UPDATED ZUBIMENDI DEAL.
Liverpool walitaka kumsajili kwa udi na uvumba Zubimendi kutoka Real Sociedad ila deal likafa kwa sababu nayoweza kuiita LOYALTY.
Zubimendi amekulia Sociedad toka akiwa na miaka 12 mpaka hivi sasa, its his club boyhood. Liverpool walivutiwa nae na walitaka ku trigger his real clause ila ikabaki kwa Zubimendi kusema Yes/No. Zubimendi alikubali deal la kuondoka Sociedad na kuhamia Liverpool, lakini utata ukaja kwa Sociedad wakamtaka ajifunge kwenye kipengele cha buy out clause maana yake ni kwamba ajinunue mwenywe kwa £51m ambacho ni kujichonganisha na mashabiki na kuonekana msaliti au abaki na kuongezewa mkataba utakomfanya kulipwa pesa nyingi kuliko mchezaji yeyote yule pale Real Sociedad. Zubi aka turn out his mind kuondoka na kuamua kubaki Sociedad.
Ishu imekuja kuwa ngumu hapa;
Liverpool walimuahidi kumlipa Triple ya anachochukua sasa hivi Sociedad (£50k per week) kwa kutua kwake Anfield angelipwa (£150k per week) maximum. Ikumbukwe mchezaji anayelipwa pesa nyingi Sociedad ni Mikel Oyarzabal kitita cha €69,231 per week. Baada ya Zubi kukataa ofa ya Liverpool ili kupata reward ya his loyalty kwa Sociedad mambo yamekua magumu huko Sociedad. Kwa mujibu wa wakala wake anasema Zubi alikubali kubaki kama uungwana kwa Sociedad ila inavyoonekana mambo yanaenda kinyume na makubaliano.
Kuna taarifa LFC wanaweza kurudi kulifufua deal upya na kuona uwezekano wa kumchukua Zubi.
Up Reds
YNWA.