INAENDELEA..........
IDARA YA WALIOSIKIA INJILI NA KIKAIDI KUTUBU.
Watu Hawa wake Kwa waume walikuwa katika mashimo ya kuzimu, Kila Mmoja ndani ya shimo lake wakizungukwa na walinzi.
Palikuwepo na picha ya Kila mtu juu yake iliyoonyesha Jina, mashtaka yake yaliyompeleka kule,
Tuliposogelea shimo la mtu mmoja picha yake alivyokuwa akionekana duniani tofauti kabisa na alivyoonekana kule, pichani alionekana mrembo sana,
Lakini katika uhalisia ilikuwa tofauti sana, kiu aliyokuwa nayo ilisababisha Ulimi Kutoka kinywani na ulionekana mrefu sana, Ulimi Ule ulikuwa mrefu sana unafika kifuani, mapepo yalishika ndimi zao na kuzivuta nje zaidi, maumivu yake nalisababisha kutotamani kuwaangalia tena,
Macho yao yalitoka nje Kwa maumivu na usingeweza linganisha mwonekano wa picha zao na uhalisia wakiwa kuzimu, na mbaya zaidi maumivu ni ya milele.
Panga zao na muundo wa visu vyao mapepo wale vilitiasha mno,
Watu Hawa Kila Mmoja alikuwa na shtaka lake,
Wengine walishiriki kuwapiga na kuwatesa watumishi wa Mungu wa Kweli walipokuwa wakihubiri.
Wengine walisikia Neno likihubiriwa na walidhihani kuwa ni waongo, wanatafuta tu sadaka.
Wengine makosa Yao ni walipinga kuwa hakuna moto wa Jehanum Wala kiyama, Kila walipopata ujumbe wa Mungu ukiwaonya watu kuacha UOVU maana Kuzimu ya moto IPO!!
Yesu alisema, niliwaonya kupitia neno langu kuwa: Nyama na Damu haziwezi kuurithi Uzima wa Milele lakini hawakusikia, walipoteza Mali na nguvu zao kuhangaikia miili iharibikayo na kuwadharau watumishi wangu waliodumu katika kuyatafuta mapenzi yangu (1Wakorithinto 15:50).
Yesu akaendelea kusema, katika neno langu, niliwaonya kuwa nimewaita nanyi mkakataa, nimenyoosha mkono wangu ,asiangalie mtu,
Bali mmebatilisha shauri langu, Wala hamkutaka maonyo yangu,
Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, nitadhihaki HOFU yenu ifikapo kama tufani, na msiba wenu ifikapo kama kisulisuli, DHIKI na taabu itakapowafikia, ndipo watakaponiita, lakini sitaitika!! (Mithali 1:24-28).
Yesu alitumia neno lake kuwajibu wale waliomwita awasaidie wale Waliosikia neno lake na kudhibaki na wasitubu!!
IDARA YA WALIORUDI NYUMA.
Tulipofika Mahali pale, Pepo walikuwa wakivuta ndimi za watu wale nje, na kuanza kuzikatakata vipande vipande Kisha mkuki ulipigwa kooni na kutokezea mdomoni.
Kila walipojaribu kumsihi Yesu awasaidie, mapepo yaliwakemea na kusema, mlipewa nafasi nzuri lakini mkaiacha njia yake, na hamtatoka hapa.
Yesu alilia Kwa huzuni kubwa lakini hakusogea kuwasaidia.
Wengine katika kundi hili, walitokea familia za kikristo,
Wengine walikuwa watoto wa Wachungaji nk nk, wakidhani Mungu angewasamehe dhambi zao sababu ya utumishi wa wazazi wao.
Wengine walitembea katika Wokovu, lakini walipofukuzwa KAZI au kupitia majaribu mazito, walimwacha BWANA na kugeukia njia zao
(Ezekiel 18:24) Yesu asema, Bali mwenye HAKI atakapoghairi, na kuiacha HAKI yake, na kutenda UOVU, na kufanya machukizo yote kama Yale afanyayo mtu mwovu, je ataishi?
Katika matendo yake yote ya HAKI aliyotenda, halitakumbukwa hata mojawapo.
Maana pia imeandikwa, jihadharini msirudi nyuma,, maana ni Afadhali usiijue njia ya HAKI kuliko kuijua Kisha ukaiacha.
Amen.
IDARA YA MUZIKI.
Tulifika Mahali katika chumba au shimo mojawapo na Pepo lilikuwa limempiga mkuki mgongoni na Kutokea upande wa pili.
Mwanamuziki huyu alikuwa maarufu sana enzi za uhai wake, na nyimbo zake zilikuwa zikivuma sana duniani,
Na Kila nyimbo zake zilipopigwa duniani, ukali wa moto na maumivu yake yaliongezwa maradufu sababu nyimbo zake zikitumika katika club mbalimbali kuwapoteza watu wasimkumbuke Mungu.
Wanamuziki wengine waliokuwemo mle, walitumika madhabahuni, kosa la mmoja wao alisuka Rasta Ili apate mwonekano sawasawa na mwonekano wa wasanii wa kidunia.
Mwingine alifika kuzimu sababu ya kufanya UASHERATI Kwa Siri na wasichana wanaoimba pamoja naye. Matendo yote mema aliyotenda hayakukumbukwa sababu hakutubu dhambi hiyo aliyoificha.
Maana imeandikwa, afichaye dhambi.hatofanikiwa..Bali aziungamaye na kutubu atapata rehema.
KITENGO CHA WAANGALIA FILAMU ZA KIDUNIA.
Mwanamke mmoja alikuwa akipigwa na kitu mithili ya nondo na kutobolewa nacho machoni, maumivu yake yalikuwa makali sana.
Mashtaka ya mwanamke huyu yalikuwa ni kuangalia tamthilia za kidunia kwenye Runinga,
Mapepo Yale katika Kuzimu level ya pili, hubuni FILAMU hizo na kuwaletea wasanii na waigizaji wa kidunia walioingia mikataba nao, tamthilia zile ziliwekewa uvuvio wa kipepo Ili Kila aangaliaye anamiwe na Roho hizo,
Roho za kipepo zilifanya KAZI ya kuleta kiburi Kwa waume zao na kusababisha hasira na zinaa kupitia tamaa Kwa waigizaji ndani ya tamthilia hizi.
Tamthilia aina hii zenye uvuvio wa kipepo zimechangia kuharibu hisia za wasichana na kubadili mtizamo wa Mungu juu ya NDOA nk nk.
IDARA YA KUJIPAMBA.
Mashimo haya yalihusika na wanawake na Mwanaume waliojipamba, wanawake wavaa suruali,nguo za kubana,waliosuka, Rasta na mitindo mbalimbali,waliofuga kucha ndefu, waliopaka wanja, kuchonga nyusi ,watiotoga masikio, pia, wavaa hereni, vikuku miguuni, nywele bandia,Vito vya puani , cheni shingoni na Kila aina ya mavazi na mapambo ya kidunia.
Kundi hili lilipewa ADHABU sawa na wazinzi na MAKAHABA.
Pepo mmoja alikamata mkufu uliovaliwa shingoni mwa mwanamke mmoja na alimnyonga kupitia cheni hiyo, na BAADAYE alichukua mnyororo mkubwa alioendekea kumnyonga shingo Ile Hadi ikakatika, Cha kushangaza baada ya muda mchache, shingo ilirudia ilivyokuwa mwanzo, na Pepo alianza mateso UPYA na endelevu,
Mwanamke mmoja aliyepelekwa kuzimu Kwa kuvaa nywele bandia, nywele zile bandia zilibadilika na kuwa nyoka wengi kichwani ambao walimuuma mfululizo na alipiga kelele ya maumivu makali ya nyoka wale kichwani mwake.
Nywele bandia Zina u uvuvio wa kishetani na Kila avaaye ,mapepo katika form ya nyoka walitoka kuwashambulia Ili kuwafanya wawe wakorofi Kwa waume zao na kuleta uongo na usaliti ndani ya NDOA.
Nami nikaona mwanamke mmoja ndani ya shimo lile aliyeletwa Kwa kosa la kuvaa viatu virefu vya kikahaba,
Alionekana kabla ya kufa alipokuwa duniani akiingia Kanisani akiwa amevaa viatu virefu na kuingia Kanisani,
Sauti za vishindo vya viatu vyake viliondoa utulivu ibadani, vijana walipoangalia viatu vyake macho yalitoka kuangalia viatu na kupanda kuiangalia miguu yake iliyovutia, ghafula Mishale ya kipepo ilitoka ndani ya macho ya msichana na kuwaarukia vijana wote walioangalia miguu kupanda juu ya mwili wake,
Mishale Ile mieusi ya kipepo, iliwafanya vijana wale kutengeneza picha katika NAFSI zao na kuanza kuzini na Binti yule katika NAFSI zao,
Imeandikwa, amtazamaye mwanamke Kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni.
Pepo mwingine alikuwa akimpiga sikioni mwanamke Kwa nyundo kubwa aliyekuwa ametoboa sikio lake na kuvaa hereni, alilia Kwa uchungu bila msaada.
(Isaya 3:16-24)
BWANA akasema tena, Kwa Sababu Binti za sayuni Wana kiburi, na kuenenda Kwa shingo zilizonyooshwa, na macho ya kutamani, wakienenda Kwa hatua za madaha, na kuliza njuga Kwa miguu Yao,
Basi Kwa hiyo BWANA atawapiga Binti za sayuni Kwa Pele za utosini, na BWANA ataifunua Aibu Yao.
Siku hiyo BWANA atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao, na Pete za masikio, na vikuku, na taji zao,, na dusumali na mafurungu na vitambi, na vibweta vya marashi na matakasimu, na Pete za azama, na mavazi ya sikukuu na debwani na shali na vifuko, na vioo vidogo na kitani nzuri na vilemba na utaji.
Hata itakuwa, Badala ya manukato mazuri kitakuwa uvundo, na Badala ya mishipi, kamba, na Badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa, na Badala ya kisibau, mavazi ya kigunia, na kutiwa alama mwilini kwa moto Badala ya uzuri.
(Yakobo 5:3) Dhahabu yenu na Fedha yenu zimeingia kutu na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto.
WACHUNGAJI WALIOPOTEZA MBINGU.
Katika vyumba hivi walifungwa Wachungaji mbalimbali, mateso ya chumba hiki ni tofauti na mateso ya vyumba vingine, ni makali na mabaya zaidi.
Pepo alomkamata Mchungaji mmoja na kumpiga pingu na minyororo, Kisha Akamweka juu ya meza ya CHUMA,
Pepo alikuwa na vifaa vingi zaidi alivyotumia kumfanyia upasuaji.
Pepo alichukua CHUMA kikubwa na kukiingiza ndani ya tumbo baada ya kulipasua Kwa kisu butu, CHUMA kile kiliingia ndani ya MWILI wa mtu yule,
Mtu yule alipiga kelele kubwa Kwa maumivu makali,
Pepo hakujali kelele zile, aliendelea na operation, Pepo alichukua kisu kikubwa Cha CHUMA na kupasua KICHWA Cha Mchungaji Kwa kutumia kisu kikubwa akigongelea na nyundo kubwa ya CHUMA,
KICHWA kilipasuka, Pepo alichukua nge wengi wawakao moto na funza wakali akawatupa ndani ya KICHWA Cha Mchungaji Kisha kilirudishwa tena KICHWA Kwa kugongelewa misumari,
Zoezi hili lilianza UPYA Kila lilipofika mwisho, maumivu Yale hayaelezeki.
WACHUNGAJI wa uongo Walio kuzimu wanapitia mateso makali sana sababu ni wasaliti.
Mchungaji na Nabii yule wa uongo, alianza vizuri KAZI ya Mungu, alipoona watu ni Wachache, alifunga ziara na kwenda Kwa Wachungaji wa uongo wachawi wenye kujaza watu wengi,
Walimpeleka Kwa agent wa kuzimu aliyempa mazindiko ya kichawi aliyoenda kuyazika madhabahuni,
Na baada ya muda mfupi kupita, watu waliongezeka, na waumini walipotoa sadaka na ZAKA, Mchungaji alizitumia kufanya biashara zKe binafsi na kuzitoa sadaka Kwa mashetani,
Malaika wa BWANA alishuka Kutoka Mbinguni na upanga mkononi na kumpiga, mchungaji yule, alipata ugonjwa na alijua ugonjwa Ule alipigwa na Mungu lakini hakutubu na ndio kulikuwa chanzo Cha kifo, akafa na kushuka kuzimu ya moto.
Mchungaji mwingine wa uongo alilia Kwa maumivu makali Kwa kuwa Pepo alichukua msumeno mkali na kukatakata mwili wa Mchungaji yule vipande vipande na kuvirusha katika moto mkali, mtu yule hakufa ,Bado mwili uliungana tena na mateso kuendelea,
Kosa la Mchungaji yule ni kuiinamia na kuabudu sanamu ya bikra maria.
(Kutoka 20:3,4) Usiwe na miungu mingine ila Mimi,
Usijifanyie sanamu ya kuchonga...
KITENGO CHA WAUMINI WALIOSALI MAKANISA YENYE KUABUDU SANAMU.
Mateso ya watu Hawa yalikuwa makali sababu waliwekwa kundi la wasaliti kama wasaliti katika NDOA wanavyohukumiwa.
(2 Kor 6:14-18).
Msifungwe nira pamoja na wasioamini, Kwa jinsi isivyo sawasawa, Kwa maana Pana urafiki Gani kati ya HAKI na uasi?
Tena Pana ushirika Gani kati ya Nuru na Giza?
Tena Pana ulinganifu Gani kati ya Kristo na Beriali?
Au Yeye aaminiye ana sehemu Gani pamoja naye asiyeamini?
Tena Pana mapatano Gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai.
(Ufunuo 21:8) Bali waoga, na wasioamini, wachukizao, na wauaji na wazinzi, na wachawi na hao waabuduo sanamu na waongo, wote, sehemu Yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti.
Yesu aliwajibu watu waliokuwa katika mateso katika kundi la waabuduo sanamu kuwa walisikia na kusoma neno lake, na kusikia makatazio ya kuacha kuabudu sanamu lakini waling'ang'ania Dini Yao ya kishetani yenye wafuasi wengi wawapelekao waumini wao Kwa maelfu kuzimu ya moto.
Waabuduo sanamu wanajumuishwa na wapagani waabudu milima, pia dini zenye kuabudu nyota na mwezi, na wenye kuabudu jua na miungu mbalimbali.
Aamen
ITAENDELEA.....