Kwa kupitia List of Shame iliyotolewa na Chadema kupitia katibu mkuu wake, Agenda kuu ya chama ikawa vita dhidi ya ufisadi.
Chadema wakatutajia majina ya mafisadi likiwemo la mgombea wake wa sasa kwa nafasi ya Urais. Wakatueleza ufisadi wake, na watanzania wengi waliwaamini.
Sasa amekwenda kujiunga nao, wanatuambia kua alionewa na hahusiki na tuhuma, hizo. Kauli hiyo ina maana kwamba walimkosea sana Lowassa kwa kumtuhumu bila kumsikiliza.
Mmoja kati ya waliopo kwenye hiyo list amashaondolewa, wamebaki 9, lakini hao vile vile hawakupewa nafasi ya kusikilizwa na chadema ili kujiridhisha kama tuhuma wanazowatuhumu ni kweli ama la. Hivyo tunapata picha kwamba, ikatokea hao wote kusikilizwa, hakuna atakayebaki katika list hiyo.
Ikatokea pia, wote waliobaki kwenye hiyo list, wakajiunga chadema, basi watapokelewa na tuhuma zao zitafutwa, kwa minajili hiyo, dhana nzima ya ufisadi inakua haipo ukiwa chadema, kila aliyepo chadema ni msafi, unafiki huu.
Msishangae sana, ikajafika siku, Chadema wakatuambia kua CCM hakuna fisadi ila sisi wanachi wa kawaida ambao si wanasiasa ndio mafisadi. Hawashindwi kufanya hivyo, maana ukweli ni kwamba, hawana ajenda ya kudumu na hakuna misingi katika ajenda zao.