Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Kadri siku zinavyoenda mgao wa maji unazidi kuwa mkali, na kwa sehemu kubwa maji hayatoki kabisa zaidi ya wiki mbili na wengine mpaka tatu.
Bei ya maji tunayouziwa mtaani inatisha, kwa jinsi gharama za maisha zilivyopanda tutafika kweli? Dumu moja la lita 20 linauzwa 1,000 mpaka 2,000, lita 1,000 hali ndiyo mbaya kabisa, huku bei inacheza kwenye sh 40,000 mpaka sh 60,000.
Kwa hali hii ni kama vile kuna mtu/watu wanaodhibiti maji yaendelee kutokupatikana ili waendelee kufaidika kwa manufaa yao yenyewe.
Hali ni mbaya, fanyeni kitu, mgao huu unatugharimu sana, hapo hujagusa gharama za bando zinazopanda kila siku pamoja na mgao wa umeme.
Wadau huko mbele kunaendeka kweli?