List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Mkuu njaa mbaya sana orodha ya mafisadi waliotajwa Mwembe Yanga na Dr.Slaa walikuwa 11 mtafute mmoja umuweke kwenye orodha yako mimi ninalo gazeti la MWANA HALISI.

Teh teh teh

Njaa waambie wabongo wenzangu wanaohangaikia kukinga vinavyoanguka toka meza za mafisadi, mimi napone changu kitokanacho na kuvuja jasho kubeba mabox ya mabepari, hayo ya njaa mwayajua wabongo wenyewe huko.
 
Mimi Nina imani na magufuli, katika maisha Yangu sina cha kumshukuru kikwete zaidi ya kutuachia magufuli, nimemsamehe kikwete yote alonikosea na pia natmia nafasi hii kumshukuru sana kwa kunipa raid niliekua namuota mheshimiwa john pombe magufuli
 
Mimi Nina imani na magufuli, katika maisha Yangu sina cha kumshukuru kikwete zaidi ya kutuachia magufuli, nimemsamehe kikwete yote alonikosea na pia natmia nafasi hii kumshukuru sana kwa kunipa raid niliekua namuota mheshimiwa john pombe magufuli

Sio bure,wewe lazima utakuwa ni Sundi Malomo!
 
Tatizo la vyombo vya habari Tanzania ni kuandika visivyofanana kwa kile kile kilichonukuliwa na wote. Orodha niliyoleta mimi ni ile ambayo nimeitohoa toka mada iliyoletwa na Mzee Mwanakijiji na nimeichukua kama ilivyotundikwa hapa JF.

Hii iliyoletwa na Mzee Mwanakijiji itakuwa imechakachuliwa ndio maana mimi nikawaomba mzee mwanakijiji na Invisible waje watupe ufafanuzi kwa hili
 
Last edited by a moderator:
Hii iliyoletwa na Mzee Mwanakijiji itakuwa imechakachuliwa ndio maana mimi nikawaomba mzee mwanakijiji na Invisible waje watupe ufafanuzi kwa hili

Haijachakachuliwa; labda watu wengine wameshasahau suala la orodha ile ya Mafisadi asili yake ilikuwa ni nini. Ni vizuri kuipitia ile mada nzima tangu wakati ule ile tujikumbushe.
 
Alichofanya hapa ni ku-expose zaidi kuwa Lowasa sio tu kuwa ni mwizi na mla rushwa.... bali pia ni mtu ambaye amepanga kuwa rais kwa LAZIMA hata kama watu wasipomchagua...

Duh watu mnamaono ya mbali, JAMBO FORUM katika ubora wake!
 
Ndio maana unakuwa mkali sana kwa sababu ni wewe mwenyene ndio unayetaka kuelewa hivyo. if you dont feel mwandosya or lowassa for 2015, do something about it now, not later. na kiwe kitu meaningful, sio kuishia kublog. atleast mimi ntapiga kura, wewe je? au kutakuja utaratibu wa kupigisha kura online?

loool....
 
wakuu,
salam,
nakumbuka list of shame imewataja kikwete,lowasa endrew chenge na wengine! naomba kuulza,hv hii list inakaz gan hasa? mbn waliotajwa wanapeta tu? mfano
1.kikwete alitajwa,lakn watz wakasema hawaitak kuickia,watamchagua kikwete 2010 tu! duuh

2.Andrew chenge,jana amepeta kura za maoni ccm, hahahaaa! kumbe tunawachagua wezi,wasaf hapana!
3.haya ANA TIBAIJUKA kura za maoni ccm amepeta, haaa mama wa escrow! duuh!

4.prof,muhongo wazir husika escrow et nae kapeta! mamaa
kumbe ccm wanafik kwel,wezi,fisad akiwa ccm anachaguliwa,lakin akihama kwenda kutubu,et hatakiwi! jaman kwa maelezo hayo na ukilnganisha pia na kule kenya,alieshtakiwa bdo akawa rais,bac hapa tz rais wa awam ya tano ni EDWARD NGOYAI LOWASA!
watz tumchague lowasa,mbn yeye kikwete alchaguliwa?
 
Kwa kupitia List of Shame iliyotolewa na Chadema kupitia katibu mkuu wake, Agenda kuu ya chama ikawa vita dhidi ya ufisadi.

Chadema wakatutajia majina ya mafisadi likiwemo la mgombea wake wa sasa kwa nafasi ya Urais. Wakatueleza ufisadi wake, na watanzania wengi waliwaamini.

Sasa amekwenda kujiunga nao, wanatuambia kua alionewa na hahusiki na tuhuma, hizo. Kauli hiyo ina maana kwamba walimkosea sana Lowassa kwa kumtuhumu bila kumsikiliza.

Mmoja kati ya waliopo kwenye hiyo list amashaondolewa, wamebaki 9, lakini hao vile vile hawakupewa nafasi ya kusikilizwa na chadema ili kujiridhisha kama tuhuma wanazowatuhumu ni kweli ama la. Hivyo tunapata picha kwamba, ikatokea hao wote kusikilizwa, hakuna atakayebaki katika list hiyo.

Ikatokea pia, wote waliobaki kwenye hiyo list, wakajiunga chadema, basi watapokelewa na tuhuma zao zitafutwa, kwa minajili hiyo, dhana nzima ya ufisadi inakua haipo ukiwa chadema, kila aliyepo chadema ni msafi, unafiki huu.

Msishangae sana, ikajafika siku, Chadema wakatuambia kua CCM hakuna fisadi ila sisi wanachi wa kawaida ambao si wanasiasa ndio mafisadi. Hawashindwi kufanya hivyo, maana ukweli ni kwamba, hawana ajenda ya kudumu na hakuna misingi katika ajenda zao.
 
Nadhani chadema sasa ndiyo kimekuwa chama cha ufisadi haswa kwasababu kiongozi wa ufisadi wanaye wao ndiye mwanzilishi wa ufisadi tanzania.
 
Hiyo Ajenda nayo sasa ihamishie nyumba ya Jirani, ili ESCROW isitokee kenye nyumba ya jirani
 
Binadamu kukosea ni kawaida. List of Shame imepungukiwa na mtu mmoja. Imekatwa. CHADEMA wameikata List of Shame. Wamebaki kumi kutoka kumi na moja.

Sasa CDM watueleze, mpaka kufikia hivi sasa, waliomsingizia ufisadi ni Lowassa tu. Au kwa kuwa ni mgombea wao wa Urais. What a coincidence! Walipobaini tu kwamba Lowassa atakuwa mgombea wao wa Urasi hapo hapo ndio wakabaini pia kwamba walikosea kumtaja kwenye List Of Shame.

CDM hebu pitieni upya ile List Of Shame. Unaweza kukuta wote mliowataja, hakuna fisadi hata mmoja. Yawezekana wote mmewasingizia. List Of Shame imepanda cheo na kuwa List of FAME.
 
moderators kuna ulazima wa kuunganisha uzi wa 2007 na huu, nyakati zimetofautiana na issues pia zimeongezeka, ukaribu wa mada hizi mbili haupo. hakukua na ulazima wa kuunganisha threads.
 
moderators kuna ulazima wa kuunganisha uzi wa 2007 na huu, nyakati zimetofautiana na issues pia zimeongezeka, ukaribu wa mada hizi mbili haupo. Hakukua na ulazima wa kuunganisha threads.
wewe mapengo usiwafundishe moderators kazi
 
Baada ya mwaka 1995 Mwalimu Nyerere kumkataa Lowassa kama angepitishwa kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM, hali imekuwa hivyo kwa upande wa Dr. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema ambaye amejitenga na wenzake juu ya maamuzi ya kumpokea Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais kwa kupitia chama hicho.

Slaa alieongoza jopo la makamanda wa Chadema kuichafua CCM kwa kumuita Lowassa fisadi, leo hii angepaswa kuratibu mpangokazi mwingine wa kumsafisha na kumpigia kampeni mtu yuleyule waliomchafua kwa kutoa ushahidi katika majukwaa mbalimbali nchi nzima.

Hata hivyo Dr. Slaa ameonelea kujiweka pembeni na kukataa kuwa mnafiki wa kisiasa kwa kumsafisha mtu ambaye ananunka rushwa.

Hakika kwa hili Dr. Slaa anafuata nyayo za Nyerere kwa kuwasema hadharani wala rushwa na kukataa kuwasafisha kwa ushawishi wa mabilioni ya pesa.
 
Back
Top Bottom