COMPARED: Liverpool's Premier League passing networks from 2023/24 and 2024/25. [emoji837]
View attachment 3122369
Spot the difference. [emoji28]
The MoNA hii kitaalamu unaielezea vipi?
Direct football vs possession football.
Let 2023/2024 be Klopp
And 2024/2025 be Slot
Klopp:
Klopp ni muumini wa direct football, na hii direct football lengo lake ni twende mbele tukafunge magoli. Tunafungaje ?just attack, attack, attack, shambulia aggressively. Hii ni mbinu wanayotumia wanyama wala nyama, hawakupi pumzi ya kufikiria cha kufanya, no time for reasoning, na kama hauna huo muda lazima upanic uingie kwenye mtego (ujae kwenye mfumo akubanike) wa anayekushambulia.
Klopp system ni Heavy Throttle Metal football, geggen pressing, electrical football, just keep ambush untill we get 1 and 2 and 3 untill the last whistle kisha tuone tumepata nini. Kwenye mfumo huu hauhitaji sana technical players, hauhitaji football brainers, zaidi unahitaji energetic players, athletic ones, horse power, wanajeshi haswa, thats why Klopp aliweza kubeba major trophies na wachezaji wa kawaida kwa hadhi ya LFC na EPL Champions.
Klopp hakuwa prioritize na ball control, he wants goals, akipige kwenye turn overs (ETH alisema baada ya Man utd 0-3 LFC, liverpool walitumia sana turnovers na kwenye turnovers wapo vizuri sana watakuua tu), counter attacks. Kwa Klopp alitumia highline with 2 CB’s ( RCB & LCB), umbali wa kipa na CB’s ni mkubwa ili akubananishe kwenye nusu yako huku nusu yake akiwa salama (risk ila inakulipa kama una wachezaji wazuri mentally). Kwenye ball movement kuanzia nyuma aliwatumia sana LB, RLB, RCB and RB, plus DM. Hapakuwa na position interchanges thats why ukiangalia hapo kwenye picha, unaona karibu kila eneo kuna mchezaji wa no husika. Kama ni LB yupo kwenye position yake, RB yupo kwenye position yake. Klopp haku involve sana his MF’s katika kutengeneza nafasi za kufunga, na alitumia sana 2-1 one shape (two CB’s n 1 DM). Highline ya Klopp unaona wachezaji nane wapo kwenye nusu ya mpinzani huku wawili wamebaki nusu ya juu ya eneo lake kama nilivyosema huko juu. Klopp hakuwa involve LW, FW & RW kwenye ball movement, walikuwa tayari kupokea long balls na kuendeleza mashambulizi.
Klopp hana haja na kubembeleza, kuwa mvumilivu, katika kulitafuta goli anakuja na 120 kwenye kona shaaa, wanasema mwendo wa ngiri mkia juu.
Kwa mfumo huu unahitaji wachezaji wanariadha wazuri, mapafu ya mbwa kichaa, kuhimili hiyo energy throughout 90’ mins & entire season.
Slot:
Slot ni possession football man, anapenda kutumia miundo ambayo, kwanza utaweza kutumia passes katika kulitafuta goli. Pasi za uhakika, kupokea, na kufanya mitembeo hata kwenye maeneo finyu sana (tight areas). Sasa msingi wa mfumo huu ni kuwa na technical players, ball carriers, passers, visionaries, ili sasa watimize majukumu ya possession (kipao mbele ni ball control, pass za uhakika na quality one).
Movement yake hapo, kwanza anabaki na mabeki watatu kwenye nusu ya eneo lake, wanakuwa kwenye eneo lake la katikati ambapo kuna RCB, LCB & LB. Kwenye nusu ya eneo la mpinzani kuna wachezaji saba lakini sasa walivyokaa wanakupa tight SPACE, kwa sababu wapo karibu karibu, kati ya mchezaji na mchezaji. Mstari unaofuatia wapo watatu na wa mwisho wanne japo mmoja kama yupo ndani kidogo huyo AM.
Again Slot movement yake inahusisha, RB, RCB,LCB,LB, na LW ndio msingi wa kufungua opponent. Hapa Slot mtu hawi involve sana kwenye ball control ni LW & FW.
Ukiangalia hiyo picha, utaona kuna pattern kadhaa zinaweza kutumika hapo wakati wa ball control, kwa sababu ni possession football lazima pattern ziundwe. Ukiangalia RCB, LCB & RCM hawa wanakupa triangle pattern, RCB, RB & RCM wanakupa triangle pattern, LCB, RCM & LCM, wanakupa triangle pattern, na nyingine tu wanakupa. Chukua LCB, RCB, RB, RCM & LCM kuna option wanakupa hapo. Maana yake sio lazima mcheze kwa pattern hizo muda wote, a ah. Ila muwe karibu karibu muda wote kwa sababu msingi wa sisi kumiliki mpira ni pasi fupi na ndefu kwa hiyo its a matter of SPACE & TIME.
Note:
Hii picha ipo kuelezea attacking wise. Mifumo yote ni mizuri, ila una watu wa kukutekelezea huo mfumo? Mwanzo wa kufeli mfumo ni kukosa watekelezaji wa mfumo.
Klopp vs Slot.
Highline Yes, ila:
Klopp alipenda wachezaji wengi wawe eneo la mpinzani.
Slot anapenda wachezaji wachache.
High pressing Yes, ila:
Klopp anapenda throughout the match
Slot anachagua kutokana na mpinzani na wachezaji alio nao, not all the time.
Build up:-
Klopp alipenda 2-1 shape
Slot anapenda 3-2, 2-2,mpaka 3-3 shape.
Slot ameongeza some small details kutoka kwa Klopp, ambavyo huenda angevifanya Klopp, tungekua naye bado. But Klopp is Klopp ana misimamo yake na misingi yake aliyoiamini. Kudo to the gaffer, time for Slot to show the world of football, what is capable of.
Up LiverpoolFC
Ynwa’