Live Kutoka Mbinguni/ Welcome back to Heaven

Live Kutoka Mbinguni/ Welcome back to Heaven

Mkuu nilitaka kujua pia kama walijiunga na watoto wao na kama wazazi wao walikuwa huko walijumuika nao.......
kama grand^10 parents waliingia huko...., je wanaishi pamoja..... hizo nyumba zikoje .... yaani kama li Bugando moja linaka ukoo wa pleo?
Samahani kwa maswali ya kitoto labda!
Mpka sasa Tangu mwanzo wa dunia Mpaka sasa kunakadiriwa kuwa na watu zaidi ya biliom 700 au tririon 1 sasa fikiria hiyo sehemu
 
Sasa bhasi wew ulimwengu wa Roho bado haijaujua vizuri jitahidi Ukomae kwenye ulimwengu wa kiroho utajua mengi..
Kikubwa usiwe mwenye kujisifu..kuwa mvumilivu..
Karibisha Mafunzo ukiwa huko ujue vingi (Kama kwako karibisha Roho mtakatifu atakufundisha vingi sana )
Jaribu uwe ni mtu wa kusikiliza Roho yako mara zote jikite kwenye kuijua nafsi yako ndani zaidi..
Utajua mengi kuhusu roho yako na ulimwengu wakiroho
Kwamba Kuna njia zaidi ya hizo mbili kuingia Ulimwengu wa Roho?

Ikiwa IPO itaje nijifunze!!
 
ITAENDELEA......

HAKIKA yote utapata majibu yake,

Mungu akipenda kesho nitaendelea kuleta mwendelezo.

Ubarikiwe.
Kuna Binti alitoa mimba 2005, kwasasa kaokoka kweli kweli sasa akiingiabinguni 2025, atakutana na mtoto wake akiwa na miaka 20 au atakuwa Bado kachanga, na vipi watatambuana?
 
INTRODUCTON:

Shalom!!

Nawakaribisha tena Mbinguni, Mbinguni ndiko tulikokuwako milele kabla ya Mungu kutuleta duniani kupitia pumzi ya uhai Kwa baba na mama zetu wa duniani.

Mbinguni ni wapi?

Hapa tunapoishi ni Mbingu ya kwanza, Mbinguni tunapoongelea Leo ni Mbingu ya tatu. Ukiigawa katika matabaka inajulikana ni Mbingu ya saba. Huko ndipo tutakapokuwa tukipaangazia katika mada hii Kwa muda mrefu sana. Ni lifetime experience, maana Yesu huwachukua watu wengi sana na kuwapeleka Mbinguni Kisha huwarudisha Ili walete shuhuda Ili kuwaimarisha WATAKATIFU walioko duniani.

MY LIFE EXPERIENCE.

Nilipokuwa mdogo sikumbuki miaka, lakini nakumbuka kumbukumbu hiyo nzuri kuwahi kuipata katika Maisha yangu hapa duniani.

Nalikuwa katika njonzi, ghafula, kufumba na kufumbua, nilikuwa katika Nchi nzuri ambayo uzuri wake hauelezeki.

Palikuwa na Nuru njema sana iliyong'aa, mwonekano wa Nuru Ile ,haukufanana na Nuru ya mchana Wala Nuru ya mbalamwezi wakati wa usiku.

Niliangaza kulia na kushoto, nyuma Ili nione asili ya Nuru Ile bila mafanikio, nilijaribu kupiga hatua nione wapi Nuru Ile njema ilikotokea, Nuru Ile haikuchoma kama mwanga wa jua, palikuwa tulivu na pazuri sana, moyoni nilijawa na furaha tele kuwapo katika Nchi Ile ambayo haikuwa na Jua Wala mwezi lakini ilijaa Nuru nzuri yenye kuvutia sana.

Kila nilipoongeza hatua kuikaribia Nuru Ile nzuri yenye RANGI nzuri ambazo kamwe Hadi Leo hii sijawahi kuziona katika Ulimwengu huu, Nuru Ile ilizidi kuwa mbali nami na nilizidi kuifuata lakini kamwe sikuweza kufika mwisho, Mahali pale na Nchi Ile nilitamani sana kuendelea kuwepo. Lakini Kwa Bahati mbaya nilistuka nikiwa nimelala kitandani na nilipatwa na huzuni kurudi katika mazingira haya ya hapa tulipo.

Katika mada hii nitakuwa nikikuletea shuhuda za Raia waliotoka Mbinguni, waliopelekwa tena Mbinguni na kuonyesha uzuri wa Mbinguni Ili kuja kuwatia moyo WATAKATIFU Duniani waendelee kuvumilia Ili siku ikifika waingie mji Ule mzuri.

LIVE KUTOKA MBINGUNI. ( Na Adam Mbaya).

Nilipokuwa katika kusoma BIBLIA, BWANA Yesu alinitokea na kuniambia kuwa, Leo nitakupeleka Mbinguni, Mahali pazuri makazi ya WATAKATIFU.

Ghafula nikajiona nimegawanyika, niliona mwili wangu Ukiwa chumbani na Mimi nikiwa naelekea juu sana Kwa Kasi ya ajabu.

Tukiendelea na safari Ile Hadi tulipofika Mahali ambapo palikuwa na mpaka kati ya uumbaji nyuma yetu, na umilele mbele yetu.

Nyuma yetu Mahali pa uumbaji niliweza kuona nyota nyingi, lakini mbele yetu katika umilele, hapakuonekana mwisho wake.

MAPOKEZI YA MBINGUNI/HUDUMA YA NYUMBANI.

Tulipofika Mahali hapa, naliona Malaika wengi sana na WATAKATIFU ambao walikuwa wanapokelewa Ili kujiandaa kupanda Mbinguni juu zaidi.

Mahali pale palikuwa pazuri sana ambapo uzuri wake Si Rahisi kuelezea,

MUZIKI.

Malaika walikuwa wakiimba huku wakipiga vifaa mbalimbali vya MUZIKI ambavyo vipo hapa duniani na vingine ambavyo SIKUWAHI kuviona kabla.

Mahali hapa palikuwa na furaha tele,WATAKATIFU waliopokelewa Mahali pale walikuwa wenye furaha tele na walipongezana na kukumbatiana Kwa furaha. Palisikika mziki mkubwa na mzuri sana wa kumsifu Mungu.

Zilisikika nyimbo nzuri za kusifu na kuabudu ambazo huimbwa hapa duniani, nilishangaa kusikia nyimbo hizo Mahali pale na nilimuuliza BWANA Yesu kuwa kwanini wanaimba nyimbo zetu.
Yesu alijibu, duniani Kuna uchafuzi mkubwa hivyo Mungu hutuma neno lake kupitia nyimbo Ili kubariki WATAKATIFU.

MIILI YA WATAKATIFU.

Mwonekano wa miili hiyo ya WATAKATIFU ilionekana kama miili ya kioo, transparent , iliyong'aa sana. Na umri wa WATAKATIFU walipofika pale mapokezi ya Mbinguni ilionekana sawa wote walionekana wenye umri sawa kama miaka 30 hivi. Hapakuwa na Mzee aliyeingia Mbinguni na uzee wake,hapakuwa na mgonjwa Wala mlemavu, walipewa miili Bora. Hapakuwa na njaa, Wala huzuni Wala DHIKI.

MIILI ya WATAKATIFU ilizidiana kungaa, wahubiri INJILI waling'aa sana miili Yao, waliotunza na kuhudumia wajane, yatima, maskini,wagonjwa Kwa pesa zao pia waling'aa sana.

NDOA.

Mmoja wa WATAKATIFU aligeuka na kumwona aliyekuwa mume wake alifika Mahali pale pa mapokezi na walikumbatiana Kwa furaha na kulia machozi ya furaha.

Hapakuwa na NDOA Mahali pale kama duniani,mke na mume waliitana kaka na dada, na tamaa za mwili hazikuwepo Mahali pale, palifunikwa na furaha na utukufu wa Mungu.

VYAKULA.

Malaika wengine walikuwa wakiwahudumia WATAKATIFU MATUNDA YA MWILI WA DHAHABU. Niliona pia Malaika wakimimina juice Kwa watakatifu ambayo ilikuwa ya kipekee.

Nilitamani kunywa juice Ile lakini Yesu aliniambia kuwa juice Ile ni spesho Kwa washindao ambao ni WATAKATIFU.

Nilimwona pia Malaika mmoja akiwa anakula EMBE!! Nilimuuliza, BWANA, Pana maembe huku?

Yesu alinijibu vyakula vyote vilivyoko duniani, vipo Mbinguni na zaidi ya hapo. Pana miti mingi ya matunda mengi ambayo mengine hayapo duniani, Mbinguni ni kizuri sana.

Yesu aliniambia huku Kuna Kila chakula Cha asili kulingana vyakula WATAKATIFU walivyokula duniani, na Malaika walihudimia WATAKATIFU, walipika na kuwahudumia maana ni Wana wa ufalme. Malaika walivutiwa sana kuwaona WATAKATIFU maana wakishinda Hila na majaribu ya mwovu duniani.

NJIA ZA MBINGUNI.

Palikuwa na njia 12 zilizokuwa na Majina ya Wana wa Israel/ Yakobo.

MALANGO YA MBINGUNI.

Pia palikuwa na Malango 12 ya Mbinguni yaliyoandikwa Majina 12 ya Wana wa Israeli kama zilivyokuwa njia zile 12. Na Kila lango alisimama Malaika mlangoni mwenye upanga mkubwa.

MAGARI YA MBINGUNI.

Baada ya mapokezi ya mahali pale, Malaika alipuliza tarumbeta kuwaarifu WATAKATIFU waliokuwa mapokezi ya Mbinguni kupanga foleni Ili kupanda magari ya Mbinguni kuwapeleka juu zaidi Mbinguni.

Yalishika magari ya Dhahabu, yenye kuwaka moto mtakatifu yaliyokuwa yakiendeshwa na Malaika, na Malaika waliwaongoza WATAKATIFU kupanda magari hayo yaliyokokotwa na farasi. Mahali pale na uzuri Ule hauelezeki.

ITAENDELEA......
Kwa sisi wenye uelewa wa kiroho tunakuelewa
Haya mambo ni kweli na hakika!..
 
Kuna Binti alitoa mimba 2005, kwasasa kaokoka kweli kweli sasa akiingiabinguni 2025, atakutana na mtoto wake akiwa na miaka 20 au atakuwa Bado kachanga, na vipi watatambuana?
Ndio watatambuana HAKIKA.

Katika Ulimwengu huo utajua yote.

Hata ukikutana na Petro, Ibrahim, Isaka utawatambua bila kutambulishwa.

Amen
 
Kwamba Kuna njia zaidi ya hizo mbili kuingia Ulimwengu wa Roho?
Siku nyingine nitakufundisha na kukuelekeza kuna only two ways kama ulivyosema njia ya Nuru na njia ya giza..
Kwenye nuru zipo njia sahihi nyingi..
Ikiwa IPO itaje nijifunze!!
Ndio watatambuana HAKIKA.

Katika Ulimwengu huo utajua yote.

Hata ukikutana na Petro, Ibrahim, Isaka utawatambua bila kutambulishwa.

Amen
Kuna vingi unaongea ukweli na ndo kitu ambacho kimenifanya mpaka mimi kuna maswali nakujibu..

Naongezea kuwa hata kama mtoto ulimzaa leo na akafariki leo utaweza kumtambua ndani ya ulimwengu wa kiroho na unaweza kuongea naye..kwa sababu katika kuongea hutumii mdomo wala lugha za Ulimwengu huu wa 3rd Dimension
 
Kuna Binti alitoa mimba 2005, kwasasa kaokoka kweli kweli sasa akiingiabinguni 2025, atakutana na mtoto wake akiwa na miaka 20 au atakuwa Bado kachanga, na vipi watatambuana?
Mtoto wake hawezi kukua, atakuwa vile vile mchanga.

Binti hata akienda Mbinguni Mzee pia, umri wake hautazidi miaka 30 Kwa appearance maana kule watu ni umri mmoja.
 
Siku nyingine nitakufundisha na kukuelekeza kuna only two ways kama ulivyosema njia ya Nuru na njia ya giza..
Kwenye nuru zipo njia sahihi nyingi..

Kuna vingi unaongea ukweli na ndo kitu ambacho kimenifanya mpaka mimi kuna maswali nakujibu..

Naongezea kuwa hata kama mtoto ulimzaa leo na akafariki leo utaweza kumtambua ndani ya ulimwengu wa kiroho na unaweza kuongea naye..kwa sababu katika kuongea hutumii mdomo wala lugha za Ulimwengu huu wa 3rd Dimension
Uko sawa kabisa.

Njia ya Nuru nayo Ina njia zake.

Mungu Hana mipaka.

Ubarikiwe sana.

Bt nakushauri endelea kutamani Mbinguni, ni kuzuri sana.

Ubarikiwe.
 
Mtoto wake hawezi kukua, atakuwa vile vile mchanga.

Binti hata akienda Mbinguni Mzee pia, umri wake hautazidi miaka 30 Kwa appearance maana kule watu ni umri mmoja.
Hapa umedanganya nafsi haina umri, wala roho haina kipimo..
Kwahyo kujua kuhusu umri ni vigumu kwa sabbu nafsi wala roho haina pia Jinsia..
Unamjua kuwa huyu ni fulan kwa utambuzi usioweza kuelezeka ila sio kwamba utaona umbo la mdada sijui au mmama
 
Uko sawa kabisa.

Njia ya Nuru nayo Ina njia zake.

Mungu Hana mipaka.

Ubarikiwe sana.

Bt nakushauri endelea kutamani Mbinguni, ni kuzuri sana.

Ubarikiwe.
Mkuu Hilo la mbinguni ntaelezea kuhusu hili
 
Hapa umedanganya nafsi haina umri, wala roho haina kipimo..
Kwahyo kujua kuhusu umri ni vigumu kwa sabbu nafsi wala roho haina pia Jinsia..
Unamjua kuwa huyu ni fulan kwa utambuzi usioweza kuelezeka ila sio kwamba utaona umbo la mdada sijui au mmama
Ni Kweli,

Utambuzi ni Kwa namna ya pekee,

Nachomaanisha mwonekano wa wote kule wanafanana,

Ila kumtambua uliyewahi kuwa naye duniani, baba au mama au mtoto ndo utamjua Kwa namna ya pekee.

Amen
 
Ubarikiwe
Ubarikiwe.

Rudia kusoma tena, nimeandika japo ni Kwa uchache, endelea kuwepo maana Uzi huu hautaisha Leo Wala kesho,

Ni wa Milele.

Amen

imeandikwa "'mwenye masikio na asikie......''
 
Mwili ,nafsi na roho.
Katika mtizamo wangu kibiblia naweza changia kwa kusema vitu hivi ni tofauti japo vinakubalia katika jambo moja.
Mwili ni body au frem ya kubeba kitu, roho ni nguvu ya utambulisho wa aina ya uhai na nafsi ni tabia ya roho husika.
Kwa hiyo kila kiumbe kilicho hai kina roho ya uhai ndani yake.
Hivyo basi tabia ambayo ni nafsi hudhihirisha roho iliyo ndani ya mtu.
Kama umezaliwa mara ya pili tabia za mnyama ambapo kimsingi sisi binadamu ni wanyama wa kundi la mamalia ndizo zinazouawa na kuwa nafsi hai ya pumzi ya Mungu.
Viumbe wa kiroho wana miili ya kiroho kama vile viumbe wa dunian wana miili ya flesh.ushuhuda wa Mungu mbinguni ni baba, roho na neno tofauti na ushuhuda wa Mungu huyo huyo akiwa duniani. Ushuhuda wake akiwa duniani ni roho, damu na maji hizi ndizo element alizokuwa nazo Yesu hapa duniani.
Kuna mengi ya kujifunza kuhusu hili ila hata sijui niliwakilishe kwa njia ipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante,

Tiririka tu.

Wengi wanabarikiwa.
 
ITAENDELEA......

HAKIKA yote utapata majibu yake,

Mungu akipenda kesho nitaendelea kuleta mwendelezo.

Ubarikiwe.
Kuna Binti alitoa mimba 2005, kwasasa kaokoka kweli kweli sasa akiingiabinguni 2025, atakutana na mtoto wake akiwa na miaka 20 au atakuwa Bado kachanga, na vipi watatambuana?
Mtoto wake hawezi kukua, atakuwa vile vile mchanga.

Binti hata akienda Mbinguni Mzee pia, umri wake hautazidi miaka 30 Kwa appearance maana kule watu ni umri mmoja.
kwa hiyo mbinguni kuna watoto wanaonyonyeshwa, ambao duniani walikuwa mimba zilizotolewa?
 
Hapakuwa na njaa, Wala huzuni Wala DHIKI.

Malaika wengine walikuwa wakiwahudumia WATAKATIFU MATUNDA YA MWILI WA DHAHABU. Niliona pia Malaika wakimimina juice Kwa watakatifu ambayo ilikuwa ya kipekee.

Hebu fafanua hapa...

Maana kuna mahali unataja hakuna kusikia njaa...lakini mahala pengine unataja kulikuwa na unywaji na ulaji...
 
Back
Top Bottom