Elections 2010 LIVE ON TV: Kikwete ashinda kuwa rais kwa 61.17%

WEZI WAKUBWA HAO!Alhmdulillah kila kukicha percentage ya kura za ccm inashuka!next election 20%.
 
ushindi mwembamba sana

halafu sijamwona kinana hapo!
 
Lipumba amwege upupu kwenye hiyo tume
 
Amesema walikubaliana mshindi wa pili ndiye awe mwongeaji lakini amelazimika kuongea baada ya Dr Slaa kutokuwepo.
 
hii 61.17 % baada ya uchakachuaji inanitia shaka, kama angeshinda bila uchakachuaji
 
Kura zilizoharibika ni 227889 ie 2.64% na harali ni 839394 ie 97.32%
Kuna mtu anaweza tupa kura zilizoharibika 2005 ili tuweze fanya comparative analysis
 
Nawona Nape, Komba Zakia nk

JK anaongea sasa
 
warioba yuko down sana namuona
 
Slaa ni Kiboko. aliamua kugombea miezi miwili tu iliyopita na bila maandalizi akapata 26% (au hata zaidi!). Nadhani 2015 akipewa nafasi mapema ushindi itakuwa ni kama kumsukoma mlevi.
 
Kikwete: CMM imepokea kwa furaha n amoyo mkunjufu matokeo, anawashukuru watanzania kwa ushindi mkubwa
 
JK Anasema hana hotuba ndefu ya kuchosha watu! Ummm thubutu itakuchosha wewe JK
 
iLA HANA FURAHA, KUMBE UKIWA MWIZI WA KURA HUFURAHII HATA MATOKEO , MAANA UNAJUA WATU WENGI HAWAKUPENDI ILA UMELAZIMISHA.
 
Kikwete: watajitahidi kutimiza ahadi walizotoa, zinazotokana na ilani pamoja na zile wananchi walizozitaka wakati wa kampeni
 
Jk anasema CCM wamepokea kwa furaha matokeo. Na watafanya kazi kwa Nguvu Zaidi, Kasi Zaidi na ari zaidi.

Anapongeza jinsi ushindani ulivyokuwa.
 


NEC ilitutangazia kwamba waliondikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ni 19.6m, sasa imekuwaje tena 20.1m?
ufafanuzi kidogo mjumbe kuhusu hizi takwimu.
 
1. Kuga peter mziray appt - maendeleo 1.12%

2. Kikwete jakaya mrisho/ccm - 5,276,827 61.17%

3. Slaa willibrod peter/chadema - 2,271,942 26.34%

4. Lipumba ibrahim haruna/cuf - 695,667 8%

5. Rungwe hashim spunda nccr-mageuzi 26,388 0.31%

6. Mgaywa muttamwega bhatt tlp 17,482 0.20%

7. Dovutwa yahmi nassoro dovutwa updp 13,176 0.15%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…