LIVE: Tanzania Primier League (TPL)... Simba SC dhidi ya Kagera Sugar moja kwa moja kutokea uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Hapa wakulaumiwa ni shabalala, beki unatulizia mpira golini uyu dogo anatakiwa awe anaingia km sub
 
Manula naye ni tatizo zaidi ya ZANA. Wasiojua mpira wanamlaumu Mohamed Husein kwa kosa la Manula. Manula kwa nafasi yake alikuwa anaona uwanja vizuri kuliiko Mohamed Husseni kwa hiyo aliona wazi Mohamed Huseni hana adui nyuma yake yeye alikwenda kufanya nini ndani ya hatua sita wakati beki wake hakuwa na adui yeyote karibu? Kwa nini asingemuita kwa sauti halafu akaenda kuudaka ule mpira mbele yake? Na ni beki gani atakayeacha mpira umpite wakati hajui nyuma kuna nani? Iwapo Manula angetulia golini kusingekuwa na madhara yoyote.

Pia kuna haja ya makocha kumwelekeza Manula na wakati mwengine kumkumbusha kurudi golini. Magoli asilimia 95 aliyofungwa kwenye champions league and hata ligi ya ndani huwa anakuwa amesogea mbele na kuliacha goli. Hata juzi goli la Coastal Union lilikuwa hivyo hivyo. Na vizuri zaidi kumleta kipa mwingine mwenye viwango ili ampe changamoto.

Lakini face to face na washambuliaji Manula nampa credit zake kwani hapa bongo hakuna anaemfikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…