Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool v Real Madrid

Hii ni Mechi ambayo inatupiwa jicho sana hasa kwa
vile inakutanisha Vigogo wenye majina makubwa
katika Historia ya Soka Barani Ulaya.
Real Madrid, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa
Ulaya, wanatua Anfield wakiwa Vinara wa Kundi A
wakiwa wameshinda Mechi zao zote mbili na
Liverpool wapo Nafasi ya 3 baada ya kushinda
moja na kufungwa na FC Basel.
Kihistoria, Real haijawahi kuifunga Liverpool kwenye
Mashindano ya Klabu Barani Ulaya kwa kukutana
mara 3 na zote Liverpool kushinda na mara ya
mwisho ilikuwa Msimu wa 2008/09 kwenye
Mashindano haya ambapo Liverpool walishinda 1-0
huko Spain na kuitwanga Real 4-0 Uwanjani Anfield
katika Marudiano.
Lakini Real ya sasa si lele mama na inaongozwa na
Mchezaji bora Duniani, Cristiano Ronaldo, na
Mfungaji Bora wa Fainali za Kombe la Dunia huko
Brazil Mwaka huu, James Rodriguez, na pia wanae
Mchezaji Ghali Duniani, Garreth Bale, ambae, hata
hivyo, kuna hatihati kama atacheza kwa vile ana
maumivu.
Kuelekea kwenye Mechi hii, Real walishinda Mechi
yao ya La Liga hapo Jumamosi kwa kuichapa 5-0
Levante na Ronaldo kufunga Bao 2 na Liverpool
kushinda Mechi yao ya Ligi Kuu England kwa
mbinde kwa Bao 3-2 dhidi ya Timu ya mkiani QPR
huku Bao la ushindi likifungwa Dakika za Majeruhi
kwa QPR kujifunga wenyewe.
Vikosi vinatarajiwa kuwa:
Liverpool: Mignolet; Johnson, Skrtel, Lovren,
Enrique; Allen, Henderson, Gerrard; Sterling,
Balotelli, Lallana
Real Madrid: Casillas; Carvajal, Ramos, Pepe,
Marcelo; Modric, Kroos, Isco; James, Benzema,
Ronaldo
REFA: Nicola Rizzoli (Italy)
 
Duuuu kweli mpira umeanza kufuatilia lini? Nne alifungiwa wapi? Moja tukamfungia kwake mechi ya maludiano, mie sina hofu na timu yangu ushindi lazima leo.
 

Last 5 previous matches CR7 hajawahi kufunga goli Anfield , lakini unaambiwa hajawahi kupoteza game hapo. Sasa unapofurahia vitu usivyovijua unachekesha.

Soma hapa: Liverpool fans shouldn't boo Cristiano Ronaldo... he'll just play better, says Carlo Ancelotti | Daily Mail Online

Mkuu wapi nimefurahia vitu nisivyo vijua? Umesoma ukaelewa nilichoandika au tu umejisikia kuleta ubishani? Kuna sehemu nimesema amepoteza gemu?

Mimi nimemzungumzia CR as a CR hajawahi score kwenye hizo game 5 za mwisho pale Anfield. So ulichoandika unaona kiko sahihi na nilicho andika?
 
Mkuu wapi nimefurahia vitu nisivyo vijua? Umesoma ukaelewa nilichoandika au tu umejisikia kuleta ubishani? Kuna sehemu nimesema amepoteza gemu?

Mimi nimemzungumzia CR as a CR hajawahi score kwenye hizo game 5 za mwisho pale Anfield. So ulichoandika unaona kiko sahihi na nilicho andika?

Calm dawn mkuu, subiri tufurahie soka, hakuna kilichoharibika, soon tutacheki game kaka.
 
liverpool.jpg
 
Wanasema dunia ina maajab saba...sasa leo la nane linatokea...pale ni anfield (the most loudest stadium)....karibuni wapinzan mshuudie show atayopigiwa madrid
 
Hakiyanan dakika ya 5 sasa vijogoo wanakimbiza balaa. Refa mchezaji wa 12 wa Madrid
 
Liverpool wanaujua mpira!Jamani team hii imeanza ku click!

Hata kama nafungwa hapa nimeonyesha soka jamani
 
Duu. Leo liver wanacheza ki'team balaa. Wakicheza hivi EPL mbona majanga
 
Back
Top Bottom