Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Klopp will resume his mentorship of Pep Lijnders, it seems. RB might be grooming Pep for the Leipzig job? Tbh, I hope Klopp doesn't stay at RB for more than a couple years because I think he has more to offer elsewhere, but regardless, he has left his mark on LFC, and the culture of the club that he developed over almost a decade is welcoming its next footballing leader as Klopp moves onto his next project, influencing much of elite football worldwide. I bet he could fix FIFA
 
Screenshot 2024-10-11 at 11.17.09 AM.png
 
COMPARED: Liverpool's Premier League passing networks from 2023/24 and 2024/25. 🔴
IMG_20241012_082724_685.jpg


Spot the difference. 😅
The MoNA hii kitaalamu unaielezea vipi?
 
COMPARED: Liverpool's Premier League passing networks from 2023/24 and 2024/25. [emoji837]
View attachment 3122369

Spot the difference. [emoji28]
The MoNA hii kitaalamu unaielezea vipi?

Direct football vs possession football.

Let 2023/2024 be Klopp
And 2024/2025 be Slot

Klopp:

Klopp ni muumini wa direct football, na hii direct football lengo lake ni twende mbele tukafunge magoli. Tunafungaje ?just attack, attack, attack, shambulia aggressively. Hii ni mbinu wanayotumia wanyama wala nyama, hawakupi pumzi ya kufikiria cha kufanya, no time for reasoning, na kama hauna huo muda lazima upanic uingie kwenye mtego (ujae kwenye mfumo akubanike) wa anayekushambulia.

Klopp system ni Heavy Throttle Metal football, geggen pressing, electrical football, just keep ambush untill we get 1 and 2 and 3 untill the last whistle kisha tuone tumepata nini. Kwenye mfumo huu hauhitaji sana technical players, hauhitaji football brainers, zaidi unahitaji energetic players, athletic ones, horse power, wanajeshi haswa, thats why Klopp aliweza kubeba major trophies na wachezaji wa kawaida kwa hadhi ya LFC na EPL Champions.

Klopp hakuwa prioritize na ball control, he wants goals, akipige kwenye turn overs (ETH alisema baada ya Man utd 0-3 LFC, liverpool walitumia sana turnovers na kwenye turnovers wapo vizuri sana watakuua tu), counter attacks. Kwa Klopp alitumia highline with 2 CB’s ( RCB & LCB), umbali wa kipa na CB’s ni mkubwa ili akubananishe kwenye nusu yako huku nusu yake akiwa salama (risk ila inakulipa kama una wachezaji wazuri mentally). Kwenye ball movement kuanzia nyuma aliwatumia sana LB, RLB, RCB and RB, plus DM. Hapakuwa na position interchanges thats why ukiangalia hapo kwenye picha, unaona karibu kila eneo kuna mchezaji wa no husika. Kama ni LB yupo kwenye position yake, RB yupo kwenye position yake. Klopp haku involve sana his MF’s katika kutengeneza nafasi za kufunga, na alitumia sana 2-1 one shape (two CB’s n 1 DM). Highline ya Klopp unaona wachezaji nane wapo kwenye nusu ya mpinzani huku wawili wamebaki nusu ya juu ya eneo lake kama nilivyosema huko juu. Klopp hakuwa involve LW, FW & RW kwenye ball movement, walikuwa tayari kupokea long balls na kuendeleza mashambulizi.

Klopp hana haja na kubembeleza, kuwa mvumilivu, katika kulitafuta goli anakuja na 120 kwenye kona shaaa, wanasema mwendo wa ngiri mkia juu.

Kwa mfumo huu unahitaji wachezaji wanariadha wazuri, mapafu ya mbwa kichaa, kuhimili hiyo energy throughout 90’ mins & entire season.


Slot:

Slot ni possession football man, anapenda kutumia miundo ambayo, kwanza utaweza kutumia passes katika kulitafuta goli. Pasi za uhakika, kupokea, na kufanya mitembeo hata kwenye maeneo finyu sana (tight areas). Sasa msingi wa mfumo huu ni kuwa na technical players, ball carriers, passers, visionaries, ili sasa watimize majukumu ya possession (kipao mbele ni ball control, pass za uhakika na quality one).

Movement yake hapo, kwanza anabaki na mabeki watatu kwenye nusu ya eneo lake, wanakuwa kwenye eneo lake la katikati ambapo kuna RCB, LCB & LB. Kwenye nusu ya eneo la mpinzani kuna wachezaji saba lakini sasa walivyokaa wanakupa tight SPACE, kwa sababu wapo karibu karibu, kati ya mchezaji na mchezaji. Mstari unaofuatia wapo watatu na wa mwisho wanne japo mmoja kama yupo ndani kidogo huyo AM.

Again Slot movement yake inahusisha, RB, RCB,LCB,LB, na LW ndio msingi wa kufungua opponent. Hapa Slot mtu hawi involve sana kwenye ball control ni LW & FW.

Ukiangalia hiyo picha, utaona kuna pattern kadhaa zinaweza kutumika hapo wakati wa ball control, kwa sababu ni possession football lazima pattern ziundwe. Ukiangalia RCB, LCB & RCM hawa wanakupa triangle pattern, RCB, RB & RCM wanakupa triangle pattern, LCB, RCM & LCM, wanakupa triangle pattern, na nyingine tu wanakupa. Chukua LCB, RCB, RB, RCM & LCM kuna option wanakupa hapo. Maana yake sio lazima mcheze kwa pattern hizo muda wote, a ah. Ila muwe karibu karibu muda wote kwa sababu msingi wa sisi kumiliki mpira ni pasi fupi na ndefu kwa hiyo its a matter of SPACE & TIME.

Note:

Hii picha ipo kuelezea attacking wise. Mifumo yote ni mizuri, ila una watu wa kukutekelezea huo mfumo? Mwanzo wa kufeli mfumo ni kukosa watekelezaji wa mfumo.

Klopp vs Slot.

Highline Yes, ila:

Klopp alipenda wachezaji wengi wawe eneo la mpinzani.
Slot anapenda wachezaji wachache.

High pressing Yes, ila:
Klopp anapenda throughout the match
Slot anachagua kutokana na mpinzani na wachezaji alio nao, not all the time.

Build up:-

Klopp alipenda 2-1 shape
Slot anapenda 3-2, 2-2,mpaka 3-3 shape.

Slot ameongeza some small details kutoka kwa Klopp, ambavyo huenda angevifanya Klopp, tungekua naye bado. But Klopp is Klopp ana misimamo yake na misingi yake aliyoiamini. Kudo to the gaffer, time for Slot to show the world of football, what is capable of.

Up LiverpoolFC
Ynwa’
 
Emotional vs Reality…


Unawaacha waamini kile wanachoamini but He will be remembered among the best.

Ynwa Jurgen Nobert Klopp.


Ilikuwa 24 April 2013 pale BVB Stadion Dortmund, Dortmund ilipowakutanisha timu mbili zenye daraja tofauti katika ulimwengu wa soka kati ya, Real Madrid na Borussia Dortmund kwenye michuano ya usiku wa ulaya, maarufu UEFA CHAMPIONS LEAGUE hatua ya nusu fainali.

Ilikuwa ni mechi ya pande moja on paper kutokana na Dortmund kutokuwa timu maarufu masikioni na machoni pa mashabiki wengi wa kabumbu duniani, haikua na mchezaji maarufu wala kocha maarufu wakati ule.
Ilionekana wazi Madrid atamtoa Dortmund na kutinga fainali, kutokana na uzoefu, aina ya wachezaji waliokuwepo na kocha aliye naye.


Basi majira ya saa 21:45 kama ilivyo ada ya michuano, timu zikaingia uwanjani, ikapigwa “UEFA ANTHEM” vikosi vikaoneshwq, hapo ndipo watu wakazidi kuona urahisi wa Madrid kushinda mechi ile.

Dortmund kikosi kiliundwa na:

Weidenfeller

Piszcek Subotic Hummels Schmeilzer


Bender Gundogan


Blaszczykowski Gotze Reus


Lewandowski



Higuain

Ronaldo Modric Ozil


Alonso Khedira



Contrao Pepe Varane Ramos


Lopez

Madrid iliundwa na full package.

Kipyenga kikapulizwa dk ya 9 kijana asiyetambulika na dunia ya mpira Lewandowski akaingia kambani, watu tukaona wamechokoza nyuki tu hawa ushindi kwa madrid haukwepeki. Dk ya 43 Cr7 akarejesha ikawa 1-1 mpaka HT.

Second Half ukapigwa mpira mmoja, wa fainali, HEAVY THROTTLE MENTAL, GEGGEN PRESSING, ELECTRIC FOOTBALL.

“Kipindi hicho nilikuwa shabiki pia wa Madrid, niliichukia Barca kwa mpira wake wa uonevu ule, ila kwa sasa siwapendi Madrid kwa sababu wamenionenea sana, last 5 matches they have won all, ikiwemo two CL final.”

Madrid hawakuelewa wao ndio underdog au Dortmund ndio underdog, mpaka kipyenga cha mwisho Dortmund 4-1 Madrid magoli yote manne yakafungwa na Robert Lewandowski kijana kutoka Poland, ndipo ilikuwa mechi ya kujitambulisha duniani who is he. And the rest is history.

Kwenye touchline ya Dortmund alisimama kocha mjerumani anaitwa Jurgen Norbert Klopp, jamaa aliitoa Dortmund kwenye hadhi ya chini sana na kuipa hadhi moja ya timu ngumu kukutana nayo nyakati zile. 2nd leg Madrid won 2-0 wasn’t enough for qualification with agg was 4-3, book his 1st CL final as a coach.

Wakaingia finali vs Bayern ambayo nao walitoka kumtoa muhispania Barcelona iliyokuwa bado ina ubora wake. Unfortunately Klopp and his boys didn’t win that final.

Klopp anastahili kuwa na makombe mengi zaidi ya yale aliyoyashinda ukilinganisha na idadi ya fainali alizozicheza.

Klopp ni mjenzi huru, mpe timu yako isiyojiweza kama utd ya sasa inayoishi maish ya Sir Alex kwenye zama za Pep, naye ataijenga na kuwa tishio baada ya hapo mshindwe wenyewe kuendeleza.


Your excellence will forever be at Anfield Jurgen Norbert Klopp.

Ynwa’
MoNa katika ubora wako...... Umenikumbusha mbali sana. Miaka hii Liverpool tunahangaika na Wasenegali akina Fadiga na Mfaransa wetu Cisse
 
MoNa katika ubora wako...... Umenikumbusha mbali sana. Miaka hii Liverpool tunahangaika na Wasenegali akina Fadiga na Mfaransa wetu Cisse

Hahahah hapo kwenye ramani ya mpira hatupo, tunatembelea Historia, tu.
Msimu mzima mnakusanya points zenu 56, mkijitahidi sana 62,

Tunasema Those days.
 
You know he will be next szobo no doubt
 

Attachments

  • 20241012_171735.jpg
    20241012_171735.jpg
    1.9 MB · Views: 6
Kuna baadhi ya watu walitaka “Pep Lijnders” achukue mikoba ya Klopp, lakini anachokifanya kwa sasa is too much worse than the worse itself.

Hii ni kuanzia 1/9/2024 to 6/10/2025

Rapid Wien 3-2 Salzburg

Sparta Prague 3-0 Salazburg

WGL Tirol 0-0 Salzburg

Wiener Victoria 0-4 Salzburg

Salzburg 2-0 Austria Wien

Salzburg 0-4 Brest

Sturm Graz 5-0 Salzburg

Jamaa anachapika sana huko, sijui hajaiba material kwa J. Klopp, wanambutua sio domestic league au huko CL,

Ynwa’
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom