TOPU OFU ZE TEBO
[emoji1593]Ni umahiri tu wa Martin Dubravka ndio umefanya Liverpool kufunga magoli 4 lakini siku nyingine yoyote basi inakuwa hata 7 kama sio 8 kabisa, kwa aina bora za nafasi walizotengeneza leo dhidi ya Newcastle
[emoji1593]Kuna muda tunaongea sana kuhusu mifumo na mbinu lakini kuna vitu ambavyo ni muhimu sana vikifanyika kwa usahihi timu inakuwa imara uwanjani .... walivyofanya Liverpool leo
1: Runs nzuri sana kwenye spaces zilizo wazi ( Salah , Diaz , Darwin , Jones , TAA )
2: Kukabia juu haraka sana pale mpira ukipotea kwa idadi kubwa ya wachezaji ( risk sana lakini inalipa . Maana ukikabia juu sana maana yake nyuma unaacha walinzi wawili tu wa kati )
3. Pass and Move : achia mali halafu tembea kwenye nafasi ni ngumu sana kukabiliana nayo maana kama Newcastle unashindwa kujua nani yupo wapi wa Liverpool
4: Piga mpira golini unapopata nafasi ya kufanya hivyo badala ya kuongeza pasi ( stop overplaying )
Hivi vyote Liverpool walifanya kwa usahihi sana , mapungufu yalikuwa sehemu tatu tu leo kwao
1: Kuna nyakati kadhaa walikuwa wanapoteza mali kirahisi sana tena hata bila kwenye presha : Hasa Szobo : katika mechi kama tatu hivi amekuwa chini sana ya kiwango
2: Umaliziaji wao : hii inamuangukia Darwin Nunez nafasi kama tatu nzuri sana . Amuangalie mwenzake Alexander Isak
3: Walipokuwa wanakabia juu sana : TAA na Gomez nao wanasogea juu sana maana yake wanaacha space kubwa ambapo mara kadhaa Newcastle walipokuwa wanaishinda pressing ya Liverpool walikuwa wanatumia space ambayo wanaiacha TAA na Gomez .
[emoji1593]Newcastle kiukweli leo ilikuwa ishu ya kucheza kwa matumaini , kwamba Dubravka kwenye ubora wake na wao wafunge magoli ya counter attacks au mipira iliyokufa .
NOTE
1: Gordon dribbling yake na kasi yake [emoji91]
2: Isak kama haendi vile kumbe anaenda aisee
3: Ile pasi ya Mo Salah kwenye goli la tatu " Outer Pass " [emoji91]
4: Luis Diaz leo nimeona kile kiwango kama alichokuja nacho [emoji91]
5: Jones kama alivyocheza dhidi ya Arsenal na leo hivyo hivyo [emoji91]
6:Martin Dubravka saves za leo [emoji91] kapunguza sana idadi ya magoli
7: NIMEFURAHI ( mtajua wenyewe kwanini nimefurahi ushindi wa Liverpool ) [emoji3] wale wana kelele sana
FT: Liverpool 4-2 Newcastle
AMBANGILE