Live kutoka kuzimu!

Mkuu hem naomba uelezee hapa,kuna fungu linasema mshahara wa dhambi ni mauti,maana yake ni nini?

Pia,naomba uelezee huko kuzimu watu wanakufa au wanaendelea kuishi milele huku wakiteseka?

Naomba pia uelezee,fungu linasema mahari pa ibilisi na waovu wote(wakiwemo hao mapepo) hapatakuwepo tena,ina maana gani?
 
Naomba uelezee sehemu unasema hizi ni roho za wafu,Yesu alisema roho haina nyama wala mifupa,sasa mbona roho hizi za wafu usemazo hapa inaonekana wazi zina nyama na mifupa?
 
Je kwenye hii passage yako kuna Habari Njema ya Ufalme wa Mungu?

Mbona unatengeneza hadithi kuwatishia watu badala ya kuwaeleza ukweli wa Mbingu na ondoleo la dhambi?
 
Je kwenye hii passage yako kuna Habari Njema ya Ufalme wa Mungu?

Mbona unatengeneza hadithi kuwatishia watu badala ya kuwaeleza ukweli wa Mbingu na ondoleo la dhambi?
Live Kutoka KUZIMU ni HAKIKA Si hadithi.

Pia imekuja Kwa uhalisia Si kutosha watu, ni kuwahakikishia nini kitatokea ikiwa mtu atakufa dhambini nini anaenda kutana nacho.

Pia report imeanza na Kuzimu sababu huko wanaenda wengi zaidi kuliko wanaoingia Mbinguni, Nia ni kupunguza msururu wa kuingia huko Kwa kutojua.

Manabii wa uongo wanadanganya watu eti hakuna mateso wakati ni Uongo. Wawawakatazi watu kuacha DHAMBI, wanawake wanavaa nusu uchi na hawaambiwi KWELI, wengine wanaabudu madhehebu ya Shetani ,viongozi wanakunywa pombe na kuwambia WAUMINI kunywa pombe Si DHAMBI, nk nk

Endelea kuwepo, tutakuletea habari za Mbinguni live pia Ili uamue kwenda huko kupitia njia nyembamba ambayo WANADAMU wengi hawaitaki.

Njia ya Mbinguni ni ya wachache, ni Hadi ujikane, ujitwike msalaba wako na kumfuata YESU.

Amen.
 
Je kwenye hii passage yako kuna Habari Njema ya Ufalme wa Mungu?

Mbona unatengeneza hadithi kuwatishia watu badala ya kuwaeleza ukweli wa Mbingu na ondoleo la dhambi?
Mada ya Live Kutoka KUZIMU lengo ni kuwajulisha yanayotokea live kuzimu,

Pia imelenga kuwambia DHAMBI ni nini, na DHAMBI zipi zinawapeleka kuzimu Kwa upana wake.

Hatua inayofuata ni kuwaelekeza jinsi ya kufanya TOBA na kuiendea njia nyembamba Kwa HIARI Yao.

Amen
 
Lini hiyo siku [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Maisha yana miaka 3.5 billion years, jua litazima 5 billion years ijayo.

Utasubiti mno si wewe tu mpaka kitukuu wa kitukuu chako
Mateso yanaanza mara tu mtu anapokufa na kuingia KUZIMU ya moto.

Hilo ni gereza la muda wakati HUKUMU ya Mungu ikisubiriwa.

Na hakuna namna mtu aliyeko kuzimu ya moto akaokoka asiende Jehanum ya milele baada ya HUKUMU.

Wewe hutaishi milele ukisubiri HUKUMU ya mwisho, ukifa hatma Yako inaanza mara Moja.

Uamuzi ni wako, na ni wakati huu Ukiwa hai,

Ukifa, hakuna masahihisho au marekebisho.

Amen
 
wee ushatinduliwa siobure
Mimi ni mwana wa ufalme wa Mungu,

Hakuna HUKUMU Kwa watakatifu,

Karibu umpokee YESU kristo wa Nazareth, utapewa Roho mtakatifu atakayekusaidia kukujulisha DHAMBI ni nini na jinsi ya kuziepuka, na kuzitubia ukianguka.

JINA lako litaandikwa katika kitabu Cha Uzima,

Ukilala MAUTI, utaingia direct Mbinguni.

Amen.
 
yesu
yesu mkatafitoo ameeeein kubwaaaaa
 
Barikiwa Mtumishi,usisahau hata mapepo na shetani na mawakala wake,wapo hapa kupindisha naweza thibitisha hilo.
Wengine c watu, lakini je naomba niulize swali je umefikaje kuzimu na upo kama agent wa nuru ama giza
Na ndio hawa wanao comment kwa hasira na kupinga kila kitu cha kimungu. Ndio hawa wanaotala uwaoneshe Mungu kama wanavyoona Milima. Ndio hawa wanataka uwaletee Mungu huku umemshika mkono. Wanatumia fake ID kujifunua humu japo mtaani hatujawahi waona kwa dhahiri na kwa kiuhalisia. Kwa miaka yangu ya kuishi duniani sijawahi kutana naye hata mmoja physically na pia kwa muda niliotumia mitandao kama FB, Twitter, Instagram na mingineyo sijawahi kukutana nao zaidi ya huku JF kwa kuwa wana fake ID.
 
Wenye macho ya Rohoni tunajua,

Wapo mapepo wenye account Facebook, insta ,Twitter nk nk na zinaoperate kama kawaida,

Wanao uwezo kufanya chochote katika ulimwengu huu, Nia ni kuleta ushetani utamalaki duniani kuwapeleka wengi zaidi kuzimu,

Hao wako layer ya pili ya kuzimu, ilipo milki Yao, palipo na ulimwengu wa Giza.
 
Binafsi sijawahi kutana nao zaidi ya hawa wa JF. Wao wanapinga kila kitu kuhusu Mungu.
 
MUNGU KAAGIZA TUPENDANE SIO TUTISHANE.
 
Ushetani ni matendo yako maovu usisingizie mapepo.
Uzinzi ni kwa tamaa ya mwili wako.
Wizi ni kwa tamaa ya usichonacho.
Inshort dhambi zote wewe ndo mkurugenzi mtendaji.

Mtu umeperuzi mwenyewe online mitandaoni ukatazama binti ukampigia ukafika ulipotaka kufika nae halafu unasema ni mapepo huko facebook. UNAFIKI.
 
Meen hiyo ya kusagwa kwenye blender kisha unarudi tena kuwa mtu Kisha unasagwa tena,that genius.
[emoji23][emoji23][emoji23], Najiuliza hiyo Blender walichomeka wapi, kwenye switch ipi huko kuzimu.

Ila tufikie mahali tuheshimiane[emoji23]. Tutumie njia polite na zenye logic kuwaambia watu waache Dhambi sio kupeana vitisho kama hivyo anavyoviongelea jamaa hapo juu.

Anasema daraja la pili kuzimu ni la majini na shetani tu binadamu hawaruhusiwi kwenda, lakini mwamba yeye ameingia hapo..[emoji1430][emoji23]
 
Huyu waumini wake kama anao watakuwa wanafiki sana sababu walimfata kwakuwa wanaogopa hayo madaraja ya adhabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…