Leo watz wanakumbuka kifo cha baba wa Taifa Mwl Julius K. Nyerere.Butima ndiko kumbukumbuku zinafanyika kitaifa, viongozi mbalimbali wakitaifa wapo hapa, brudani za ngoma zinaendelea na wakati wowote mh! Rais wa Jamhuri ya Munnganio-Kikwete atafika hapa badi sijafahamu kama atalihutubia taifa katika kilele hichi. Ila kumbukumbu zimefana sana.
Na kama kuna sehemu yeyote watu wamekusanyika au kuna mdahalo wa kumuenzi mwl hata nje ya mipaka ya nchi yetu tungependa kujuzwa nini kinajiri huko.
Shida kubwa si ngoma na vinywaji, its about delivery! Wanaboa sana hao viongozi uchwara! Utakuta wameenda hapo na magari ya fahari, ambayo hata Mwalimu mwenyewe hakuwahi kuyaona au kuyapanda... Wamemuenzi Mwalimu kivipi?Wameipiga vita rushwa kivipi?Ni kwa kiasi gani wanaingia Ikulu kwa Usafi?Hapo kinachofanyika ni Ngonjera tu...yani kujiwekea fedha zaidi mifukoni kwa wale walio kwenye kamati za maandalizi... fyuuuuuu!!! Aibu!
Kama kawaida yake Mkapa bila aibu lazima awepo kumkumbuka shujaa aliyefanikisha ulaji wake
Mkuu umekuwa mkali sn hapa, da! kweli unauchungu na hii nchi, mimi sio mzuri kwenye siasa nafikiri mpwa unafahamu, nimereport tu na baada ya kutuma hii thread net ilikata na hata hii post sijui kama utaisoma. Naona hapa ngonjera zimepamba moto watoto wako trained vizuri wametoa shoo kali ya martial arts nzuri.
Pole pole kaka usije toboa macho watotoJamani achaneni na habari hizo za Butiama, mimi nina hasira hadi ninataka kupiga watoto wangu wanapofosi waendelee kuangalia hayo matumizi ya hela za serikali bila tija!...Mitumbo yao mikubwa mipana, kama magunia, na hawaoni aibu jinsi walivyo tofauti na wananchi wa kawaida...puuuuuhh!. Wananiboa mimi bana! Mikalio ndo usiseme.. Ikianzisha mada ya kujenga chuo kikuu hapo Butiama wataanza kuinamisha sura kama vile wanashikisha mtu ukuta!...sIWAPENDI HAO WANGEJUA...!
Zanzibar wamesema hawautambui Muungano leo huyo waziri kiongozi kafuata nini?Kapuya katika salamu zake kamsahau Waziri kiongozi hadi akakumbushwa
Waziri Kapuya anataka kumkaribisha rais kuhutubia sijui ataongea nini,kwa sasa mh. anapumzika.Kapuya kisha ingiza mambo yake ya Simba sport clu kwa kuhoji kwanini haoni laki yake kwenye waimba halaiki bali rangi ya jangwani?????