List ya wanawake kumi wanaoshika vyeo vikubwa bongo

List ya wanawake kumi wanaoshika vyeo vikubwa bongo

Status
Not open for further replies.
Khaa!! List yako haikidhi vigezo. Mbona umewaacha wengi sana? Tena wengine wameisaidia jamii kwa kiasi kikubwa!! Hata uwe na cheo au elimu kubwa kiasi gani na hujaisaidia jamii basi you are NOTHING :bored:


At the apex.... there you find BIBI TITI MOHAMED...wengine hao nafasi zao katika jamii yetu ni mjadala
 
Wapi mama Salma, tibaijukja bila kusahau mama anna.
 
Mama Chakaza, huyu anacheo cha kuwa first lady mwanzilishi wa Chakaza na ni mtaalamu mkubwa wa kupika makande.
 
Last edited by a moderator:
Duh! Hadi Joyce Kiria?! Ngoja niendelee na swaumu...

Mkuu, nimemjumuisha Joyce Kiria kwa sababu ukiangalia kiwango chake cha elimu, huko alikotoka, ukatazama na mambo anayofanya hivi sasa, inaonesha ametumia jitihada kubwa sana kufikia hapo alipo. granted, huwezi kumlinganisha moja kwa moja na hao wenzake wawili, wako viwango tofauti, lakini jitihada yake ni kubwa sana na hana woga! imagine angepata elimu kubwa tangu mwanzo angekuwa wapi hivi sasa?
 
Huyu aliyetoa orodha hii yeye kaona hawa tu? Mbona wapo wengi sana. Anyway, ni mtazamo wake tu!
 
Dr. Chijoriga, mwenyekiti bodi ya wakurugenzi TRA na mkuu UDSM School of Business kwa muda mrefu. Elimu wala uhitaji kupepesa

Mkuu nadhani uko nje ya nchi. Chijoriga alishatolewa siku nyiiingi kwenye uenyekiti wa Bodi. Mwenyekiti wa Bodi ya TRA kwa sasa ni Mzee Mchomvu.
 
Huyu nae ni kwa vile amevizia Salma yuko Lindi akahakikisha JK hapigi short time analala usiku kucha nyumbani kwake?

Bwana sitaki kucheka. Sasa unadhani kwa rais kulala kwako ni issue ndogo? Lazima uwe mwanamke wa shoka tena mwenye mvuto.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Listi hii imekaa kishoga zaidi unapomtaja raia wa Zambia mbona kuna wengi tuu kama tukigusa nje ya mipaka?Kama Liberata kuwa balozi ni ishu...?Mongella mwenyewe kakumbwa na likashfa akafukuzwa huko alikokuwa anahudumu kaja kuangukia aibu nyingine kuu ya kupigwa chini ubunge na mtu asiyekuwa maarufu hata uongozi hakuwa na uzoefu!
 
Bwana sitaki kucheka. Sasa unadhani kwa rais kulala kwako ni issue ndogo? Lazima uwe mwanamke wa shoka tena mwenye mvuto.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Blandina Nyoni, kamishina TRA and former PS Health. Yeye je? Naona ana afadhali kuliko Ana Abdalah aliyevunja ndoa ya mwenzake na kuondoka na Msekwa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mbona wako wengi tu na wanafanya makubwa lakini hawajamulikwa na vyombo vya habari? Hawa ni kwa sababu wako 'machoni' na 'midomoni' mwa watu. Lakini tukiamua kuwataja hawa watakuwa 'sisimizi'. Hao wanaotajwa sasa hivi wameongeza nini katika kuifanya Tanzania 'a better place to live'..?
 
Mh.anna makinda amekuwa mbunge wa njombe kusini kuanzia mwaka 1995 na siyo mwaka 1975 kama ulivyoeleza.hayati makwetta ndiye aliyekuwa mbunge mwaka 1975.

Unajua unachokiandika au umekurupuka tu kama umetoka chooni? Unabsha nn sasa? Makinda ndo mbunge mkongwe bungen kwa sasa had mwaka 2015 atakuwa na miaka 40 ya ubunge toka 1975! Alikuwa mbunge baada ya kumaliza shule tu IDM mzumbe wakaigawana Njombe na mwalimu wake makweta. Wote walikuwa wabunge toka mwaka 1975
 
sawa hongera kwa kuwataja hao ingawa wako wengine kibao.
 
Umemuacha mama mkulu wa kaya : anasifa za kufunga barabara kwa saa kadhaa kumpisha apite na pia kukutana na michele obama & laura bush huku akisoma hotuba kama imla au pengine shairi la kumaliza shule ya msingi wakati anajua fika kuwa yuko kwenye mkutanao wa kimataifa na dunia nzima inamtizama kwa ung'eng'e wake wa kuunga unga na super glue / ulimbo. sema tz nchi yenye maajabu ya kipekee duniani.

JF kweli ina mambo,utake usitake utacheka tu........haya bhana we mzodoe mama yetu tu ipo siku atakijua vizuri,kwani si miaka kumi bado haojaisha.
 
Hapo kwa Mchungaji Lwakatare umekosea mleta mada ....
 
Blandina Nyoni, kamishina TRA and former PS Health. Yeye je? Naona ana afadhali kuliko Ana Abdalah aliyevunja ndoa ya mwenzake na kuondoka na Msekwa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Kumbe huyu alikuja hifadhiwa huku .....ma doctor wana taarifa hizi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom