Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Thats football. Kila mtu na pressure zake kwa aina ya mchezaji na uchezaji anaoupendelea.

Wapo wengine kwenye build up wanalaumu wachezaji kwa nini huko nyuma mipira si iende mbele? Ndio Modern Football inavyotaka.
niko hapa na mimi mmojawapo

Mpira uende mbele, ndio maana Henderson na Lovren nilikuwa nawachukia wazee wa back pass
 
Ubinafsi Salah umemuishia baada ya Mane kuondoka lakini kipindi kile wapo wote dah majamaa walikuwa na nani awe mkubwa

Salah sasa ana madogo hashindani nao bali anashirikiana nao
 
Edwards anatosha, ni yeye aliemleta Klopp Liverpool badae Klopp akabadili gear angani na kuanza kumwingilia na hatimae Edwards yakamshinda na kusepa bila Edwards hakuna Klopp Liverpool, hakuna Salah, VVD nk huyu mwamba anajua kuchakata data kujenga kile anachotaka mwalimu lakin sio muumin mkubwa sana kuwapa wazee mikataba mirefu anaaminia mchezaji akishageuka upande wa pili wa mwaka 30 basi hapo ni wa aidha kuuzwa ama kuachiwa...lakin pia kwa data zake zinampa fomu ya mchezaji husika miaka ijayo ndio maana aligoma sana kuwapa nyongeza Gini, Keita, Henderson, Milner, Lallana, Mane nk alijua fika hapo mbele mishe zao zitakua na mashaka na wote ni mashahidi kwamba alikua sahihi kwan hao wachezaji kwa sasa ni kama hawamo kwenye ramani za wachezaji wakali...

Huyu bwana alikomaa sana kwa Salah alikiona kile ambao leo hii tunakiona..

Ujio wake Edwards unaweza kua kaa la moto kwa Allison, VVD, Salah, Thiago, Matip, Robertson ambao aidha hatatoa nyongeza ya mkataba ama atawauza kama akipata ofa na sana sana Salah hapo naona safari yake kama inazid kusongea.

YNWA
 
Unless uniambie business perception side lakin kwa Edward sio muumin wa ku retain over 30yrs klabuni kwa mud mrefu sana kwanza ni costly mishahara yao lakin kwa bajeti ya FSG ni pigo kubwa kwa payroll itambana zaid kwenye usajili..
Ikiwa business side outweighs foot ball side anaweza akakumbali kuwapa nyongeza.. Muda utasema ndio maana anataka full control na sio kama hii ya Klopp alikua kama rubber stamp anayotaka Klopp wao ni ye yes....

YNWA
 
Alafu Klopp bhana kipindi cha nyuma alikuwa hawatumii hawa makinda, eti baada ya kutaka kuondoka ndio anawatumia sana na mafanikio yanaonekana sijajua kwanini tu.
sio kweli wewe labda hufuatilii Liverpool,klopp toka zamani ni muumin wa falsafa ya makinda
amewapa nafasi wengi,na walioendelea wameendelea
Trent Alexander Arnold ni mojawapo alipopewa nafasi akaprove mpaka leo yupo alipo,Kuna Curtis Jones pia
miaka yote aliyopo Liverpool makombe ya FA na league amekuwa akiwapa nafasi, Sasa sijui unamuongelea Klopp yupi?
 
View attachment 2921827niko hapa na mimi mmojawapo

Mpira uende mbele, ndio maana Henderson na Lovren nilikuwa nawachukia wazee wa back pass

Hahah Henderson ule tu uwezo wa kuukokota mpira avuke msatari hana, back bass za kutosha wide pass za kutosha, mpaka mechi inaisha. Captain ambaye huwezi kumuona wakati muhimu kama VVD juzi Gerrard mara kibao ila famous Istanbul 2005.

Nikumbushe ya Henderson.
 
Ubinafsi Salah umemuishia baada ya Mane kuondoka lakini kipindi kile wapo wote dah majamaa walikuwa na nani awe mkubwa

Salah sasa ana madogo hashindani nao bali anashirikiana nao

Ushindani ni jambo zuri sana kwenye timu, ila walichokosea hawakujua ni wakati gani muhimu zaidi ninyime na wakati gani funika kombe mwanaharamu apotelee huko..!!! Nimpe afunge sifa itapata timu.
 

Jamaa nilimkubali sana toka aje LFC na kilichonishawishi ni uwezo wa kuziona talents kwa bei nafuu zikiwa bado chini sana. Na mauzo yake bado alijua kufanya biashara.

Sioni kama Edward atafanya yote haya kwa wakati mmoja labda 1-3 season ili asiathiri kikosi moja kwa moja.
Naamin VVD Beckor na Salah bado watakuwepo, ila Robbo ndio mashaka yangu ni sell au mkataba uishe aondoke. Matip & Thiago haihitaji hata uwepo wa Edward kila mtu anaona hali halisi.
 

Yes ishu ya Salah ni kibiashara zaidi. Na bado Salah uwanjani anakupa ambacho hao youth hawakupi. Timu iwe nzuri au iwe mbaya.

Over 30’ watakao baki i think alison vvd & salah, kuna watakaoachwa na kuuzwa Matip, Thiago, Adrian, hawa free agent itakuwa ngumu kuwaondoa another 3 senior players labda after 1-2 seasons huko.

Na kocha ajaye pia maana Lazima kocha aje na mapendekezo yake pia. Kuwa na full control ina side effect kama mtu anaamini yake ndio sahihi ila ya wengine sio sahihi isiyo kama Klopp kwa akina Milner, Keita, Ox, Hendo n.k
 
Alafu Klopp bhana kipindi cha nyuma alikuwa hawatumii hawa makinda, eti baada ya kutaka kuondoka ndio anawatumia sana na mafanikio yanaonekana sijajua kwanini tu.

Aliwapa nafasi sema hivyo hawakufikia level hizo isipokuwa

Trent.[emoji736]
Jones.[emoji736]
Kelleher.[emoji736]
Bajcetic (if not injury angekuwa anaelekea kuwa senior player).
Elliot.[emoji736]
Kaide Gordon (alipata injury ya muda mrefu ndio amerejea).
Sheyi Ojo.
Rhian Brewster
Ben Woodburn
Conor Randall
Neco Williams
Billy Koumetio
Harry Wilson.

Wengi hapo walishindwa kufikia level za juu, ila kama ulikuwa haupitwi na mechi za Liverpool na unazifuatalia kwa ukaribu walau hao niliowataja utakuwa unawajua.


Na hawa unawaongelea kwa sasa wengi last 2-3 seasons walikuwa na miaka 16-18, hivyo ilikuwa bado huwezi kuwachezesha wote hawa kwa wakati mmoja.
 
Jones anachezaje mbele ya Gini?

Trent alipata namba baada ya Clyne kuumia tofauti na hapo huwezi kumtumia kama mfano

Klopp sasa hivi madogo anawatumia kuliko kipindi chochote kile tangu awe pale mitaa ya Merseyside
 
Kupiga kelele uwanjani
 
Ila mechi za EPL alikuwa hathubutu aisee, mpaka kikosi chake nilikuwa nishakikariri

Lakini kwa sasa hivi anawaanzisha hata mechi za EPL

Ulikuwa humwambii chochote kwa wale wazee wake akina Lallana, Chamberlain, Milner, Origi n,k hawa ndio mara kwa mara walikuwa wanaingia kutoka benchi

Makinda wanabaki tu wamekalia mbao ndefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…