Live Updates: Simba Sc-Wenye nchi tunaiweka nchi mbele

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001



Maandalizi yote ya tukio letu yamekamilika. Muda mfupi kutoka sasa tukio la wenye nchi tukiiweka nchi mbele litaanza.

Tunakwenda kuzindua jezi za Simba za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na tumepata baraka zote kutoka kwa mdhamini mkuu M-Bet."- Semaji la CAF Ahmed Ally.
 
Simba wanaenda kupita mule mule Yanga walipoteleza.

Yanga kujibrand kama "timu ya wananchi" ilikuwa bonge la idea ila baadae kuja kusema hatuwezi kuitangaza nchi kimataifa mpaka tulipwe imeitia doa brand yao. Walijaribu kujirudi kwenye ile barua yao ila utetezi wao kuwa hawakuwa approached na wamiliki wa Visit Tanzania ni hoja isiyo na mashiko.

Simba wanaenda kuwaadhibu kwa kosa hili na kuwanyang'anya hoja ya kuwa timu ya wananchi.
 
Kwenye barua gani?

Ile press release yao?

Mbona mle ndio wameharibu kabisa kwa kutilia mkazo kuwa maamuzi yao ya kuikataa Visit Tanzania haikuwa bahati mbaya bali walimaanisha
 
Misimu iliyopita Simba ilipoweka hiyo visit Tanzania ilipata faida gani?
 
Kwenye barua gani?

Ile press release yao?

Mbona mle ndio wameharibu kabisa kwa kutilia mkazo kuwa maamuzi yao ya kuikataa Visit Tanzania haikuwa bahati mbaya bali walimaanisha
Nakubaliana na wewe, waliharibu sana na utetezi wao ulikuwa dhaifu mno. Kwanza kwenye barua ya kiingereza maelezo yale hawakuyaweka.

Pia maelezo yao yanaonyesha kama vile SportPesa walikuja na wazo la Visit Tanzania baada ya mawazo mengine kushindikana wakati kama nakumbuka vizuri, SportPesa walisema hilo lilikuwa ni moja ya mawazo ya mwanzo yaliyokataliwa na Yanga.
 
Misimu iliyopita Simba ilipoweka hiyo visit Tanzania ilipata faida gani?
Faida ilienda kuinufaisha nchi kawaulize sector ya utalii

Lakini

Ikiwemo kuitangaza mpira wetu na kutoa fursa ya wadau wa nje kuanza kufatilia ligi yetu pamoja na Clubs zingine ambazo hazifahamiki (ikiwemo Yanga)

Kujulikana kwa Yanga kumechagizwa na Visit Tanzania waliyoitumia Simba kupitia mafanikio yake kwenye hiyo michuano.

We don't need you but you need us
 
Kumbe Yanga kuitwa timu ya Wananchi inawauma na mnatamani Simba ichukue iyo nafasi?? Duuuh mnashangaza sana
 
Yanga ndio wananchi hawaitaji kuji bland popote, walio anzisha TAA, TANU, CCM, SIMBA, RED STAR n.k ao wote wametoka katika viuno vya Yanga.
Yanga ata isipovaa jezi zenye nembo ya Visit Tanzania, uzalendo wa Yanga kwenye nchi hii haupimwi Kwa jezi Bali kupigania uhuru wa Tanzania na nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. Harakati nyingi za ukombozi wa kusini zilifanyika pale Jangwani.

Simba ilizaliwa baada ya baadhi ya waliokua wanachama wa Yanga kurubuniwa wajiondoe kwenye timu(Yanga) Ili kusaliti vuguvugu la kupambania uhuru wa nchi hii.

Wahindi na waarabu ambao walikua watawala baada ya Mwingereza na raia daraja la pili baada ya mkoloni(Mwingereza)walitumika kuwarubuni wanachama ao waliokua wa Yanga Kwa zawadi ya viatu baadae jezi Ili wajiondoe ndani ya Yanga na walifanikiwa.

Baada ya kufanikiwa kujiondoa Yanga wakapewa viatu vya kuchezea mpira na kuanzishwa timu Yao iliyayo itwa queen [emoji146] Kwa kumfurahisha Mtawala mwingereza.
Yanga ndio nchi, Yanga ndio Wananchi, itabaki hivyo siku zote ndugu wasaliti mbumbumbu fc.
 
Zungumzieni tukio la Simba. Mbona uzi unaanza kutawaliwa na habari za YANGA?
 
kumbe simba walishaachana na african carriers?....
basi ule mgogoro wa bus inawezekana kweli ulikuwepo, maana siioni logo ya african carriers hapo
 
"Niwashukuru uongozi wa Simba kwa namna walivyotupokea. Tumeridhia kutokana na mashindano ya Ligi ya Mabingwa ambayo wanashiriki ikiwa ni timu pekee kutoka Tanzania. Tumekubali kabisa kuitangaza nchi yetu kimataifa"- Meneja Masoko wa M-Bet, Allen Mushi.

#WenyeNchi
#NguvuMoja
 
"Tunakwenda kuzindua jezi za Simba za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na tumepata baraka zote kutoka kwa mdhamini mkuu M-Bet."- Ahmed Ally.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…