choza choza
JF-Expert Member
- Jan 17, 2019
- 2,081
- 3,831
Huyu mzee kufuga deadwoods ndio kumemfanya 8 years 1pl titleHakumchoka Lovren, Sakho, Henderson, Milner, Lallana, Keita, Karius, Mignolet nk bila kuwapa nafasi...
Klopp hua ni muumini wa kutoa muda kwa wachezaji yupo tofauti na wengine hii ina mazuri na mambya yake...
Wapo walioshindwa kabisa kumuonyesha Klopp anachokitaka kama Solanke, Grujic, Kabak, Arthur Melo nk nk...
Kwa Pep ni njia moja tu upo kwa mfumo ama haupo tazama Philips, Danilo, Nolito, Mendy nk Pep hanaga muda wa kusubiri ni kupiga bei ama kusota benchi na yeye kuingia sokoni kwa bahati mbaya Klopp hama matajiri wa mafuta wa kumpa anachokitaka sana sana yeye Klopp' anakomaa na kufundisha alionao mpaka wafike levo anazohitaji...
YNWA
Lakini pia simlaumu sana maana ni mfumo wa wamarekani, Nunez tunaye sana maana FSG hawawezi kupa 85m kisha misimu miwili ijayo wakupe tena hela kwa nafasi ile ile
Hilo hata Man United lipo, Anthony wanae sana
Chelsea walinunua lukaku 98m, msimu uliofuata wakatoa kwa mkopo
Wakavunja rekodi ya Kipa, baada ya msimu benchi
Sasa wamarekani wa Liverpool na Man United hawawezi hilo, watampetipeti mchezaji mpaka waone ameshindikana kabisa
Klopp alimpetipeti keita, united walimpetipeti Pogba ilivoshindikana kabisa ndio wakaachiwa
United walipiga kelele na Maguire ila bado yupo, wakati Chelsea koulibaly walimtoa mapema tuu
Kwa bei ya Nunez tutarajie Klopp ataendelea kumtetea kwa kila hali mpaka itakaposhindikana
Minamino, shakiri, solanke, hawa waliachiwa mapema tuu kutokana na bei alizowanunua