Listening Audio Booth:John Malecela: Alichoongea

Listening Audio Booth:John Malecela: Alichoongea

Yeye amelitumikia taifa na CCM with honour, amefika mwisho amestaafu ndio mfano tunaoutaka Tanzania.

Amelitumikia Taifa kwa kweli.

Ukitamka neno "Malecela," watu wanakumbuka utumishi na uzalendo. Lakini pia wanakumbuka "go to hell" na kibaya zaidi "uhuni" wake uliomghafirisha mlezi wake wa kisiasa. "Honor" inapungua.

Kuhusu kuwa mfano wa kuigwa kwa kustaafu nadhani Mzee Malecela amesema jana kwamba aligombea hata mwaka 2005. Sasa huo moyo wa kuigwa kwa kustaafu sijui uko wapi hapo
 
Pato la mwananchi wa kawaida wa Mtera ni shilingi ngapi kwa Mwaka, je pato hilo hilo ndio wewe na Malecela mnalipata kwa mwaka?

- Ni kazi ya mbunge kujua pato la wananchi wake? what this has anything to do na press yake ya jana kama kichwa cha hii mada?

Mkuu kama hakuna hoja za kuelimishana taifa, basi naomba ku-retire huu mjadala.

Thanxs

FMES!
 
Amelitumikia Taifa kwa kweli.

Ukitamka neno "Malecela," watu wanakumbuka utumishi na uzalendo. Lakini pia wanakumbuka "go to hell" na kibaya zaidi "uhuni" uliomghafirisha mlezi wake wa kisiasa. "Honor" inapungua.

Kuhusu kuwa mfano wa kuigwa kwa kustaafu nadhani Mzee Malecela amesema jana kwamba aligombea hata mwaka 2005. Sasa huo moyo wa kuigwa kwa kustaafu sijui uko wapi hapo

- hopefully kuna siku m-Tanzania atakuja na mapya aginst Malecela maana haya yamekuwa kama wimbo wa taifa na hayamsaidi mwananchi wa kawaida kule kijijini anything, nilitegemea mapya kwa mtu kama wewe, samahani naomba sasa ku-retire.

CCM juu na idumu zaidi.

FMES!
 
- Ni kazi ya mbunge kujua pato la wananchi wake?

FMES!

Kama sio kazi ya mbunge kujua hilo, nani anapaswa kujua. Je wewe kama Mwanamtera, unajua pato la wastani la wananchi la jimbo lenu? Na kama hujui, umeshawahi kuuliza kwa viongozi wa jimbo lako? Kama sivyo, hii inaonyesha kwamba jimbo hilo halina mipango yeyote ya maendeleo. Mipango ya maendeleo haiwezi kupangwa bila kujua pato la wastani la wananchi wa sehemu husika!

Pia ulizungumzia hospitali, shule, vitabu na barabara toka Dodoma hadi Mvumi.

Je hizo shule na hospitali zinahudumia wananchi wangapi kwa ujumla. Na vipi ratio ya daktari kwa mgonjwa na mwanafunzi kwa mwalimu? Vipi kuhusu swala la madawati.

Je hiyo barabara toka Mvumi kwenda Dodoma, imesaidia vipi kuboresha maisha ya Wanamtera? Je hiyo tofauti imeshakuwa quantified?
 
Last edited by a moderator:
Hujui pato la wastani la wananchi la jimbo lenu, okay okay. Hii inaonyesha kwamba jimbo hilo halina mipango yeyote ya maendeleo. Mipango ya maendeleo haiwezi kupangwa bila kujua pato la wastani la wananchi wa sehemu husika!

Pia ulizungumzia hospitali, shule, vitabu na barabara toka Dodoma hadi Mvumi.

Je hizo shule na hospitali zinahudumia wananchi wangapi kwa ujumla. Na vipi ratio ya daktari kwa mgonjwa na mwanasunzi kwa mwalimu? Vipi kuhusu swala la madawati.

Je hiyo barabara toka Mvumi kwenda Dodoma, imesaidia vipi kuboresha maisha ya Wanamtera? Je hiyo tofauti imeshakuwa quantified?

- Mkuu ninaweza kukupatia namba umpigie simu mkuu, maana haya maswali anaweza kujibu yeye mwenyewe mbunge wetu.

Respect!

FMES!

Nna mimi nimechelewa mpaka mjadara umehama kutoka hutuba yake na kuwa yeye mwenyewe. kwa maoni yangu sijaona kitu cha maana hata cha wana CCM wenyewe kushaniglia kwani hutuba haikuwapa watu kitu walichotegemea kupokea isipokuwa kwa mkuu mmoja aliyetabiri maneno ataayosema na ndio hayo aliyosema.

Sijaona kama anakemea ufisadi, zaidi ya kutoa statement ya jumla kuwa mafisadi wameshapelekwa mahakamani na kama kuna mwingine basi utolewe ushaidi, huyu anasema bila hata haibu kama alivyokuwa anasema Mkapa, ushaidi upo kuwa RA alihusika kwa 100% bado anasema mafisadi ni waliopelekwa mahakamani na kama kuna wengine utolewe ushaidi? ushaidi gani anaoutaka zaidi ya unaotolewa kila siku kwenye vyombo vya habari?

Hoja ya RD imeongelewa bungeni kwahiyo hakuna kuiongelea tena, hii sio haki kwani bungeni hawakumaliza yote, kuna yaliyoachwa kwa usalama wa viongozi wa CCM tunayataka wayaweke wazi ili watu wajue kuwa hule mradi ulukuwa wa viongozi wa CCM.

huyu mzee naona kwa mawazo yangu angeachana na siasa kwani amepitwa na wakati, kumshauri raisi kukemea vyombo vya habari kwa wakati huu sio sahihi labda kwa vyombo uchwala vya RA ambavyo vinatetea ufisadi kwa nguvu zote.

Kwa vyombo ya habari vya RA, wahariri wake siku moja historia ya tanzania itawahukumu kwa mnayoyafanya sasa bila kujali masirahi ya nchi sababu ya mshahara, kumbukeni hayo magazeti yenu yanaifadhiwa kuna siku mtatafutwa kujieleza mlipata wapi nguvu kubwa namna hiyo ya kutetea ufisadi
 
mkuu FM ..unaonaje ushujaa wa malecela kusamehe kikwete kwa mbinu chafu alizotumia dhidi yake.......?...ndio maana nikasema atakuwa na roho ya ajabu ya kusamehe ..inaweza ikakaribia ya mandela!

au baada ya kikwete kuwachimba mkwara viongozi waandamizi wastaafu kwa kutofautiana naye,na kumkosoa hadharani na yeye ameamua kuwa kwenye kundi la the darling wa muungwana kina kawawa na mwinyi..unlike warioba,sumaye,watendaji wastaafu[butikus/kitines na salim/c;eopa[ambao wameamua kukaa kimya]..
 
- Mkuu ukweli ni kwamba kuna political miscalculations nyingi sana ambazo Mzee, alizifanya regarding ule uchaguzi ndio maana aliposhindwa haikuwa tatizo sana kwake zaidi tu ya wananchi wasioelewa what went down na ambazo hazikusemwa wazi, infact Mh. Kikwete did all he could kumpa heshima mzee, lakini hakuweza kuelewa what he was up against ndio maana nikampa rais wa sasa jina la Muungwana kwa sababu ya ustaarabu wake mwingi kwenye ule uchaguzi, kama sio yeye it could have been real ugly.

- Ninaamini with time mzee amekuja kuelewa kwamba it was his political mistake and manouvers, kitu ambacho ni cha kawaida sana kwenye siasa kwa wanasiasa waliokomaa kama yeye. Baada tu ya kupitishwa kwa muungwana pale Chimwanga, Muungwana aliwakimbia hata walinzi wake na kwenda Kilimani kwa mzee na kuka naye chini for two hours na kusawazisha tofauti, na that was it.

Thanxs!

FMES!
 
leo Mtera ndio jimbo pekee Tanzania nzima lenye zahanati na shule kwenye kila kata ya jimbo.

FMES

Oh yeah? Including constituencies in Dar? Are you positive on the authenticity of this statement?

Just some fact checking, it does not ring true to me.
 
Mkuu FMES,

hongera sana umefanya kazi kubwa sana ya kusimama kati na kuweka mambo sawa hapa kwenye hii thread. In fact nilikuwa busy na madaftari yangu hapa kwahiyo kuingia huku ilikuwa kama kituo cha polisi. Lakini sasa niko huru sina deni na washika chaki wangu hapa.

Kusema ukweli Makamu Mstaafu ni kisima cha busara, maneno yake ni msumari wa moto ambao hata ukiangalia hapa JF wachangiaji wanashindwa kuja na hoja za kuyabomoa aliyoyasema. Ni wazi kabisa wachangiaji wamemalizwa na hotuba ile kiasi cha kwamba wamekosa kabisa cha kuonngea. Ushahidi uko wazi, hebu angalia walivyoendesha mjadala mrefu wa 'kung'atuka' baada ya kushindwa kujadili maneno yake. Wapo waliojaribu kuleta tafsiri zao kana kwamba hatukusikia kwa masikio yetu alichokiongea.

Chama Cha Mapinduzi ni SAFI na kimesheheni wanasiasa waliobobea kwenye hekima na busara. Sasa yule ambaye alitarajia Mzee malecela ataongea yale anayotaka ya mfurahishe yeye amenoa step, Mzee Malecela anaongea kwa kujali maslahi ya chama chake ambacho anakipenda kwa dhati kabisa ya moyo wake.

I love CCM
 
Naam, Mkuu Pundamilia. Na busara hii ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo.

Amandla........
 
Naam, Mkuu Pundamilia. Na busara hii ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo.

Amandla........

Kweli Fundi, busara ya kukisujudu Chama na kukosa uzalendo kabisa wa Taifa lako, kukumbatia mafisadi eti kulinda heshima ya chama! No wonder sasa kimegeuka kuwa chaka la mafisadi
 
FMES

Oh yeah? Including constituencies in Dar? Are you positive on the authenticity of this statement?

Just some fact checking, it does not ring true to me.

- Mkuu mimi ni mwananchi wa Mtera, ninakwambia kwamba jimbo langu lina zahanati na shule katika kila kata ya jimbo, sasa ninaweza kukupa namba ya simu ya mbunge wangu umpigie akusaidia, kama nilivyompa Mkulu mwingine jana, ya Dar mimi siyajui mkuu.

Respect.

FMES!
 
Mkuu FMES,

hongera sana umefanya kazi kubwa sana ya kusimama kati na kuweka mambo sawa hapa kwenye hii thread. In fact nilikuwa busy na madaftari yangu hapa kwahiyo kuingia huku ilikuwa kama kituo cha polisi. Lakini sasa niko huru sina deni na washika chaki wangu hapa.

Kusema ukweli Makamu Mstaafu ni kisima cha busara, maneno yake ni msumari wa moto ambao hata ukiangalia hapa JF wachangiaji wanashindwa kuja na hoja za kuyabomoa aliyoyasema. Ni wazi kabisa wachangiaji wamemalizwa na hotuba ile kiasi cha kwamba wamekosa kabisa cha kuonngea. Ushahidi uko wazi, hebu angalia walivyoendesha mjadala mrefu wa 'kung'atuka' baada ya kushindwa kujadili maneno yake. Wapo waliojaribu kuleta tafsiri zao kana kwamba hatukusikia kwa masikio yetu alichokiongea.

Chama Cha Mapinduzi ni SAFI na kimesheheni wanasiasa waliobobea kwenye hekima na busara. Sasa yule ambaye alitarajia Mzee malecela ataongea yale anayotaka ya mfurahishe yeye amenoa step, Mzee Malecela anaongea kwa kujali maslahi ya chama chake ambacho anakipenda kwa dhati kabisa ya moyo wake.

I love CCM

- Mkuu Pundamilia, tupo pamoja sana mkuu saafi sana.

FMES.
 
..mkuu FMES maelezo yako yamekamilika....lakini kuna jambo lina nikera sana ..nikibahatika kukaa na watu wenye nafasi huwa pia napenda kuwaambia!!

hawa wazee wetu hawaandiki vitabu ,tutakuja kupoteza historia za taifa na maisha ..kwani miaka kumi ijayo waazilishi wengi watakuwa wamekwenda ..tutaanzia wapi???

tumepoteza nafasi ya nyerere kuandika kitabu [kwa mkono wake mwenyewe kuhusu maisha yake]

naomba tusaidie tunahitaji hawa wazee waandike vitabu kuhusu maisha.

watu kama ...

1.john malecela
2.salim ahmed salim
3.kawawa
4.msuya
5.mzee mwinyi
5.warioba
6.mama maria

Hawa inabidi washauriwe kuandika vitabu..sikupenda kitabu cha kawawa kwa kuwa kipo too shallow na ameandika prof magoti...kwani kama kawawa yupo hai ingebidi dr magoti amuongoze aandike kwa mikono au muongozo wake mwenyewe....

pia nimependa kusikia dr bilal anafundisha dodoma ...ningefurahi kuona wanasiasa wasomi kama malecela na salim,warioba wawe wanatoa mihadhara kwenye vyuo vikuu vya mbalimbali.........
 
- Sijui kwa viongozi wengine, nijuavyo watoto wa mzee Malecela, sasa hivi wanamalizia vitabu na video documentaries kuhusiana na historia form baba yao, kwa hiyo naamini when the time is right watavitoa wazi, ni moja ya faid kubwa ya kuwa na watoto wasomi waliobobea kama huyu mzee, kwa hiyo is just the matter of time.

- Nimewahi kuwashawishi watoto wa wazee kama Kawawa, Kingunge, Kimbau, Msuya, Mwakawago, na wengineo wenye watoto wasomi on this ishu hopefully watafuata nyayo za wenzao wa Trekta.

FMES!

FMES!
 
philemon mikael said:

pia nimependa kusikia dr bilal anafundisha dodoma ...ningefurahi kuona wanasiasa wasomi kama malecela na salim,warioba wawe wanatoa mihadhara kwenye vyuo vikuu vya mbalimbali......

Phillemon Mikael,

..ni kweli kabisa wanasiasa uliowataja wanapaswa kuandikia vitabu kuhusu ushiriki wao ktk siasa.

..wengine ni askari na makamanda wa JWTZ walioshiriki opereshen mbalimbali.

..tumewapoteza Maj.Gen.John Walden "black mamba", Brig.Gen.Makaranga, na Col.Mahfoudh, ambao walishiriki kwa kiwango kikubwa sana ktk harakati za ukombozi wa Msumbiji.

..makaburu wa afrika kusini, pamoja na walowezi wa Zimbabwe, wako ktk harakati kubwa sana za ku-document experiences zao wakati wakipambana dhidi ya vyama vya ukombozi vya afrika kusini,zimbabwe,msumbiji,na angola.angalia vitabu vyao hapa

..hata makamanda walioongoza vita vya Kagera wako waliopoteza maisha, na vita ile haijawa documented inavyostahili.

..wengine wanaopaswa kuandika vitabu ni wataalamu wetu ktk fani mbalimbali. tena kwa mtizamo wangu nadhani hawa wana umuhimu kuliko wanasiasa.

..nimesoma kitabu kilichoandikwa na Proffesor Joseph Shija mtaalamu bingwa wa upasuaji akielezea historia ya kazi zake. vitabu vya aina hiyo vinaweza kuwa-encourage watoto vijijini kufuata nyayo za Proffesor Shija.
 
- Sijui kwa viongozi wengine, nijuavyo watoto wa mzee Malecela, sasa hivi wanamalizia vitabu na video documentaries kuhusiana na historia form baba yao, kwa hiyo naamini when the time is right watavitoa wazi, ni moja ya faid kubwa ya kuwa na watoto wasomi waliobobea kama huyu mzee, kwa hiyo is just the matter of time.

- Nimewahi kuwashawishi watoto wa wazee kama Kawawa, Kingunge, Kimbau, Msuya, Mwakawago, na wengineo wenye watoto wasomi on this ishu hopefully watafuata nyayo za wenzao wa Trekta.

FMES!

FMES!

hiyo itakuwa safi san...wenzetu wa kenya ...hata wakiwa wabunge tu inatosha kuwafanya waandike VITABU...hata wasaidizi wa viongozi kule huandika vitabu...hapa tumelala sana..sijui ni uvivu wa kusoma....nadhani kuna idara serikalini ya vielelezo ingetakiwa pia iwe mstari wa mbele kuweka vielelezo kwa faida ya baaadaye......

wanaotaka kuandika kitabu cha mwalimu[true story] pia watakuwa hawajachelewa kwani bado mkewe yupo hai na watu waliofanya naye kazi kwa karibu!!!
 
Back
Top Bottom