Elections 2010 List ya viti maalumu yatoka

Elections 2010 List ya viti maalumu yatoka

Hapana analysis yako ina mushkeli kidogo mkuu, umesahau kuwa CHADEMA haikusimamisha wagombea Ubunge kwenye majimbo mengi tu lakini majimbo hayo hayo bado wananchi walipata fursa ya kumpigia kura Dr. (PhD) Slaa kwenye nafasi ya Urais. Kwa mantiki hiyo basi ni lazima Dr. atakuwa amepata kura nyingi zaidi ya wagombea wote (combined) wa viti vya Ubunge kupitia CHADEMA.

Mkuu,

Asante, hiyo ni valid point na ndio maana ya analysis maana unaangalia pande zote na kujua kwanini jambo fulani liko hivyo? Lakini kama nilivyoandika awali, matokeo hayo kwa CHADEMA yalitegemewa kwasababu hizo ambazo tumezitaja. Ila hilo la wabunge wa CCM kuwa na kura nyingi kuliko JK binafsi sikulitegemea.
 
Inafaa mtu uwe na peremende kidogo mfukoni, unaposikia njaa kwa mbaliiii unakuwa na kitu chako cha kumumunya mumunya yahe ili kupunguza makali ya njaa au kusafisha kinywa kidogo.[/




Duu mwaka huu Dodoma hapatoshi!
 
Naandaa Popcorn na kreti la Tusker Bariiiidiiiiiiiiiiii... Kwani Bunge letu litakuwa c mchezo.
 
Kiungani,

Hapo juu hesabu zako zimenichanganya na nimeshindwa kukuelewa.

Nilichoandika ni kwamba inaelekea kwenye ubunge CHADEMA wamepata kura chache kuliko za urais. Kitu ambacho nilitegemea maana Slaa alikuwa maarufu kuliko wabunge wake. Kama wana viti 23 katika 102 ina maana wana around 23% ya kura za ubunge. Lakini kwasababu unatoa kura za vyama vidogo (kwasababu havishiriki mgao wa viti maalum kwa sababu ya kukosa at least 5% ya kura) basi hiyo asilimia 23 inashuka na kuwa chini ya asilimia 23. Ndio maana nika conclude kwamba wabunge wamepata kura chache kuliko rais wao maana Slaa alipata zaidi ya 26%

Upande wa CCM, kama wana viti at least 67 ina maana wamepata kura around asilimia 67 za wabunge wakati rais wao alipata kura asilimia 61. Hivyo conclusion yangu ya kwamba wabunge wamepata kura nyingi kuliko rais wao.

Hiyo ya wabunge kuongezeka kutoka 6 kwenda 23 ilikuwa haina uhusiano na analysis ya hapo juu. Ilikuwa ni information ya ziada tu.

Na hiyo ya CCM kutoka 58 kwenda 67 pia ilikuwa information ya ziada. Ndio maana nikaonyesha effect ya 40% maana mtu mwingine angeshangaa iweje CCM wamepata kura chache lakini viti viongezeke?

Nafikiri umenielewa!

Japo ni nje kidogo ya mada hapo penye nyekundu nimepapenda na ni muhimu nikawakumbusha kuwa kuna ripoti ya hawa wanaojikomba ilituambia kuwa umaarufu wa kikwete umeongezeka ila wa watu wake umeshuka. Uchaguzi huu umetuonyesha kinyume. Hii inadhihirisha kuwa hizi ripoti ni za kupikwa.
 
Back
Top Bottom