake au waume za watu akifumwa live anajitetea kusingiziwa. Hiyo ni hulka ya kibinadamu kukataa mpaka sheria ithibitishe kwamba ni kweli umekuwa mhalifu. Kama tendo lenyewe lingelikuwa lenye sifa si ajabu kusikia mtu akitamba mitaani kuwa yeye ndiye kafanya. Kitu cha aibu hatutegemei kuwa mtendaji wake atakubali kirahisi. Ni maiti tu ambaye anaruhusiwa kutojitetea, utamfanya upendavyo sambi sako mwenyewe.

Viongozi wetu wa Tanzania jadi iliyopo sio kujiuzuru. Ndiyo maana Mzee Ruksa alipofanya hivyo kila kiumbe kilimshangaa. Lakini si alibarikiwa? Tena basi alijiuzuru kwa sababu uchafu umefanyika na wengine lakini chini ya himaya yake, wala yeye hakuwahi kufanya. Waache waende mahakamani, hapo ndio yatafichuliwa hata yale ambayo wadai hawakutaka kuyaanika kwa utu wema tu.

Lakini si kesi nyingi zimeyeyuka hivi hivi kama zinawahusu vigogo? Hata hizo kesi zinazoimbiwa nyimbo sana hazitadumu. Ni danganya toto. Hii ndiyo Bongoland.

Leka
 
Watu makini wataenda kusikiliza nondoz za Zitto na wale ambao wamelewa Ze Commedy wataenda One Coconut Tree kuangalia midebwedo. Jogoo awike asiwike lakini lazima kutakucha tu, hapo hakuna ujanja!
 
Samahani,
Orodha ya aibu ipo kwa kiingereza? Mimi kiswahili iko gumu sana, iko hangaika kutafsiri kwa hii jamii hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…