Lisu wa CHADEMA atasababisha atokee Lisu mwingine wa CCM. Ndio maana tunahitaji Lisu awe Mwenyekiti.

Lisu wa CHADEMA atasababisha atokee Lisu mwingine wa CCM. Ndio maana tunahitaji Lisu awe Mwenyekiti.

Watu kuimba wanaimani na Lowasa ndio kumzomea Kikwete?

Unazungumzia tukio la mwaka gani Mkuu?
Wewe unaubishi wa kitoto alafu unabishana ili ushinde na sio kujifunza

Kuimbiwa hatuna imani ndo zomea zenyewe hizo
Wewe unaona ni sawa mwenyekiti wa ccm taifa kuimbiwa vile mbele ya kadamnasi nchi nzima inaona kama unaona ni sawa basi unasafari ndefu sana kifikra
 
Wewe unaubishi wa kitoto alafu unabishana ili ushinde na sio kujifunza

Kuimbiwa hatuna imani ndo zomea zenyewe hizo
Wewe unaona ni sawa mwenyekiti wa ccm taifa kuimbiwa vile mbele ya kadamnasi nchi nzima inaona kama unaona ni sawa basi unasafari ndefu sana kifikra

Mkuu.
Ule ni wakati wa uchaguzi.

Sheria gani iliwazuia kufanya hivyo? Kumuimbia mtu wanayeona anafaa?

Role ya Mwenyekiti kwenye huo mkutano ilikuwa ni nini?
 
Kwa Hotuba ya leo ni wazi Mbowe hagombei ndio maana akasema, nikiona chama kinaenda kuzamishwa, naingia mzigoni. Hilo ni jibu tosha kwamba mpaka sasa hajaona chama kikizama. Huwezi kufanya analysis ya masaa 48 ili ujue kinazama au hakizami. Hiyo analysis tayari imekwishwa fanywa ndio maana Lissu kaingia mzigoni. Kinacho fanyika sasa ni ku- nunua muda tu ili pressure ya mashabiki wake itulie, na hili ni kawaida.
 
Kwa Hotuba ya leo ni wazi Mbowe hagombei ndio maana akasema, nikiona chama kinaenda kuzamishwa, naingia mzigoni. Hilo ni jibu tosha kwamba mpaka sasa hajaona chama kikizama. Huwezi kufanya analysis ya masaa 48 ili ujue kinazama au hakizami. Hiyo analysis tayari imekwishwa fanywa ndio maana Lissu kaingia mzigoni. Kinacho fanyika sasa ni ku- nunua muda tu ili pressure ya mashabiki wake itulie, na hili ni kawaida.

Mimi nataka agombee watu Wachague wenyewe.
Nataka nione mtazamo, akili na maoni ya CHADEMA kwenye huu uchaguzi kwa vitendo
 
CHADEMA ilitakiwa iongozwe na mwanamke na wao wawe na Samia wao sema tu kina Mdee na Bulaya walikengeuka🐼
 
Umeelezea vizuri sana Mkuu

Kupitia Chaguzi hii ya Chadema Mwaka huu, CCM inatumia mbinu zote kuhakikisha Lissu hawi Mwenyekiti wake.

Lissu asipokuwa Mwenyekiti, ina maana CCM haitatumia nguvu kubwa mwakani kushinda Uchaguzi Mkuu

Kwanini,
Chadema itaendelea kuzorota hivi hivi, kwani Mwenyekiti aliyehudumu miaka 20 hatokuwa na jipya ya kuifanya CCM ishindwe

Pili, Lissu hatokuwa Lissu huyu tena.
Morale pamoja na Ari itakuwa imeshuka, hivyo anaweza kuhama Chama kabisa ama kupumzika Siasa
 
LISU WA CHADEMA ATASABABISHA ATOKEE LISU MWINGINE WA CCM. NDIO MAANA TUNAHITAJI LISU AWE MWENYEKITI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kwa Sisi Watibeli ambao kiasili ni wanafalsafa, wanasaikolojia, wanasosholojia, na kama haitoshi Majasusi wa kuzaliwa. Tunajua kuna kanuni za vita, mapambano na michezo ambayo ili mtu ashinde na ambadilishe adui lazima atumie baadhi ya Kanuni na Sheria hizo.

Mojawapo ya Kanuni ambayo Leo Mtibeli nitakupatia sio tuu itumiwayo na watu Wakubwa Bali hata wewe unaweza kuitumia katika shughuli zako za kila siku ni hii hapa;

"Muunde Mhusika anayefanana karibu kila kitu na adui yako kisha mtumie kubadilisha uwanja wa mapambano au vita. Utashinda. KANUNI zingine za vita zikiwa constant"

Mfano,
Wakati Barcelona wanaringa na Leone Messi. Real Madrid iliwapasa wamtafute Messi mwingine ili waweze kukabiliana na Messi wa Barcelona. Hapo ndipo Cr7 alipoonekana anaweza ku-fit hiyo nafasi. Hii ni ili kupambana na kuleta ushindani Mkubwa baina ya Real Madrid Vs Barcelona.

Mfano2.
Kibiashara,
Wakati Marekani, Japan na nchi za magharibi zikiwa zinatawala soko la teknolojia duniani. Taifa la china lilijua nguvu ya mbinu hii ya kivita na mapambano ambayo ipo accuracy kwa asilimia 90.
Unatengeneza bidhaa inayofanana na bidhaa ya adui inaingia sokoni. Vita inaendelea. Ushindi kupatikana kuna uhakika wa asilimia 90.

CHADEMA 2010 ilimsimamisha Wilbrod Slaa kuwania kiti cha Urais kupitia Tiketi ya CHADEMA. Moto wa Slaa ulikuwa Mkali Sana. Jakaya Kikwete aliyekuwa anatetea kiti chake tumbo lilikuwa linafukuta. CCM wakaona hapa tukileta Mchezo Dola tunaachia.
Falsafa za CHADEMA wakati huo zilikuwa kukemea ufisadi, ubadhirifu wa Mali za Umma, demokrasia, Uhuru na maendeleo.

Wilbrod Slaa ndiye aliyesababisha John Pombe Magufuli apitishwe kimazabe zabe pasipo hata yeye mwenyewe kujua imekuwaje amepewa Tiketi ya Urais na chama chake. Kwa sababu JPM hakuwa na nguvu Wala Jina kubwa kuliko washindani wake akina Edward Lowasa na Bernard Membe.

Kitu pekee ambacho Magufuli alikuwa anacho ambacho kilimfanya awashinde wenzake ni Falsafa zake ambazo kwa ukaribu zilikuwa zinakaribiana na Upinzani yaani CHADEMA.
Kumbuka hapo nyuma, CCM kupitia Kikwete imekoswakoswa kuvuliwa madaraka na Wilbrod Slaa kupitia CHADEMA.

Watu walikuwa wameanza kuwa na imani na CHADEMA, falsafa na Sera za CHADEMA zilikuwa zimeangusha mioyo ya Watanzania wengi.

Unafikiri CCM wangefanya nini? Nini wafanye kuwavusha katika Kipindi kile ambacho wakileta Mchezo au kujifanya hawaelewi watadondoka.

Harakaharaka, jamani! Wanazengo, makada! Wote mnajua Hali ilivyo huko mtaani. Wananchi mnawaona wanavyotuchukulia, Imani Yao kwetu imeshuka kutokana na baadhi ya Tabia mbaya zinazofanywa na baadhi yetu. Huu sio Muda WA kulaumiana. Hapa tunapaswa tumchague mtu mwenye falsafa na Sera na Msimamo kama ya kwao. Lakini yupo huko kwetu.

Mtu huyo si mwingine zaidi ya John Pombe Magufuli.
Ndipo Hayati Magufuli akapatamo nafasi kuokoa jahazi na kushinda hiyo vita. Akawa game changer.

Magufuli anamapungufu ya kutumia ubabe, au kutopenda kusikiliza wengine lakini sifa ya uchapakazi, kukemea ufisadi na majizi, kupambana na wahujumi uchumi hata kama sio kwa asilimia Mia lakini angalau ilitosha kuridhisha Umma. Na alikuwa silaha muhimu ya CCM kushinda vita Ile.

Sasa wapinzani hapo wakapoteana, kwa sababu hoja walizokuwa nazo CCM wamemteua mtu wa aina Yao. Yaani dawa ya Moto ni Moto.
Kufikia hapo CHADEMA ikawa imepoteana isijue chakufanya.

Mbaya zaidi ikaingizwa zaidi mkenge kwa kupewa Lowasa ambaye miaka nenda Rudi Miaka Rudi walimtangaza kama fisadi. Leo wakampokea. Hiyo ikaondoa uaminifu wao, Tabia Yao, hulka Yao, utambulisho wao ambao walijinadi kwa wananchi.

Sisi Majasusi kuna kanuni inasema;
" If you lose Money , you lose nothing.
If you lose Health, you lose something.
But if you lose character you lose everything"
Kwa wasiojua kimombo, kanuni hiyo inaeleza kuwa "ukipoteza Pesa au Mali haujapoteza chochote, afya yako ikidorora au kupotea umepoteza kitu Fulani. Lakini ukipoteza utambulisho(uhusika) umepoteza kila kitu"

Tangu siku Ile CHADEMA watapoteza utambulisho wao. Hawajulikani wao ni kina Nani hasa. Na wao wenyewe hawajielewi au hawajijui wanataka kitu gani.

Huo ulikuwa ushindi Mkubwa wa CCM ambao hawakuwahi kuupata popote pale tangu siasa za ushindani zilivyoanza hapa nchini.

2015 Ingawaje watu wengi waliona upinzani wameshinda na Kupata Kura nyingi na baadhi ya wabunge na vinafasi vya hapa na pale.

Wengine wakajitapa kuwa ndio mwaka ambao upinzani umeshinda kuliko wakati wowote lakini kwa Sisi Watibeli, wanafalsafa, vionambali tulijua yaelewa matokeo katika uhalisia wake kuwa CCM ilishinda kwa kishindo kikubwa Sana

Kuna ushindi wa aina mbili,
1. Ushindi wa nje, macho
2. Ushindi wa ndani Kabisa.

Ushindi wa macho ni ule unaoonekana kwa mfano kupambana na adui ukampiga, ukaharibu Majengo na miundombinu huo ni ushindi wa nje au machoni. Kuteka eneo na kulitawala

Lakini ushindi wa ndani ndio ushindi unaokusudiwa zaidi.
Ushindi wa ndani huo ndio ushindi halisi.
Kuteka hisia za watu. Kuteka ngome za moyo za adui, kuangusha ujasiri na tumaini la watu. Kuharibu mapenzi ya adui yako katika mioyo ya watu. Huo ndio ushindi ambao CCM ulishinda siku Ile.

CHADEMA kabla ya 2015 walisonga Sana kuiangusha CCM ndani kwa ndani katika mioyo ya Watanzania. Hivyo ilibakia Muda mchache Sana ushindi wa ndani kutoka uwe ushindi wa nje.

CCM kwa sasa Hapana Shaka wanajiamini Sana kuliko wakati wowote ule.

Kwa Sababu wanajua fika ngome ya upinzani imeangushwa kwa kishindo kikuu.

Upinzani ukiteka ngome za mioyo ya watu inauwezo wa kuwaambia waandamane na watu wakatoka na serikali isifanye chochote.

Ingawaje CHADEMA wanaisingizia CCM kutumia mabavu na kutumia Dola lakini haitaondoa ukweli kuwa kama wananchi wangekuwa na mapenzi na CHADEMA wasingehitaji kushawishiwa kuipinga serikali ikiwa inaonea vipenzi vyao CHADEMA.

Changamoto inakuja huwezi mpenda mtu ambaye Hana character. Mtu hupendwa kwa character zake. Ieleweke kwamba mtu huweza kukupenda kwa bad character au Good Character lakini watu wengi hawavutiwi na Tabia za watu zinazobadilika badilika

Ikiwa Lisu atapewa uenyekiti na kwa miaka aliyoonyesha Msimamo isiyoyumba anaweza kuirejesha CHADEMA ya 2010-2015 Jambo ambalo CCM Hilo hawataki litokee.

Na ikiwa CCM watashindwa kumzuia Lisu kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA hapana Shaka mbinu watakayobakiwa nayo ni kumtafuta Lisu mwingine wa CCM ambaye atam- neutralise LISU wa CHADEMA.
Na mbinu hiyo itakuwa perfect kwa asilimia 90%

Mtibeli Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mfumo wa ki-imla wa CCM hauwezi kuruhusu "Lissu" wa CCM akatokea, hilo linawezekana tu CDM.
 
Umeelezea vizuri sana Mkuu

Kupitia Chaguzi hii ya Chadema Mwaka huu, CCM inatumia mbinu zote kuhakikisha Lissu hawi Mwenyekiti wake.

Lissu asipokuwa Mwenyekiti, ina maana CCM haitatumia nguvu kubwa mwakani kushinda Uchaguzi Mkuu

Kwanini,
Chadema itaendelea kuzorota hivi hivi, kwani Mwenyekiti aliyehudumu miaka 20 hatokuwa na jipya ya kuifanya CCM ishindwe

Pili, Lissu hatokuwa Lissu huyu tena.
Morale pamoja na Ari itakuwa imeshuka, hivyo anaweza kuhama Chama kabisa ama kupumzika Siasa

Sahihi kabisa

Lisu
Mfumo wa ki-imla wa CCM hauwezi kuruhusu "Lissu" wa CCM akatokea, hilo linawezekana tu CDM.

Mazingira wakati mwingine hulazimisha mabadiliko ya lazima
 
Sahihi kabisa

Mazingira wakati mwingine hulazimisha mabadiliko ya lazima
Ni kweli, Kuna mabadiriko mengine yanakuwa ni matokeo ya misuguano

Bila kugoma Kwa madaktari wakiongozwa na Dr Ulimboka miaka ile, Watumishi wa afya wasingeboreshewa Mishahara yao
 
Back
Top Bottom