Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Dah, wee tablet na wenzako...yamekuwa hayo???? Timu itakuwa kali kweli mda mfupi ujao! Mtarudi hapa na misifa kibao nyie subirini magarasa waondoke hlf mtaona mambo...YNWA.
 
Dah, wee tablet na wenzako...yamekuwa hayo???? Timu itakuwa kali kweli mda mfupi ujao! Mtarudi hapa na misifa kibao nyie subirini magarasa waondoke hlf mtaona mambo...YNWA.

Wachana nao hao juu hawaoni unachokiona au nachokiona hii timu kati Roy na Kenny na sasa hivi basi ya sasa hivi japo tupo table kubaya inatia uhai ya kwamba miaka ijayo itakuwa ya maana taratibu tutafika tu nikuwagawa tu kina Downing wapotelee mbali hata EPL nisimuone kucheza kuna madogo wakali sasa hivi Under 21 pale LFC timu ya wadogo kibao kina Abe,Sinclair,Michael Ngoo na kibao na tulichokosea Kenny alivyomuachia Tom Ince tu LFC wanatakiwa wamrudishe dogo then wawapange Kina Suso na hao madogo wengine kwa muda mmoja kwa miaka wakianza kuelewana itatisha timu. Kenny ndio alichotakiwa kufanya sema sifa zake za kusikiliza migazeti British player sijui so and so ndio akaleta ma Bouncer wa Club za Bongo kina Andy Carrol kuja kucheza mpira. Downing anakimbia kama lunyamila anatizama chini tu mpaka anagongana na kibendera cha kona.
 
Haya tunaongoza 1-0 anaingizwa Hendo vichekesho sitizami tena Huyu Hendo anakuja kufungisha tu anachojali nywele zake na sox kama zimekaa vizuri.
 
Result sio Mbaya Suarez kakosa vipi pale? Fulltime Liverpool 1 Southampton 0.
 
Michu just shows how overpriced British players are. He cost Swansea just £2m, which is so cheap compared to the fees British players go for." Robbie Savage. Wenye LFC wakimtizama Michu wakiuliza bei alionunuliwa na Kenny kupewa pesa kuwapa bure Newcastle basi ni aibu tosha kuwa Andy Carrol.
 
Mmmmhh! Afadhali!

Nina imani kwa kuwa club yetu inahitaji marekebisho nina uhakika wa kufanya vizuri tu ktk siku za usoni!
 
Tumeshinda lakini bado timu hii ni mbovu. Inahitaji reinforcements. Tunahitaji 2 pure strikers (goal poachers), 2 speedy wingers na 1 center back. Tukiweza hayo basi tutarudi enzi zile ya kubeba ile ndoo yetu "UEFA champions league"
 
Kazeni buti mtafika mbali naona mshawakaribia Arsenal
 
526941_10151195664723598_1596907149_n.jpg


hapa ni wakati anafunga goli la kuongoza la liverpool Jordan Henderson
 
Tumeshinda lakini bado timu hii ni mbovu. Inahitaji reinforcements. Tunahitaji 2 pure strikers (goal poachers), 2 speedy wingers na 1 center back. Tukiweza hayo basi tutarudi enzi zile ya kubeba ile ndoo yetu "UEFA champions league"
Mkuu kinachohitajika zaidi ni accuracy ya wachezaji hasa wanapokuwa kwenye eneo la kufunga. Kwenye gemu hii liva walipoteza clear chances nyingi sana hasa kipindi cha kwanza.
Wachezaji wa liva siku hizi (ukimtoa Gerrard na Cara ambaye umri unamtupa mkono) hawana ile "The Kop Spirit" ambayo tulikuwa tukiishuhudia miaka ya nyuma.
 
ndetichia; Hakika nakwambia hii club itakuja kushangaza ulimwengu majira kidogo ijayo!

Mkuu tusijidanganye kuwa na matumaini tele kwa kikosi hiki cha sasa kama hatutaongeza wachezaji wazuri. Huyo Henderson na Jonjo wanatakiwa wauzwe. Hamna vipaji hapo. Both of them are just average players. Downing and Joe Cole should also be traded or just cut both of them
 
Back
Top Bottom