Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Mambo vipi Kops
Captain Marvelous brother za siku nyingi? Sijapita muda sana humu

Anyway naona wazi tumepata gold chance kukaa kileleni ..

Wasalaam
🙆🏿‍♀️🙆🏿‍♀️🙆🏿‍♀️🔥🔥Bro niaje mbona umekimbia sana humu.
Uzima upooo?

Za siku nyingi ni fresh kabisa.
Majogooo tunaongoza ligi. Mambo ni bam bam kabisa.

YNWA
 
Bro mambo ndio yalikuwa mengi kidogo but tuko pamoja ndugu mpaka pale tutakapopewa mwali wetu

Hivi hawa Aston villa hamuoni watakuja kutupa tabu
 
Villa naona mnawapuuzia tu wakati yamechanja mbuga sana
 
Bro mambo ndio yalikuwa mengi kidogo but tuko pamoja ndugu mpaka pale tutakapopewa mwali wetu

Hivi hawa Aston villa hamuoni watakuja kutupa tabu
Huyu tulishamalizana nae hivyo pointi tulichukua pointi 3 safi n mechi inayofuata ni May 24 2024 saa kumi na moja pale Villa Park hivyo kwa sasa kila mmoja ashinde mechi zake aafu mpaka tunafika hukoo April ndio mbio za ubingwa tutajua ni namna gani.

Kwanza kafanya jambo safiii kuwapiga Manchester City na Arsenal amewapunguza pointi haswa huku akisogea... Ni bora iwe mbio za timu 4 kwenye ubingwa kuliko mbili aisee zikiwa nyingi na burudani inakua powaa kabisa.

YNWA
 
Ile game ya Totenham inaweza Ku Tu cost ubingwa...Leo tungekuwa point tisa clear of man city
 
Msimamo wangu ni uleule
Kelleher ni the best golikipa

Good 👍

Kumbe my fellow Kop unazungumzia msimamo na sio facts?

Kama ni hivyo upo sahihi kwasababu hata Privaldinho anaamini Yanga ni bora kuliko Masandawana (Mamelody) kwasababu ndiyo msimamo wake.

Ni sawa na Malafyale anaamini kuwa Henderson ni bora kuliko Gerrard kwasababu ndiyo msimamo wake.

Ni sawa na wengi humu kuna kipindi waliamini Origi na Shaqiri ni bora kuliko Salah.

😅
 
30 minutes still struggling to find a goal against a mid table team, yet you think of beating arsenal?

Kijana Aliyekubaka jana sisi tulimuoa na Mahari ya Milioni 3 tukamtolea.
Sasa kama Mke wetu mpendwa alikunyanyasa hivi je sisi Waume tutakufanyaje utakapoingia Getoni kwetu Anfield?

Munapoanza kushabikia Mpira muwe munatuuliza sisi Wazee jinsi ya kushabikia mpira usionekane Mpumbavu.
 
 
King ngwaba hizi mechi za maelekezo, sisi huwezi kutufunga bila maelekezo, waliotufunga wote hakuna aliyetuzidi mpira ni support ya Marefa, sisi ni moto wewe.
 
King ngwaba hizi mechi za maelekezo, sisi huwezi kutufunga bila maelekezo, waliotufunga wote hakuna aliyetuzidi mpira ni support ya Marefa, sisi ni moto wewe.

Kumbuka aliyekuwa anabeba ubingwa kwa favours za Marefa ni Manure ya Ferguson na Man City ya Pep tu.

Chelsea kipindi chote cha Abramovic hakuwahi kubeba ubengwa kwa Favours za Marefa bali alipigana kiume kivyake vyake.

Hivi na wewe Arsenal na sisi LiverpoolFC tusitegemee kubeba ubingwa kwa Favours za Marefa ndiyomana mpaka sasa tuna Red Cards 4 huku tukinyimwa points 3 za wazi dhidi ya Spurs.

Kiufupi ili ushindwe ubingwa unatakiwa uyashinde mazingira magumu kama hayo bila ya kutegemea huruma.

But Anfield hata aje achezesha Arteta nadhani unajua wazi kuwa huwezi kuondoka na points.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…