Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Jamani eeh,nadhani leo mtaungana na mimi kwamba huyu GJ ndo kirusi pale nyuma,leo hajacheza na tumepata clean sheet kwenye gem ngumu ya away! Akae hukohuko kwnye majeruhi daima
 
Jamani eeh,nadhani leo mtaungana na mimi kwamba huyu GJ ndo kirusi pale nyuma,leo hajacheza na tumepata clean sheet kwenye gem ngumu ya away! Akae hukohuko kwnye majeruhi daima

Apone aje atusaidie kwenye Carling Cup...ila kwenye ligi as in use au awe anaingia dk 10 za mwisho tukiwa mbele kwa goli zaidi ya tatu!
 
Beer sasa zitanyweka kiurahisi sana!Nilikuwa na msongo sana wa mawazo na matokeo ya Man City!!
Sasa vijana wetu watakuwa na confidence na nzuri zaidi week ijayo hamna mechi ya ligi sababu ya international games break!
YNWA
 
Majembe mapya yamefanya kazi ya maana leo.....timu ina quality na bench pia limesimama. Leo kuna watu tutakuwa tumewapa a second thought on their assessment about our squad.
 

Attachments

  • 1409497386873.jpg
    115.4 KB · Views: 106
  • 1409497399934.jpg
    92.6 KB · Views: 102
Jamani eeh,nadhani leo mtaungana na mimi kwamba huyu GJ ndo kirusi pale nyuma,leo hajacheza na tumepata clean sheet kwenye gem ngumu ya away! Akae hukohuko kwnye majeruhi daima

Kiongozi with all the respect kwako, that's unfair comment on your own player. Acha apone anyang'anywe namba na hao watoto lakini usimuombee kukaa majeruhi.
 
Nadhani leo BR hatalaumiwa kwa kumchezesha Moreno 'asiye na uzoefu na premier,game ya away'!Watu bhana,ha ha ha!

Last week tulisema ni makosa kumchezesha Moreno kwenye game yake ya kwanza na Man city, na MIMI nikasema hapa angemuanzisha dhidi ya spurs katika game ya away..Man city unaifananisha na spurs??..

Na leo tumecheza Diamond formation, syo 4-3-3 tuliyocheza na Man city..

Man city had Jovetic, navas, nasri wote walikuwa wanakuja upande wake...

Kwa hyo kama BR akikosea ndo tusiseme??

Perfomance ya Moreno dhidi ya Man city utaifananisha na ya Leo???
 
Wanachama tuhongere bwana, iliyowauma wajinyonge. Kazi tumeanza
 
Beer sasa zitanyweka kiurahisi sana!Nilikuwa na msongo sana wa mawazo na matokeo ya Man City!!
Sasa vijana wetu watakuwa na confidence na nzuri zaidi week ijayo hamna mechi ya ligi sababu ya international games break!
YNWA

Usihofu kiongozi, mambo yatakaa level kwani hata mbaya wetu Man City jana kakalishwa chini na watoto
 
Timu ikicheza poa wacha isifiwe ikizingua wacha iongelewe pia, dizaini Leo nimependa tulivyo cheza
 

Leo imekuwa perfomance lakini na man city ilikuwa ugeni wa premier!Sasa kama unasifia kiwango cha moreno cha leo ndo tuseme ameshakuwa mzoefu na premier baada ya mechi moja?Kuna siku tu huwa inatokea mchezaji aka underperfome lakini haimaanishi ni mbovu au hana uzoefu.Leo umeisifia diamond kwa kuwa tumeshinda lakini tungepigwa uogeiponda pia!4-3-3 tungeitumia leo na kushinda ungekuja tena na stori nyingine! Pointi yangu ni kuwa tusiwe wepesi sana kulaumu kocha au wachezaji.Tuwe fair
 

Mkuu umeongea vizuri sana...kufungwa timu zote zinafungwa tu ila criticism watu wanazotoa yaani utadhani tumefungwa mechi tatu mfululizo yaani.

Cheki jana Man City kapigwa... leo Arsenal kadroo na Leicester City. Jamani hii ligi ngumu tupunguze lawama zisizo na msingi... huyu BR kazi aliyoifanya ni kubwa mno!
 

Kuna siku gani ushaona nimeiponda Diamond au xmas tree formation hapa?? Wakati hizo ndo formations ambazo zilileta mafanikio last season!!!, na unajua ni kwa nini BR alianza na 4-3-3 katika game mbili za kwanza????

Unajua kwamba Katika 4-3-3, Hendo huwa anaPerfome vibaya??? The same to coutinho??

And ooooh!!!, unasema nilisema MORENO ni m-bovu last week, Really??..nioneshe sehem niliyosema MORENO ni M-bovu??..ulikuwa unafatilia posts zetu za usajili??..who was so.excited about us signing Moreno?? Apart from akina Pazi, Magnificent, Janjaweed na kina Tores????

Nimeanza kumjua Moreno tangu yupo Seville ya kina Rakitic mwaka Juzi, Tangu kipindi kile RMA walipokuwa so close kumsajili BUT walihairisha kutokana na Coentrao form ya msimu uliopita na Carvaraj..na hayo tushaongea sana na kina Pazi humu..

Nilichosema Week iliyopita Man City was a BIG GAME for Moreno's DEBUT, it was a tough TEST for him, and we both saw that siku ile na kilichonipelekea kusema hivyo ni kutokana na kwamba hatukuwa naye kwenye pre-season yote, mbona sikusema kuwa Lovren na Manquillo ilikuwa ni tough debut kwao against Southampton??? Coz southampton ni Average team..

MAN CITY, was a BIG TEST kwa Moreno, na kama unajua football utakuwa unajua nini maana ya DEBUT katika big games tena AWAY na unacheza na mtetezi wa LEAGUE..

Na huwez kamwe kufananisha approach ya game kama ManCity vs Stoke na ManCity Vs LFC, (hii ilikuwa game kati ya TWO TOP TEAMS katika EPL last season), so usingetegemea Pelegrin aje na mbinu kama za stoke city, Na itabidi ujue inamaanisha nini kwa kocha kushinda katika BIG MATCHES, jana kafungwa na Stoke city kwake Etihad, Lakini in TWO WEEKS, anaenda kucheza na Arsenal pale Emirate...utashuhudia mwenyewe..

Afu kitu kingine kama huwa unasoma Posts zetu kimya kimya, uwe unajitahid kuzisoma kwa umakini sana, kwani tukifungwa na tukiweka mijadala na ideas zetu humu huwa mnakaa kimya TU, na TUKISHINDA, mnajaa humu na kuanza kutoa comments za UONGO kama hizo (eti nishawahi kusema Moreno ni M-bovu!!!!!!)

Me ni shabiki wa LIVERPOOL na LFC hainilipi mshahara wowote kama kina BR, Poscoe, Marsh, Morgan na Players, Na ikiboronga wenyewe watajipoza na mishahara yao MIKUBWA, na mwisho wa msimu wanaenda na wake zao fukwe za IBZA au COPA CABANA kula raha, me nitabaki na Maumivu yangu tu na mwisho wa mwezi nitakatwa kama kawaida HELA katika my A/C kwa ajili ya LFCTV na Ile ya Membership ya Club, for whic hainisaidii chochote kile, Lakini kutokana na mapenzi yangu kwa LFC, nimeamua mimi mwenyewe kufanya hivyo, so ikiboronga kwa makosa ya kipuuzi lazima nilalamike sana humu, coz ni mimi ndiye ninayeumia zaidi kama Mshabiki na siyo kocha wala Players, coz wenyewe wanafanya kazi wapate mshahara, ndo maana leo hii AGGER AMEONDOKA LFC.

Na humu ndani muwe mnajitokeza kila siku kama LFC ipo mioyoni mwenu, IKIBORONGA AU IKISHINDA, muwe mnajaa kama leo humu, kina Pazi, The Magnificent, Tores, Malafyale, osokonoi, Ed, The Boss, Janjaweed Blac kid Gwamahala, +255, Mzee Wa Rubisi Amanijua @Punein wenyewe pia wana shughuli zao kibao za kufanya lakini kila siku wanapitia humu na KUCOMMENT katika mijadala mbalimbali katika kuifanya thread hii kuwa ACTIVE kila siku, lakini nyie wengine mnasoma kimya kimya humu, team ikushinda (which is NOT bad kwa shabikj yoyote yule), lakin kinachoboa mnaquote comments za watu wrong, kwa dhihaka na dharau.

Me nishawahi kusema MORENO ni M-BOVU???

Kwa mfano Arsenal wametoa draw leo na LECESTER CITY, kwahiyo itakuwa dhambi kwa kina Mbu na kina BAK, Kumlaumu WENGER kusuasua kuleta DM na ST mzuri???..kwa kuwa kisa tu ni Wenger??? Ndo asilalamikiwe???

BR akikosea nitaendelea kumkosoa kama kawaida..akishinda nitampongeza yeye na players wote..thats what a REAL FAN who loves his CLUB anafanya! PERIOD.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…