Umeanza kunitisha eti namcrush roho mtakatifu,acha uongo mkuu!
Katika biblia yote,kinachotakiwa ni kuihubiri habari njema kwa kusema neema ya Kristo na kazi zake kwetu,ndio uhubiri unavyotakiwa kuwa yaani mahubiri yabebe ujumbe wa Mungu sana.
Nani anamjua shetani vizuri zaidi ya Yesu mwenyewe,ila mbona ametumia muda mwingi kuelezea ufalme wa mbingu sio mabaya ya shetani,ila nyie eti mnasimulia kuzimu kulivyo,tena kwa uongo wa wazi kabisa kiasi mkiulizwa maswali hamjibu mnataka muaniwe tu.
Acheni kupotosha watu,sio kuwa wote wanaokataa uhubiri wenu wanamkataa Mungu,la hasha,nakataa upotovu wa kumtangaza Mungu kwa njia hii.