List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Bila shaka wanachedema wanao pata mhemko na kumtaka Lowassa wapitie humu. Kama walimtimua Zitto, watawezaje kumkumbatia Lowassa?
 
Bila shaka wanachedema wanao pata mhemko na kumtaka Lowassa wapitie humu. Kama walimtimua Zitto, watawezaje kumkumbatia Lowassa?

zitto ni mamluki aliyetumiwa na ccm kutoa siri za Chadema❕ kama ulikuwa haujui,kapiga Sana hela kutoka chama cha majambazi (CCM)
 

Dr Slaa katika uzinduzi kampeni Uchaguzi Mkuu 2010 Chadema Mwembeyanga Dar alipoanika list hiyo


Kumekuwepo uvumi wa uongo ya kuwa kwenye ile list of shame iliyotamkwa na Dr. Wilbard Slaa pale Mwembe Yanga eti jina la Mhe. Edward Ngoiyai Lowassa lilitajwa.

Ukweli ni kuwa orodha ya majina kumi ni hii hapa na Lowassa hayumo. Mnyonge msimnyonge bali haki yake ya kiukweli tumpe...

  1. Daudi Balali.
  2. Andrew Change.
  3. Basil Mramba.
  4. Agrey Mgonja.
  5. Patrick W.R. Rutabazibwa.
  6. Nimrodi Elirehema Mkono.
  7. Benjamin William Mkapa.
  8. Jakaya Mrisho Kikwete.
  9. Nazil Karamagi.
  10. Rostamu Azizi.
 
Mi sijui kama ni kweli au ndo tunamsafisha! maana habari yako haina source
 



Katika kumbukumbu zangu Lowasa alishakuwa kipenzi Chadema kama angekuwa mwepesi kusoma mzunguko wa sayari ya CCM inavyobadilikabadilika.

Chadema walieleza hadharani na bayana kwamba wapo tayari kumsafisha Lowasa angegeukia upande wao mara baada ya kujiuzuru Uwaziri Mkuu bungeni Dodoma. Wenye kumbukumbu mpo katika hilo?
 
Mi naona kama list hii imechakachuliwa. List halisi ya awali ilikuwa na majina 11 Lowasa akiwemo ndani.
Usafishaji wa namna hii utajenga Taifa kweli? Unafanywa kwa manufaa ya nani? Ni wazi hizi jitihada zote za kumsafisha mtu ni kwa maslahi binafsi: ila ya nani? Ya Lowasa au ya wapambe wake?
Ndiyo maana napinga Lowasa kuja UKAWA, uchafu wote utahamia kwenye UKAWA!!!
 
Naona na mtaka kwa hali na mali....

mchukueni tuu....ni Bomu na litalipuka muda wowote
 
Duh!fedha inaweza kununua uhai!
 

Angalia hapo juu nimeleta orodha ambayo Mzee Mwanakijiji aliweka mada mara baada ya mkutano mkubwa pale Mwembeyanga. Sidhani kama saver ya JF ina nafasi ya kuchakachuliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…