kijiweni kazi
Member
- Oct 9, 2014
- 10
- 0
Liverpool v Real Madrid
Hii ni Mechi ambayo inatupiwa jicho sana hasa kwa
vile inakutanisha Vigogo wenye majina makubwa
katika Historia ya Soka Barani Ulaya.
Real Madrid, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa
Ulaya, wanatua Anfield wakiwa Vinara wa Kundi A
wakiwa wameshinda Mechi zao zote mbili na
Liverpool wapo Nafasi ya 3 baada ya kushinda
moja na kufungwa na FC Basel.
Kihistoria, Real haijawahi kuifunga Liverpool kwenye
Mashindano ya Klabu Barani Ulaya kwa kukutana
mara 3 na zote Liverpool kushinda na mara ya
mwisho ilikuwa Msimu wa 2008/09 kwenye
Mashindano haya ambapo Liverpool walishinda 1-0
huko Spain na kuitwanga Real 4-0 Uwanjani Anfield
katika Marudiano.
Lakini Real ya sasa si lele mama na inaongozwa na
Mchezaji bora Duniani, Cristiano Ronaldo, na
Mfungaji Bora wa Fainali za Kombe la Dunia huko
Brazil Mwaka huu, James Rodriguez, na pia wanae
Mchezaji Ghali Duniani, Garreth Bale, ambae, hata
hivyo, kuna hatihati kama atacheza kwa vile ana
maumivu.
Kuelekea kwenye Mechi hii, Real walishinda Mechi
yao ya La Liga hapo Jumamosi kwa kuichapa 5-0
Levante na Ronaldo kufunga Bao 2 na Liverpool
kushinda Mechi yao ya Ligi Kuu England kwa
mbinde kwa Bao 3-2 dhidi ya Timu ya mkiani QPR
huku Bao la ushindi likifungwa Dakika za Majeruhi
kwa QPR kujifunga wenyewe.
Vikosi vinatarajiwa kuwa:
Liverpool: Mignolet; Johnson, Skrtel, Lovren,
Enrique; Allen, Henderson, Gerrard; Sterling,
Balotelli, Lallana
Real Madrid: Casillas; Carvajal, Ramos, Pepe,
Marcelo; Modric, Kroos, Isco; James, Benzema,
Ronaldo
REFA: Nicola Rizzoli (Italy)