Mleta mada umeafanya jambo jema ingawa kama walivyochangia watangulizi wangu inawezekana unawajua wachache sana kati ya wengi tulionao. Lakini pia nilitegemea kuona uliowaorodhesha ni watanzania zaidi kuliko kuchanganya na wazawa na wageni! Lakini pia ungeturuhusu kuongeza wengine ambao hukuwaorodhesha kama akina Prof. Tibaijuka, Mh. Halima Mdee (Mb), n.k.
Ukipenda basi mimi nakuongezea wachache niwajuao; 1. Mama yangu Mazazi (jina kapuni) yeye ni mtanzania ambaye hakuwahi kuajiriwa zaidi ya kujiajiri mwenyewe na kwa kushirikiana na mumewe waliweza kutusomesha sisi watoto wao hata kufikia uwezo wa kuwa kati wa wachangiaji wa mijadala ya hapa jf
2. Dr. Albina Chuwa, yeye ni mkurugenzi mkuu wa kwanza mwanamke wa ofisi muhimu (ofisi ya taifa ya takwimu) hapa tanzania sina uhakika aliishikilia kuanzia lini nafasi hii
3. Dr. Joyce Ndalichako, pale baraza la mitihani (mwenye kujua historia yake, tafadhali)
4. ...................,