Lisu wa CHADEMA atasababisha atokee Lisu mwingine wa CCM. Ndio maana tunahitaji Lisu awe Mwenyekiti.

Watu kuimba wanaimani na Lowasa ndio kumzomea Kikwete?

Unazungumzia tukio la mwaka gani Mkuu?
Wewe unaubishi wa kitoto alafu unabishana ili ushinde na sio kujifunza

Kuimbiwa hatuna imani ndo zomea zenyewe hizo
Wewe unaona ni sawa mwenyekiti wa ccm taifa kuimbiwa vile mbele ya kadamnasi nchi nzima inaona kama unaona ni sawa basi unasafari ndefu sana kifikra
 

Mkuu.
Ule ni wakati wa uchaguzi.

Sheria gani iliwazuia kufanya hivyo? Kumuimbia mtu wanayeona anafaa?

Role ya Mwenyekiti kwenye huo mkutano ilikuwa ni nini?
 
Kwa Hotuba ya leo ni wazi Mbowe hagombei ndio maana akasema, nikiona chama kinaenda kuzamishwa, naingia mzigoni. Hilo ni jibu tosha kwamba mpaka sasa hajaona chama kikizama. Huwezi kufanya analysis ya masaa 48 ili ujue kinazama au hakizami. Hiyo analysis tayari imekwishwa fanywa ndio maana Lissu kaingia mzigoni. Kinacho fanyika sasa ni ku- nunua muda tu ili pressure ya mashabiki wake itulie, na hili ni kawaida.
 

Mimi nataka agombee watu Wachague wenyewe.
Nataka nione mtazamo, akili na maoni ya CHADEMA kwenye huu uchaguzi kwa vitendo
 
CHADEMA ilitakiwa iongozwe na mwanamke na wao wawe na Samia wao sema tu kina Mdee na Bulaya walikengeuka🐼
 
Umeelezea vizuri sana Mkuu

Kupitia Chaguzi hii ya Chadema Mwaka huu, CCM inatumia mbinu zote kuhakikisha Lissu hawi Mwenyekiti wake.

Lissu asipokuwa Mwenyekiti, ina maana CCM haitatumia nguvu kubwa mwakani kushinda Uchaguzi Mkuu

Kwanini,
Chadema itaendelea kuzorota hivi hivi, kwani Mwenyekiti aliyehudumu miaka 20 hatokuwa na jipya ya kuifanya CCM ishindwe

Pili, Lissu hatokuwa Lissu huyu tena.
Morale pamoja na Ari itakuwa imeshuka, hivyo anaweza kuhama Chama kabisa ama kupumzika Siasa
 
Mfumo wa ki-imla wa CCM hauwezi kuruhusu "Lissu" wa CCM akatokea, hilo linawezekana tu CDM.
 

Sahihi kabisa

Lisu
Mfumo wa ki-imla wa CCM hauwezi kuruhusu "Lissu" wa CCM akatokea, hilo linawezekana tu CDM.

Mazingira wakati mwingine hulazimisha mabadiliko ya lazima
 
Sahihi kabisa

Mazingira wakati mwingine hulazimisha mabadiliko ya lazima
Ni kweli, Kuna mabadiriko mengine yanakuwa ni matokeo ya misuguano

Bila kugoma Kwa madaktari wakiongozwa na Dr Ulimboka miaka ile, Watumishi wa afya wasingeboreshewa Mishahara yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…