Aisee mpira sio wa wote na inategemea na fate muda mwingine.
Kuna mchezaji alikipiga Spurs, QPR, Brighton, Fulham, Westham enzi hizo. Kwa walioingalia Fulham ya 2008-2011 hivi watamkumbuka jamaa, na Fulham ya Clint Demspey, Philip Sendaros, Muphy, Hangeland,Mousa Dembele, timu ya nguvu hii ukikutana nayo Craven Cortage unajiuliza mara mbili mbili.
Sasa Zamora na kiwango kile alishangaza watu kwa kusema hapendi kucheza mpira. Unajiuliza commitment ya mazoezi anaipata wapi?
Sasa tuje kwenye story moja hivi. Kuna jamaa anaitwa Jerome Sinclair. Huyu jamaa alikulia academy ya LFC aliichezea LFC not to senior level, but cups game na europe games japo not as a starter those days. Speaking of 2014 huko. He was playing as CF. Katolewa kwa mkopo weee akaamua kustaafu.
Sasa hivi ana Fried Chicken Shop huko Uingereza. Ukisikia “KAMA HAIPO NI HAIPO” ndio hivi visa viwili.
Bobby Zamora hakupenda kucheza mpira ila alipata kuucheza mpira. Jerome Sinclair aliupenda mpira lkn mpira haukumpenda.
Zamora kwa sasa ni 42’
Jerome ni 27’