Recta,
..Mwalimu Nyerere aliendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM hata baada ya kuondoka ktk nafasi ya Raisi wa Muungano mwaka 1985.
..Mzee Mwinyi aliendelea kuwa Makamu wa Mwenyekiti CCM, huku Rashidi Kawawa akiwa Katibu Mkuu.
..Mwalimu alipong'atuka Uenyekiti wa CCM alimpendekeza Mzee Mwinyi kuwa Mwenyekiti, na Mzee Rashidi Kawawa kuwa Makamu Mwenyekiti.
..nimeangalia kwenye Wikipedia wanasema Mwalimu alingatuka CCM mwaka 1990.
..statement inayobishaniwa hapa kuna uwezekano mkubwa sana ilitolewa na Mwalimu ktk hotuba yake ya kung'atuka Uenyekiti wa CCM.
..ilikuwa hotuba nzito iliyosheheni historia ya Tanganyika,Tanzania,Tanu, na CCM. ilikuwa ni kama hotuba ya wosia wa Mwalimu kwa wana-CCM wenzake, na wa-Tanzania kwa ujumla.
..katika hotuba hiyo Mwalimu alifanya kazi kubwa kuelezea historia na mchango wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa "simba wa vita" katika harakati za uhuru, na uongozi wa Tanganyika na Tanzania.
..Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alitoa machozi wakati akimuelezea Mzee Kawawa kama kiongozi aliyemsaidia yeye Mwalimu tangu kabla ya uhuru, na ambaye wakati mwingine alitwisha lawama zilizopaswa kuelekezwa kwake Mwalimu, kwa serikali, au chama.