List ya wanawake kumi wanaoshika vyeo vikubwa bongo

List ya wanawake kumi wanaoshika vyeo vikubwa bongo

Status
Not open for further replies.
Marital status zao?-Mwanamke shupavu ni yule aliyeweza kuitunza ndoa yake,alafu akaweza kuexcel kwenye career pia.

At lease najua
Mama Rwakatare-divorced
Makinda-divorced

Shame.

Asha rose ungemtoa hapo-aliunder perform vibaya sana UN.

I concur
 
Mleta mada umeafanya jambo jema ingawa kama walivyochangia watangulizi wangu inawezekana unawajua wachache sana kati ya wengi tulionao. Lakini pia nilitegemea kuona uliowaorodhesha ni watanzania zaidi kuliko kuchanganya na wazawa na wageni! Lakini pia ungeturuhusu kuongeza wengine ambao hukuwaorodhesha kama akina Prof. Tibaijuka, Mh. Halima Mdee (Mb), n.k.

Ukipenda basi mimi nakuongezea wachache niwajuao; 1. Mama yangu Mazazi (jina kapuni) yeye ni mtanzania ambaye hakuwahi kuajiriwa zaidi ya kujiajiri mwenyewe na kwa kushirikiana na mumewe waliweza kutusomesha sisi watoto wao hata kufikia uwezo wa kuwa kati wa wachangiaji wa mijadala ya hapa jf

2. Dr. Albina Chuwa, yeye ni mkurugenzi mkuu wa kwanza mwanamke wa ofisi muhimu (ofisi ya taifa ya takwimu) hapa tanzania sina uhakika aliishikilia kuanzia lini nafasi hii

3. Dr. Joyce Ndalichako, pale baraza la mitihani (mwenye kujua historia yake, tafadhali)

4. ...................,
 
Marital status zao?-Mwanamke shupavu ni yule aliyeweza kuitunza ndoa yake,alafu akaweza kuexcel kwenye career pia.

At lease najua
Mama Rwakatare-divorced
Makinda-divorced

Shame.

Asha rose ungemtoa hapo-aliunder perform vibaya sana UN.


Anna Makinda hajawahi kuolewa kwahiyo haiwezekani kuwa divorced; ila ana mtoto kama amepata wajukuu sina hakika !! Baba watoto wake sasa ni marehemu!!
 
Pia kuna Prof. Esther Mwaiakambo, ni Profesa na Daktari nguli wa watoto Tanzania, na ni mwanamke wa kwanza nchini kuwa daktari na pia ameongoza taasisi nyingi kwa mafanikio makubwa. Elimu yake haina shaka si uprofesa au udaktari w akupeana kwenye vikao vya chama, huyu mama ni nguli kweli kweli. Hao akina Ana Abdallah hawapaswi kuwemo kwenye orodha hii. lakini ni vyema sana ili uwe na mtiririko ulio sawa taja elimu za wote unaowataja.
 
Marital status zao?-Mwanamke shupavu ni yule aliyeweza kuitunza ndoa yake,alafu akaweza kuexcel kwenye career pia.

At lease najua
Mama Rwakatare-divorced
Makinda-divorced

Shame.

Asha rose ungemtoa hapo-aliunder perform vibaya sana UN.

Aibu yako mama Makinda hajawahi olewa umemdivorce wewe
 
mkuu asante sana kwa uzi huu , unafikirisha japo kuna majina umeyachinjia baharini , mfano MARY CHIPUNGAHELO , labda tunaweza kuondoa porojo za wanawake wakiwezeshwa wanaweza !
 
Nia, shabaha, lengo, dhumuni ya hii post?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
mhh...?nampongeza mwandishi kwa kuibua mawazo haya kama heshima kwa wanawake. Pamoja na hayo kuna watu kadhaa ambao hajawataja ambao wangefaa kuwa katika 10 yake bora: Prof.anna tibaijuka ni mmoja wao-un-habitat .halafu tusisahau pia hawa:mama maria nyerere,mama siti mwinyi,na sasa mama salma kikwete.salute!




wamefanya nini hawa cha maana ikulu?? Wameharibu ikulu hawa! Labda huyo mwingine umeona sifa yake ya kuingiza steratour bear enzi zetu...!
 
wamefanya nini hawa cha maana ikulu?? Wameharibu ikulu hawa! Labda huyo mwingine umeona sifa yake ya kuingiza steratour bear enzi zetu...!

Pamoja sana mkuu.Hawa "ma-First Lady" wana mchango wao-Kuishi tu pale ikulu na kumfanya rais awaze changamoto zinazowakabili wananchi wake badala ya kuwaza amfurahisheje mama watoto wake, si kazi ndogo.Pongezi kwao hawa ma-First Lady-kwa kujua wajibu wao kwa umma.
 
Mh! ovyoo yani ktk hii list nadhani namba moja ni huyu mama Prof Tibaijuka michango yake ni zaidi ata ya nanii yuhu yani UNHABITAT sio mchezi DR migiro pale UN nadhani alikua km secretary
 
Mbona hayupo ktk list Salama Jabir? Huyu nae jasiri jamani.
 

JUL302013


WANAWAKE wengi nchini wameshika vyeo mbalimbali vya juu serikali au kwenye taasisi binafsi. Wafuatao ni wanawake 10 ambao wanakalia au wamekalia vyeo hivyo hapa nchini kama walivyomulikwa na Elvan Stambuli.

JULIET KARIUKI
HUYU ni Mkuruggenzi Mtendaji wa kwanza mwanamke katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) . Uteuzi wake ulifanywa na Rais Jakaya Kikwete Aprili 12 mwaka
huu na akakabidhiwa ofisi siku hiyohiyo.

Bibi Kariuki ana shahada ya kwanza ya sheria na ya uzamili, kwenye sheria ni mtalamu wa ubia kati ya serikali na watu binafsi (Public Private Partnership). Aliwahi kufanya kazi katika Chama Cha Mabenki ya Afrika Kusini.


MIZINGA MELU
NI Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC tangu Machi 20 mwaka
huu. Alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Lawrance Mafuru. Ni mzaliwa wa Zambia katika Kijiji cha Mazabuka na ana shahada ya juu ya biashara (MBA), Zambia National Commercial Bank na Standard CharteredBank.


SAUDA S. RAJABU
NAYE ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa juu wa Mkurugenzi Mkuu na Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Ndege ya Precision Air hapa nchini. Alianza kutumikia nafasi hiyo Machi Mosi, mwaka
huu baada ya aliyekuwa akikalia kiti hicho, Alfonce Kioko kumaliza muda wake.

Ana shahada ya kwanza ya biashara na sasa yupo mbioni ‘kuchimbua’ shahada ya juu ya biashara. Amewahi kufanya kazi katika mashirika mengine ya ndege kama vile
Kenya Airways na ya Rwanda na Burundi.


ANNE MAKINDA
NI mwanamke wa kwanza nchini kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Samwel Sitta ambaye aliliendesha Bunge kwa msimu mmoja tu mwaka 2005 hadi 2010.
Makinda amevunja rekodi kwa kukaa bungeni kwa miaka mingi kwani alianza kuwa Mbunge wa Jimbo la Njombe mwaka 1975 hadi leo. Tayari ametangaza kung’atuka (2015).


BALOZI LIBERATA MULAMULA
NI Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico. Amewahi kuwa balozi wetu nchini Canada kuanzia mwaka 1999 hadi 2002. Amewahi kuteuliwa kuwa mmoja wa wasuluhishi wa mgogoro wa Rwanda. Ni msomi mwenye shahada ya kwanza na ya pili ya sanaa,alisomea Chuo Kikuu cha St. John’s, Marekani, 1989. (Pichani akiwa na Rais Obama.)


MCHUNGAJI G.RWAKATARE
HUYU ni Mchungaji na kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na mwanzilishi wa shule za St. Mary’s International alizozifungua mwaka 1997.
Licha ya kazi ya kuhubiri Injili, Mama Rwakatare ana chombo cha habari ambacho ni
Praise Power Radio 99.2 FM inayoelimisha jamii na kutoa burudani za kiroho.


GETRUDE MONGELLA
ALIKUWA mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Bunge la Afrika, amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini India 1991 hadi 1992 na akawa Katibu Mkuu katika Mkutano wa Wanawake Duniani uliofanyika Beijing, China mwaka 1995.

Aliwahi kuwa mshauri wa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco na aliwatumikia wananchi wa Ukerewe akiwa ni mbunge kuanzia 2000 hadi 2010 na Februari mwaka 2008 alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya African Press Organization (APO).


ASHA ROSE MIGIRO
Asha-Rose Mtengeti Migiro ni mwanasheria na mwanasiasa. Licha ya kufundisha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mama huyu aliwahi kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania. Lakini kikubwa zaidi ni pale alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Juni 2012. Baada ya kumaliza muda wake Umoja wa Mataifa, Migiro hivi sasa yupo nchini akiongoza kitengo cha Mambo ya Nchi za Nje cha Chama Cha Mapinduzi.


SUSAN MASHIBE
HUYU ni rubani na ni injinia wa ndege, hivyo kuwa mwanamke wa kwanza nchini kuwa na elimu hizo alizopatia Chuo Kikuu cha Michigan, Marekani. Ni Mwanzilishi na kiongozi wa Tanzanite Jet Centre Ltd, kampuni aliyoianzisha mwaka 2003 ambayo sasa inajulikana kama Via Aviation na inajishughulisha na biashara ya mambo ya anga nchini na barani Afrika. Alikutana na Rais Barrack Obama alipokuja nchini hivi karibuni.


JOYCE MHAVILE
NI Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One kuanzia 1994. Amekiongoza kituo hicho cha runinga hadi kushika nafasi ya kwanza kwa ufanisi mwaka jana.

Amebobea kwenye taaluma ya uandishi wa habari. Ni mmoja wa wanawake katika Bara la Afrika walioongoza chombo cha habari kwa mafanikio na kuwa mfano kwa wasichana wanaochipukia hivi sasa katika nchi yetu.




Ndugu yangu nngu007 ninashukuru kwa upeo wako hasa unapowaongelea dada au mama zetu kwa shughuli zao pamoja na elimu. Mimi ninafikri ingelikuwa vizuri kama hiyo orodha yako ingekuwa ya majina kuanzia 15-20!!! Kwa sababu ninaona kama hapa hujawa makini katika kutoa hiyo orodha! Ebu fikiria zaidi kwani wote walotajwa ni sawa kwa uataratibu wako lkn kumbuka prof Tibaijuka ni very senior kwa hao wote na she has delivered something beyond doubt!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom