Hapana analysis yako ina mushkeli kidogo mkuu, umesahau kuwa CHADEMA haikusimamisha wagombea Ubunge kwenye majimbo mengi tu lakini majimbo hayo hayo bado wananchi walipata fursa ya kumpigia kura Dr. (PhD) Slaa kwenye nafasi ya Urais. Kwa mantiki hiyo basi ni lazima Dr. atakuwa amepata kura nyingi zaidi ya wagombea wote (combined) wa viti vya Ubunge kupitia CHADEMA.
Mkuu,
Asante, hiyo ni valid point na ndio maana ya analysis maana unaangalia pande zote na kujua kwanini jambo fulani liko hivyo? Lakini kama nilivyoandika awali, matokeo hayo kwa CHADEMA yalitegemewa kwasababu hizo ambazo tumezitaja. Ila hilo la wabunge wa CCM kuwa na kura nyingi kuliko JK binafsi sikulitegemea.