Anaejua anakotupeleka Edwards na Hughes ni @TheMoNA [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]mie wala sielewi ndugu yaani [emoji2307][emoji2307]... Hatukua na mapungufu upande wa kipa wala winga wa kushoto lakini tazama jamaa zako walivyosajili.
Unless hii Slot ball ieleweke mapema na kusiwe na majeruhi sioni tukiwa contenders popote aisee.
Huyu dogo lile jeraha naona halikua powa sana kiasi anahitaji ligi ambayo itakua haina mishe kama EPL ndio maana wanamtoa kwa mkopo binafsi angebakia kama serial sub mpaka pale sasa angefaa.
YNWA
Hahah [emoji81][emoji81][emoji81] Mie kibaraka wa Edward na Hughes dah.!!!
Anyway ngoja nijaribu kuelezea mambo fulani hivi. Kuhusu hizi Sajili.
Tukianza na Academy.
Hakuna muda sahihi zaidi wa kuuza academic players kama wakati huu. Why??
Wamepanda value sababu ya Carabao last season na zile mechi walizocheza btn Feb-March. Hakuna namna wanaweza kuingia first eleven hata under Klopp kama sio injured forced him wasingepata nafasi.
Uhalisia na matarajio ndio yanatuangashi big time hata kwenye maisha ya kawaida. Bobby Clark, Carvalho, Blair hawa wasingeweza kuingia kwenye timu ya wakubwa hata kuwa Squad players. Clark at the age of 21 bado hajawa Squad player?? Huoni ni uongo kusema ataingia kwenye senior team?? Jones alianza at the age of 17-18 watu tukawa na matarajio makubwa kwake binafsi gari lake nilipanda those days. What about Trent?? Vipi kuhusu Kelleher? Kawaida at 17 hivi to 19 unaonesha every quality ya kuaminiwa kwenye senior team. See Trey Nyoni?? Ndio maana huwa tunamkataliw
Saint Anne kuhusu Kelleher kuichukua no. Ya Beckor kwa sababu kwa umri wake Alison alikuwa already top top GK. At 25 Alison alikuwa LFC no. 1 GK and Brazil.
Umri na no. Havidanganyi.
Kuna muda naona tunawa hype our academic players. Unawakumbuka hawa jamaa
—> Ben Woodburn
—> Rhian Brewster
—> Harry Wilson
—> Jordan Ibe
Na matarajio yetu?? Hawakuwa vile tulivyodhania why?? They were never be top talent with big club materials.
Musialowski tukamuita Polish Messi, ila hiyo ameondoka as a free agent kama ni top talent asingekosa timu hata championship huko ila unajua alipoenda?? Ameenda Cyprus timu inaitwa Omonia good thing inashiriki Conference anaweza kuonekana.
Watu wanalalamika kuhusu Carvalho jamaa kipaji kipo ila kuna sababu isiyosemwa as to why Klopp alimsajili mwenyewe kwa kumsubiri, alikuwa atue winter 2022 ila mambo yakaenda kombo ikabidi achukuliwe summer 2022. Licha ya kusubiriwa huko ila hakupata nafasi ndani ya kikosi cha Klopp akaishia kwenye mikopo. Mchezaji wa hivi ukipata £27M unaanza kuikataa?? Ngumu, cash on him maana huenda next time ukaishia kupata chini ya hapo.
Academic deals are good so far.
Senior Team.
Hapa sasa ndio pagumu sana, maana haka ka utamudi kapo toka Klopp atengeneze timu ya kuogofya. Tulihitaji DM tukaletewa Gakpo na maisha yakasonga. Hapa dirisha likifungwa bila signing ya maana hasa DM/LCB nitakuja kutoa neno kwa sasa tuyaache. Ils ukinipa kati ya DM na LCB, Nachagua LCB over DM why?? Build up from behind inahitaji LCB mwenye uwezo wa maamuzi mazuri na uwezo wa kuzipiga passes, Tsimikas ni mzuri ila ahead of Robbo atacheza Robbo na Robbo sio yule tena injury za mara kwa mara na sio modern LB ni mzuri wa safari ndio maana kwa Klopp alikiwasha sana ila for possession football he is not good enough.
Chiesa sio injury prone kama wengi walivyomezwa na Media. Ishu ya Chiesa ipo hivi.
Jamaa alitaka New contract ambayo Juve walishindwana na hiyo contract hivyo akakataa kuongeza kwa matakwa na Juve. Chiesa contract yake imebaki 12 months kuliko kuondoka for free wamuuze tu ndicho kilichofanyika, ila wengi wanaamini Juve wamemkataa hapana.
Kuhusu injury prone si kweli kama inavyokuzwa sana na Media nyingi. Alipata ACL 2021-2022 ambayo ilimuweka nje muda mrefu karibu 3/4 ya mwaka. Hii tuliishuhudia kwa VVD 2020/2021. Hii lazima imuathiri mchezaji kimwili na kiakili. Vvd aliporejea tuliona uchezaji wake ila kadiri siku zinavyosogea uoga inampungua mpaka kumuisha. Last season alikosa only six games kutokana na injury less than Jota.
As time goes atakaa sawa tu kama alivyokaa vvd. Kwa nini naona hivi?? Aina ya kocha aliyepo kwa sasa, possession football with less intensity will reduce injury crisis. Unakumbuka Szobo na Keita kwa nyakati tofauti wakiwa Leipzig, they were injury free, ila intensity game ya Klopp miili ilishindwa kukabiliana nayo.
“It is a surprise deal of the summer”
Six frontline ni depth nzuri sana, Chiesa is not directly through in atapata game time itakayomsaidia kukaa sawa. Uwezo wake hauna any doubt anatumia miguu yote vizuri, dribbling nzuri, Pace ya maana kabisa…
Where are we heading??! Kwenye timu ya makombe, how and when we have to wait & to see it. Ila mipango ni mizuri tu, tunakusanya pesa kwa mipango mirefu na mifupi. Naamini Edward na Hughes watafit sana kwenye sera ya Sell to buy.
Up reds YNWA.