Kiungani,
Hapo juu hesabu zako zimenichanganya na nimeshindwa kukuelewa.
Nilichoandika ni kwamba inaelekea kwenye ubunge CHADEMA wamepata kura chache kuliko za urais. Kitu ambacho nilitegemea maana Slaa alikuwa maarufu kuliko wabunge wake. Kama wana viti 23 katika 102 ina maana wana around 23% ya kura za ubunge. Lakini kwasababu unatoa kura za vyama vidogo (kwasababu havishiriki mgao wa viti maalum kwa sababu ya kukosa at least 5% ya kura) basi hiyo asilimia 23 inashuka na kuwa chini ya asilimia 23. Ndio maana nika conclude kwamba wabunge wamepata kura chache kuliko rais wao maana Slaa alipata zaidi ya 26%
Upande wa CCM, kama wana viti at least 67 ina maana wamepata kura around asilimia 67 za wabunge wakati rais wao alipata kura asilimia 61. Hivyo conclusion yangu ya kwamba wabunge wamepata kura nyingi kuliko rais wao.
Hiyo ya wabunge kuongezeka kutoka 6 kwenda 23 ilikuwa haina uhusiano na analysis ya hapo juu. Ilikuwa ni information ya ziada tu.
Na hiyo ya CCM kutoka 58 kwenda 67 pia ilikuwa information ya ziada. Ndio maana nikaonyesha effect ya 40% maana mtu mwingine angeshangaa iweje CCM wamepata kura chache lakini viti viongezeke?
Nafikiri umenielewa!