Live Kutoka Mbinguni/ Welcome back to Heaven

Unifundishe au unipotoshe?yaani hiyo story ya Mbaya Huwezi hata msimulia mtoto wa Sunday school..Kwanza neno la Mungu linasema hivi,hukumu itafanywa na Mwana wa Adam siku atakaporudi kuwahukumu walio hai na wafu.Sasa mbona mnaonyesha huko mbinguni mmewakuta watakatifu waliotenda mema wanakunywa juice,Je walihukumiwa lini??
Unajua au hujui kuwa ukiingia Ulimwengu wa Roho hakuna time?

Ukiwa humo unaona yote yaliyopita na yajayo.

Pia ujue tangu kufufuka Kwa Yesu, wafao katika kristo hawabaki kaburini, huenda Mbinguni direct.

Ndomana ni kheri ukae ufundishwe kuliko kusoma BIBLIA na kuielewa kibinadamu bila msaada wa Roho mtakatifu.

Nawe ubarikiwe.
 
Amesema kuna lugha ya mbinguni, sasa najiuliza bwana Adam Mbaya alijifunzia wapi hiyo lugha ya mbinguni?
WATAKATIFU waliookoka waliopo duniani, waliojazwa ROHO MTAKATIFU wanaongea lugha za Mbinguni hata sasa.

Kunena Kwa lugha kupo na ni HALISI.

Zipo lugha za WANADAMU, na lugha za Malaika/Mbinguni.

Amen
 
Unajua au hujui kuwa ukiingia Ulimwengu wa Roho hakuna time?

Ukiwa humo unaona yote yaliyopita na yajayo.

Pia ujue tangu kufufuka Kwa Yesu, wafao katika kristo hawabaki kaburini, huenda Mbinguni direct.

Ndomana ni kheri ukae ufundishwe kuliko kusoma BIBLIA na kuielewa kibinadamu bila msaada wa Roho mtakatifu.

Nawe ubari
We hayo maneno unayosema tangu kufa Kwa Yesu watu ni straight mbinguni unayatoa wapi?Kitabu gani,Sura gani na mstari gani maana biblia ndio muongozo wetu.

Halafu unavyosema Heri nikae nifundishwe kuliko kusoma biblia mwenyewe,kwani anayenifundisha si binadamu kama Mimi?yeye anampataje roho MTAKATIFU wa kumuelewesha Mimi nimkose?au roho anachagua watu?
 
(Matendo 7:59.)

Stephano alipokuwa akipigwa mawe aliinua macho Mbinguni na kumwona Yesu.

Na alipokuwa akifa alipiga kelele kuwambia Yesu ipokee Roho yangu.

Roho za WATAKATIFU baada ya kufufuka Yesu hazifungwi tena kaburini Wala kuzimu. Ni Mbinguni direct.
 
INTRODUCTON:

Shalom!!

Nawakaribisha tena Mbinguni, Mbinguni ndiko tulikokuwako milele kabla ya Mungu kutuleta duniani kupitia pumzi ya uhai Kwa baba na mama zetu wa duniani.

Mbinguni ni wapi?

Hapa tunapoishi ni Mbingu ya kwanza, Mbinguni tunapoongelea Leo ni Mbingu ya tatu. Ukiigawa katika matabaka inajulikana ni Mbingu ya saba. Huko ndipo tutakapokuwa tukipaangazia katika mada hii Kwa muda mrefu sana. Ni lifetime experience, maana Yesu huwachukua watu wengi sana na kuwapeleka Mbinguni Kisha huwarudisha Ili walete shuhuda Ili kuwaimarisha WATAKATIFU walioko duniani.

MY LIFE EXPERIENCE.

Nilipokuwa mdogo sikumbuki miaka, lakini nakumbuka kumbukumbu hiyo nzuri kuwahi kuipata katika Maisha yangu hapa duniani.

Nalikuwa katika njonzi, ghafula, kufumba na kufumbua, nilikuwa katika Nchi nzuri ambayo uzuri wake hauelezeki.

Palikuwa na Nuru njema sana iliyong'aa, mwonekano wa Nuru Ile ,haukufanana na Nuru ya mchana Wala Nuru ya mbalamwezi wakati wa usiku.

Niliangaza kulia na kushoto, nyuma Ili nione asili ya Nuru Ile bila mafanikio, nilijaribu kupiga hatua nione wapi Nuru Ile njema ilikotokea, Nuru Ile haikuchoma kama mwanga wa jua, palikuwa tulivu na pazuri sana, moyoni nilijawa na furaha tele kuwapo katika Nchi Ile ambayo haikuwa na Jua Wala mwezi lakini ilijaa Nuru nzuri yenye kuvutia sana.

Kila nilipoongeza hatua kuikaribia Nuru Ile nzuri yenye RANGI nzuri ambazo kamwe Hadi Leo hii sijawahi kuziona katika Ulimwengu huu, Nuru Ile ilizidi kuwa mbali nami na nilizidi kuifuata lakini kamwe sikuweza kufika mwisho, Mahali pale na Nchi Ile nilitamani sana kuendelea kuwepo. Lakini Kwa Bahati mbaya nilistuka nikiwa nimelala kitandani na nilipatwa na huzuni kurudi katika mazingira haya ya hapa tulipo.

Katika mada hii nitakuwa nikikuletea shuhuda za Raia waliotoka Mbinguni, waliopelekwa tena Mbinguni na kuonyesha uzuri wa Mbinguni Ili kuja kuwatia moyo WATAKATIFU Duniani waendelee kuvumilia Ili siku ikifika waingie mji Ule mzuri.

LIVE KUTOKA MBINGUNI. ( Na Adam Mbaya).

Nilipokuwa katika kusoma BIBLIA, BWANA Yesu alinitokea na kuniambia kuwa, Leo nitakupeleka Mbinguni, Mahali pazuri makazi ya WATAKATIFU.

Ghafula nikajiona nimegawanyika, niliona mwili wangu Ukiwa chumbani na Mimi nikiwa naelekea juu sana Kwa Kasi ya ajabu.

Tukiendelea na safari Ile Hadi tulipofika Mahali ambapo palikuwa na mpaka kati ya uumbaji nyuma yetu, na umilele mbele yetu.

Nyuma yetu Mahali pa uumbaji niliweza kuona nyota nyingi, lakini mbele yetu katika umilele, hapakuonekana mwisho wake.

MAPOKEZI YA MBINGUNI/HUDUMA YA NYUMBANI.

Tulipofika Mahali hapa, naliona Malaika wengi sana na WATAKATIFU ambao walikuwa wanapokelewa Ili kujiandaa kupanda Mbinguni juu zaidi.

Mahali pale palikuwa pazuri sana ambapo uzuri wake Si Rahisi kuelezea,

MUZIKI.

Malaika walikuwa wakiimba huku wakipiga vifaa mbalimbali vya MUZIKI ambavyo vipo hapa duniani na vingine ambavyo SIKUWAHI kuviona kabla.

Mahali hapa palikuwa na furaha tele,WATAKATIFU waliopokelewa Mahali pale walikuwa wenye furaha tele na walipongezana na kukumbatiana Kwa furaha. Palisikika mziki mkubwa na mzuri sana wa kumsifu Mungu.

Zilisikika nyimbo nzuri za kusifu na kuabudu ambazo huimbwa hapa duniani, nilishangaa kusikia nyimbo hizo Mahali pale na nilimuuliza BWANA Yesu kuwa kwanini wanaimba nyimbo zetu.
Yesu alijibu, duniani Kuna uchafuzi mkubwa hivyo Mungu hutuma neno lake kupitia nyimbo Ili kubariki WATAKATIFU.

MIILI YA WATAKATIFU.

Mwonekano wa miili hiyo ya WATAKATIFU ilionekana kama miili ya kioo, transparent , iliyong'aa sana. Na umri wa WATAKATIFU walipofika pale mapokezi ya Mbinguni ilionekana sawa wote walionekana wenye umri sawa kama miaka 30 hivi. Hapakuwa na Mzee aliyeingia Mbinguni na uzee wake,hapakuwa na mgonjwa Wala mlemavu, walipewa miili Bora. Hapakuwa na njaa, Wala huzuni Wala DHIKI.

MIILI ya WATAKATIFU ilizidiana kungaa, wahubiri INJILI waling'aa sana miili Yao, waliotunza na kuhudumia wajane, yatima, maskini,wagonjwa Kwa pesa zao pia waling'aa sana.

NDOA.

Mmoja wa WATAKATIFU aligeuka na kumwona aliyekuwa mume wake alifika Mahali pale pa mapokezi na walikumbatiana Kwa furaha na kulia machozi ya furaha.

Hapakuwa na NDOA Mahali pale kama duniani,mke na mume waliitana kaka na dada, na tamaa za mwili hazikuwepo Mahali pale, palifunikwa na furaha na utukufu wa Mungu.

VYAKULA.

Malaika wengine walikuwa wakiwahudumia WATAKATIFU MATUNDA YA MWILI WA DHAHABU. Niliona pia Malaika wakimimina juice Kwa watakatifu ambayo ilikuwa ya kipekee.

Nilitamani kunywa juice Ile lakini Yesu aliniambia kuwa juice Ile ni spesho Kwa washindao ambao ni WATAKATIFU.

Nilimwona pia Malaika mmoja akiwa anakula EMBE!! Nilimuuliza, BWANA, Pana maembe huku?

Yesu alinijibu vyakula vyote vilivyoko duniani, vipo Mbinguni na zaidi ya hapo. Pana miti mingi ya matunda mengi ambayo mengine hayapo duniani, Mbinguni ni kizuri sana.

Yesu aliniambia huku Kuna Kila chakula Cha asili kulingana vyakula WATAKATIFU walivyokula duniani, na Malaika walihudimia WATAKATIFU, walipika na kuwahudumia maana ni Wana wa ufalme. Malaika walivutiwa sana kuwaona WATAKATIFU maana wakishinda Hila na majaribu ya mwovu duniani.

NJIA ZA MBINGUNI.

Palikuwa na njia 12 zilizokuwa na Majina ya Wana wa Israel/ Yakobo.

MALANGO YA MBINGUNI.

Pia palikuwa na Malango 12 ya Mbinguni yaliyoandikwa Majina 12 ya Wana wa Israeli kama zilivyokuwa njia zile 12. Na Kila lango alisimama Malaika mlangoni mwenye upanga mkubwa.

MAGARI YA MBINGUNI.

Baada ya mapokezi ya mahali pale, Malaika alipuliza tarumbeta kuwaarifu WATAKATIFU waliokuwa mapokezi ya Mbinguni kupanga foleni Ili kupanda magari ya Mbinguni kuwapeleka juu zaidi Mbinguni.

Yalishika magari ya Dhahabu, yenye kuwaka moto mtakatifu yaliyokuwa yakiendeshwa na Malaika, na Malaika waliwaongoza WATAKATIFU kupanda magari hayo yaliyokokotwa na farasi. Mahali pale na uzuri Ule hauelezeki.

ITAENDELEA......
Dah kama ndo tulikofikia huku!
Inabdi kuwahi matibabu
 
Lk 17:20-21 SUV​

Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuona; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
 
(Matendo 7:59.)

Stephano alipokuwa akipigwa mawe aliinua macho Mbinguni na kumwona Yesu.

Na alipokuwa akifa alipiga kelele kuwambia Yesu ipokee Roho yangu.

Roho za WATAKATIFU baada ya kufufuka Yesu hazifungwi tena kaburini Wala kuzimu. Ni Mbinguni direct.
Kama roho ni mbinguni Direct bhasi wewe u kinyume na biblia soma hapa!

Mhubiri 3:18-21

Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama.
Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.
Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.
Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?
 
Unajua au hujui kuwa ukiingia Ulimwengu wa Roho hakuna time?

Ukiwa humo unaona yote yaliyopita na yajayo.

Pia ujue tangu kufufuka Kwa Yesu, wafao katika kristo hawabaki kaburini, huenda Mbinguni direct.

Ndomana ni kheri ukae ufundishwe kuliko kusoma BIBLIA na kuielewa kibinadamu bila msaada wa Roho mtakatifu.

Nawe ubarikiwe.
Kwanini hukujiona weww ukinywa Juice mkuu kama upandw huo hauna time au muda huo wwe ulikuwa Motoni ?
 
Lk 17:20-21 SUV​

Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuona; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
Short sighted.

Maandiko uliyoquote ni sawa, na kilichoelezwa hapo juu ni sawa.

Ulichoshindwa ni kuelewa kipi ni kipi, kinaanzia kipi kipi kinafuata.

Tunarudi pale pale, Bila KUONGOZWA na ROHO MTAKATIFU,kamwe huwezi elewa Neno la Mungu.

Kitabu Cha ufunuo kinaeleza IPO siku ya HUKUMU, na watakaoshinda watatawala milele pamoja naye.

Ni Kweli ufalme wa Mungu umo ndani yetu, tulioamini na kuokoka, lakini vile vile IPO siku ya mwisho na utimilifu wake.

Ubarikiwe.
 
Ndo mnakokimbiliaga huku weww unajuaje kama mimi sina huyo roho mtakatifu au huyo roho alikuorodheshea majina ya watu wote walio naye?
 
Kama roho ni mbinguni Direct bhasi wewe u kinyume na biblia soma hapa!

Mhubiri 3:18-21

Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama.
Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.
Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.
Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?
Umequote kabisa, " Nani ajuaye kama Roho ya binadamu huenda juu na kama Roho ya mnyama huenda chini"

Ndo ujue Suleiman hakuwa akijua UKWELI.

AGANO jipya, Yesu amekuja kuyafunua yote.

WATAKATIFU waliookoka wakifa ni Mbinguni direct.
 
Ndo mnakokimbiliaga huku weww unajuaje kama mimi sina huyo roho mtakatifu au huyo roho alikuorodheshea majina ya watu wote walio naye?
Ndo nasema, ingekuwa na Roho mtakatifu, angekufunulia kuijua Kweli yote.

BIBLIA ni coded, usijechukua mstari mmoja ukajenga HOJA,

Soma yote na uombe mwongozo wa Roho mtakatifu.

Na wengi wenu ni WASABATO, Mko mwilini,

Hamkubali kufundishwa na Roho mtakatifu sababu hamumuamini.

Na we ubarikiwe, neema yake ikufikie,

Siku ya HUKUMU uingie Mbinguni.

Amen
 
(Matendo 7:59.)

Stephano alipokuwa akipigwa mawe aliinua macho Mbinguni na kumwona Yesu.

Na alipokuwa akifa alipiga kelele kuwambia Yesu ipokee Roho yangu.

Roho za WATAKATIFU baada ya kufufuka Yesu hazifungwi tena kaburini Wala kuzimu. Ni Mbinguni direct.
Kwa nini una edit neno la Mungu?hujui imekatazea kufanya hivyo?hebu soma vizuri Huo mstari

Ni wapi alipoinua macho yake juu akamuona Yesu??Mstari ulikuwa wazi kabisa kwamba akaomba bwana Yesu ipokee roho yangu,hiyo ni kawaida kuomba hivyo.
 
Attachments

  • Screenshot_20231103-171156_1.jpg
    Screenshot_20231103-171156_1.jpg
    21.1 KB · Views: 3
Ndugu Kiby karibu sana kushare nasi shuhuda za Mbinguni ulizo nazo katika Uzi huu Ili kuwatia moyo WATAKATIFU na kuhubiri INJILI.

Ubarikiwe.
Mambo ya rohoni hayana matunda kwa watu wa mwilini na mara nyingi husikika kama kufuru na ushahidi wa haya upo kibao kwa hukumu zilizowahi kutolewa na watawaba(dini) kwa manabii au wapakwa mafuta.
Ushuhuda huu uliouleta umelenga sana utawala ule wa milele na maskani yake itakavyo kuwa. Ramani yake kwa uhalisi inapatikana katika kitabu cha ufunuo 21 yaani yerusalemu ya mbinguni. Ni mji wa mraba marefu na mapana yake yakilingana kwa kipimo cha maili 1,500. Hakuna hekalu ndani yake wala kanuni za maumbile ya asili mfano wa jua la mchana na nyota za usiku wala majira ya nyakati kwa sababu uumbaji umerudishwa kwenye umilele(eternity) Ni kweli kuna mto wa maji ya uzima na pia kuna mti wa matunda ukizaa kila matunda mfululizo matunda kwa ajili ya wateule na majani yake ni uponyaji kwa wenyeji. Haya yote ni mambo ya kilindi sana maana hutambulikana kwa jinsi ya roho. Katika bustani ya Edeni palikuwa na mti wa uzima katikati yake ambapo kabla ya anguko katika ule umilele uliopotezwa na Adamu kwa kula kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya uliokatazwa. Huo mti uliwekewa makerubi kuulinda hata ukombozi mkamilifu wa miili ya watakatifu. Tunayo arabuni(dhamana) ya roho wa Kristo hata huo ukamilifu wa wakati.
Kwenye ulimwengu wa roho kuna tofauti ya mbingu moja kwenda nyingine hadi mbingu ya saba iliyo mbingu za mbingu.
Hivyo unapotoa ushuhuda ni lazima ujue unashuhudia mbingu ipi. Kuna ufufuo wa kwanza na ufufuo wa pili, kuna mauti ya kwanza na mauti ya pili yaani lile ziwa la moto, kuna harusi ya mwana kondoo(miaka 1,000) na umilele(eternity) vitu hivi huchanganywa sana.
Lakini uaminifu wa wateule wa Mungu wajapokuwa wajinga hawatapotea katika ile njia ila ieleweka kati ya tofauti ya wajinga na wapumbavu. Wajinga ni wanyoofu wa moyo na hufu dishika bali wapumbavu ni washupavu wasiofundishika wala kurekebishika.
Chariot ni gari la moto la farasi katika ulimwengu wa roho nalo huwabeba watakatifu walalapo mauti.
Farasi hawa wa moto mtumishi wa Elisha aliombewa macho yake yafunguke aone jeshi hili la Mungu katika farasi na alipoona hofu ya asili ya kanuni za maumbile ikamtoka na kuwaita adui waje ili waufikilie mwisho wao.
Hakuna kilicho katika maumbile ya asili ya mwili ambacho hakikuanzia rohoni kwamba ni ulimwengu wa roho wa Mungu ama ulimwengu wa roho wa upotofu wa shetani.

Barikiwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini una edit neno la Mungu?hujui imekatazea kufanya hivyo?hebu soma vizuri Huo mstari

Ni wapi alipoinua macho yake juu akamuona Yesu??Mstari ulikuwa wazi kabisa kwamba akaomba bwana Yesu ipokee roho yangu,hiyo ni kawaida kuomba hivyo.
(Matendo 7:56)

Iko wazi anasema alionao Mbingu zimefunguka na kumwona mwana wa Adam ameketi mkono wa kuume wa Mungu.

HOJA Iko pale pale, WATAKATIFU waliookoka wafapo baada ya kufufuka Yesu huenda direct Mbinguni.
 
Umequote kabisa, " Nani ajuaye kama Roho ya binadamu huenda juu na kama Roho ya mnyama huenda chini"

Ndo ujue Suleiman hakuwa akijua UKWELI.

AGANO jipya, Yesu amekuja kuyafunua yote.

WATAKATIFU waliookoka wakifa ni Mbinguni direct.
Hamna kitu mnakosea walokole kama kukosa vitabu vya Mungu,yaani wewe ni WA kusema Suleiman alikuwa hajui KWELI yaani wewe unajua kushinda Yeye?Huyo Yesu mwenyewe alishasema soma hapo
 
Attachments

  • Screenshot_20231103-172135_1.jpg
    Screenshot_20231103-172135_1.jpg
    75.3 KB · Views: 2
Umequote kabisa, " Nani ajuaye kama Roho ya binadamu huenda juu na kama Roho ya mnyama huenda chini"

Ndo ujue Suleiman hakuwa akijua UKWELI.

AGANO jipya, Yesu amekuja kuyafunua yote.

WATAKATIFU waliookoka wakifa ni Mbinguni direct.
Haya nionyeshe sehemu Ambayo imeandikwa ukifa unaenda juu direct nionyeshe kutumia Mafungu ya biblia maana imeandikwa waenende kwa ushuhuda...

Mhubiri 9:5​

kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana tuzo tena; maana hata kumbukumbu lao limesahauliwa.

Zaburi 146 :4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.
(Zaburi 115:17), “…wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu yao, husuda yao, imepotea yote pamoja…”
(Mhubiri 9:10), waliokufa “hawawezi kuitarajia kweli”

(Isaya 38:18), waliokufa “hawawezi kumwona Mungu wala kumwona mwanadamu”
(Isaya 38:10,12); roho ya mtu aliyekufa pia “huzimika”,

Ayubu 17:1 inasema, Roho yangu imezimika, siku zangu zimekoma, Kaburi i tayari kunipokea.”
Ayubu 14:10,12,21 inasema, “Lakini mwanadamu hufa…Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?…Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa uzingizini…”

NAJUA KUWA MWILI NA NYAMA HAZITAURITHI UFALME KWA HIYO ROHO ZITURITHI SASA SWALI KWAKO KAMA ROHO IMESHAANZA KUURITHI UFALME YESU ANAKUJA KUFANYAJE NA ANAKUJA KUFUFUA NINI...?
 
Back
Top Bottom