Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

BREAKING: A proposal to ban state-controlled clubs from English football has been included in the Football Governance Bill.

If passed, Manchester City and Newcastle would need to change ownership to obtain a licence from the new independent regulator.

[@TimesSport]

Mmeelewa vipi hii statement Wakuu
MosDef
Captain Marvelous
The MoNA

Hii habari imependekezwa muswada kuhusu vilabu vinavyomilikiwa au kudhibitiwa na Serikali kufutiwa leseni ya umiliki kwa vilabu husika vinavyoshiriki ligi kuu nchi uongereza.

Man City na Newcastle wametajwa. Kwa nini?

Man City mmiliki wake vice president wa Unated Arab Emirate bwana Sheikh Mansour,
huku Newcastle wakimilikiwa na Saudi Arabia’s Public Investment Fund chini ya m/kiti Mohamed bin Salman (crown Prince)

Ukiwatazama hao wamiliki hapo ni wahusika wa moja kwa moja na serikali wanazozihudumu na wana madaraka makubwa nchini mwao. Sasa ishu inataka kuwatenga watu wanaomiliki vilabu wasihusike na serikali, wawe individual owners lengo ni kukwepa kutumika fedha za nchi wanazotoka kuendeshea timu hizo.

Waliobaki wote ni individual owners wakiwemo wabahili kutoka USA, FSG wa LFC.

Ngoja tuone kama muswada utapita tushuhudie oil money ikipotea.

Hapa M16 wamenusa harufu ya pesa chafu kutumika hasa na wamiliki wa City, huu muswada haujaanzia from Nowhere tu,

Vuta kiti chukua visheti endelea kusikilizia, ukipita uniarifu[emoji81]maana wameanza kuwaandama.

Ynwa’
 
5 wins 🏆, 5 Man of the Match
 

Attachments

  • Screenshot_20241129_082351_Threads.jpg
    Screenshot_20241129_082351_Threads.jpg
    1,009.8 KB · Views: 2
Hakuna mahali tumesema tunabeba makombe, ila yakija it’s a bonus for sure.
Hii statement nimeielewa aisee
Incredible Incredible Incredible start for Arne Slot with his boys.

We have started our match vs Madrid with three worriors from LFC Academy:-

Kelleher
Bradley
Jones

With top top top performance,Just outstanding performance.

And other top worriors from bench from LFC Academy product
Trent
Quansah
Elliot*

I said nikiwa na pressure kubwa na mechi mostly huwa tunashinda and it went on our side completely. Its my fortune, na huwa naandika nione ni kweli hutokea? Yes.! 90% hutokea.

Slot alitazama fainali ya 2022 Lfc vs Madrid na 2-5 lost to Madrid. He told his Feyenoord’s boys this is a football we want. Just find any how to win games.
Huyo ndiye mdachi aliyerithi mikoba ya Klopp. Klopp huko alipo anajionea mbegu aliyoipanda imeota na perhaps miti imekomaa bado kuzaa matunda matunda.

It was always easy for Ancelotti akikutana na Klopp, why?? Always Klopp kwenye maisha yake ya soka anaamini anachoamini na kitampa matokeo kitu hicho (PLAN A). Hii ndiyo system yake aliyoitaka “ATTACK ATTACK ATTACK”, aliamini ndio namna kumshinda mpinzani and no otherswise you could say akuelewe. It was easy kwa Don Carlo kwa sababu alizuia chini most of the time akiamini LFC hawana creator kwenye final third Silaha yao kubwa ni RB & LB, RW & LW weakness yao Highline cheat code counter attack football with low block system and its over.
Committ more bodies kwenye eneo lako na uwasubirie waje target yetu ni their weak side RHS through their RB. Hapo tu ndio tulipowakosea Madrid plus Courtois anapenda sana kucheza na LFC huwa anakuwa prime Dida mix, Cassilas, Mix De Gea Mix, Neur, Mix Buffon, Mix Reina anafanya saves za kukera sana. Amefanya saves hizo na mechi ya jana n leo, Saves za kukatisha tamaa.

Ancelloti alinyumbulika kidogo kwa sababu LFC kwa sasa haina muundo ule aliyouzoea misimu mingine. Akaanza na 4-3-3 why? Kutengeneza press kuanzia juu kwa sababu LFC msingi wa mashambulizi unaanzia kwa GK & CB’s hivyo mstari wa kwanza akatengeneza very tight with Mbappe Guler and Brahim Diaz, ili kuwazuia Macca & Gravern wasipokee mipira kutoka kwa Vvd, Konate, and Kelleher. Hili halikuwa suluhisho still Vvd, Konate & Kelleher walifanikiwa kupenyeza mipira mingi hasa kwa Gravern ambaye ana deadly half turns, mpira ukawa unatembea bila vikwazo vikubwa. Kwenye football tactics pekee hazikusaidi inahitaji technical players kutimiza hizo tactics ndio kama game ya jana. Don Carlo alijua kila kitu kuhusu Slot ila Slot alikuwa na technical player kutekeleza matakwa ya Slot, Gravern, Jones, Macca technical players mguuni akilini vimo.

Basi:-

Don Carlo akabadili mbinu baada ya kuona haimpi akitakacho akabadilika na kurudi 4-4-2 diamond/flat (huu ndio mfumo wake aliotuadhibu nao mechi tano hivi akiwa na Madrid). Why alirudi 4-4-2?? Sababu ni moja kwenye 4-3-3 yake LFC walisambaza mipira ndani na nje kiwepesi, akaona sasa dawa ni kuwaacha waje mpaka katikati ya uwanja na kuanzia hapo tuwanyime uhuru wanaoutaka kutupia mipira ndani na wakaanza kuzuia kwa kuanzia nusu yao ya uwanja tu. Ikawa nyie LFC njooni na mpira wenu mpaka hapa katikati ila ndani hatuwaruhusu kupita, tafuteni ufumbuzi wa pembeni na sisi, tunasubiri mpoteze mpira tuinyakue tuitupe kwenye njia mbele kule kwa Diaz Guler Mbappe.

Kwa hapa Don Carlo alirudi kwenye mbinu yake ya siku zote ya achezapo na LFC, akawa amefanikiwa japo LFC walijaribu mara kadhaa kupenya na wakafanikiwa ila goli kulikuwa na mtu anaitwa Thibaut Courtois akiona Jersey nyekundu anavaa mikono mingi. Huyu Huyu Courtois kamwangalie akicheza na kina Elche na Leganes huko, two different player (its just a notion).

Na hivi ndivyo kipindi cha kwanza kikaisha My man of the match for that 1st half was Courtois good game even 2nd half.

Second half Slot is master of second half so far, ameonesha hivyo kwemye michezo kadhaa. Sio kitu kizuri but as long as kinakulipa its a good.

Jamaa anajua kuusoma sana mchezo he is among the best.

Baada ya kuona struggling kwenye low block ya Don Carlo, Slot akaja na Combination play. Unafanya overload ama centrally au wide side ila Slot chosen wide combination ili kuwatoa Madrid kwenye Shape yao ya kuzuia kwa idadi kubwa ya wachezaji na spaces zipatikane. 1-2s ikapigwa, overlapp ikafanyika, third man run ikafanywa, especially RHS.

Goli la Macca ilitokana na Combination play, Juu kulikua na Robbo, Jones, Diaz na Macca chini yao kidogo, lengo unawavuta Madrid upande huo na kufungua Spaces, then Robbo anafanya third man runner ama pembeni au katikati ya mabeki, same to Bradley ikiwa movement itakuwa upande wa kulia. SPACES & TIME ukivitumia vizuri chance ya kuwin huwa kubwa.

With combination play goli la kwanza likapatikana, ndipo Don Carlo akaamua na yeye afunguke, ikiwa sasa ni mwenye nguvu mpishe. There were time LFC we used 3-1-6 ili kutengeneza Combination play plus turn overs.

“ETH alikuambia LFC are deadly recently kwenye turn overs usipowakabili “they will kill you” zingatia they will kill you.” Utd wakaacha kichwa Slot wakamchukua ETH heheh Thats football life, kama LFC tukabeba Minamino tukaacha Haaland.

Ndio maisha ya mpira. Hivyo ndivyo mechi ilimalizika kwa mbinu za Slot vs Don Carlo. High pressing High defensive line ilitumika kwa tahadhari kubwa sana. Slot told the boys untill you hear final whistle then you are free to do anything and withdraw your attention and focus vs Madrid.

Courtois and Kelleher waliamua mechi iende 0-0 HT.

Kelleher aliamua mechi imalizike kwa cleansheet, with that penalty save ilituacha mchezoni big time.

“Heroic Moment” View attachment 3164365


Kelleher is a #2 best ever GK in the world no debate. Three concecatve PK saved, 1 with his national team 2 vs S’ton na 3 vs Madrid.
View attachment 3164366

Bradley famous tackling against Mbappe, itawekwa kwenye historia ni moja ya picha itasambaa mitandaoni kwa wapenda soka ulimwenguni.
View attachment 3164367

View attachment 3164368


Bradly without the ball and with the ball was exceptional, 1v1 ya Mbappe na kupanda kufanya overload at the age of 21 real phenomenal, Bravol Conor, confidence, intelligence, composure.

View attachment 3164370


Jones

Possession footballer i rated him highly since those days akiwa u18, changamoto kwake ni maamuzi, good technical player, kuna tuvitu alivifanya hahah Mr. Confidence (
emoji881.png
)yupo on form. Ndilo soka analolipenda na kulifurahia.

Gravern any debate about him ??possession footballer, half turns za maana sana, Robbo “another good dutch player” alipotuwa Axa yalikuwa maneno ya Mscotish Andrew Robertson.

Konate & Vvd boss and comand the atteckers very well. Another cleansheet for them. View attachment 3164372



Macca as 10.
Ni mzuri mno mno, hana pace slow but sure, he knows where to gear up when to slow the tempo, quality passes, goli lake ni very Class kumpa pass Bradley na kuutaki ndani ya box sio kwa ajili ya wengi.


Salah,
should come down on his revenge desire aliwapania sana Madrid, the rest he did it well.

Nunez & Diaz all could have scored, but Courtois quality denied them.

Kuna battle ilikuwa inaendelea btn Ansencio na Nunez, plus Rudiger na Vvd ikitokea set pieces. Pale unajaribu kujazwa kama una temper nyekundu inaanza kubisha hodi,

Lets enjoy our moment regardless output of what we are doing currently.

Chelsea
emoji736.png

Leipzig
emoji736.png

Arsenal
emoji1754.png

Brighton
emoji736.png

Brighton
emoji736.png

Leverkusen
emoji736.png

Aston Villa
emoji736.png

Southampton
emoji736.png

Real Madrid
emoji736.png

Man City
emoji3480.png




Incredible records for Arne Slot with his boys. 17 win out of 19 one defeat and one draw.

Nottigham watajiuliza how did we win vs this team?? Its was a good defeat.

We are enjoying with what we have and earn at time.
Hakuna mahali tumesema tunabeba makombe, ila yakija it’s a bonus for sure.

Know You Can,
Ynwa’
e
 
Salah hakutakiwa kupewa penalty mechi dhidi ya Madrid.
Anataka alipe kisasi, probably angekosa tu.
 
Endrick baada ya kumuumiza konate mashabiki wa Liverpool sasa 😂
 

Attachments

  • FB_IMG_1732942392163.jpg
    FB_IMG_1732942392163.jpg
    46.1 KB · Views: 2
Hivi nikwanini wanaikataa Liverpool nakwenda Madrid?
 

Attachments

  • FB_IMG_1732953804134.jpg
    FB_IMG_1732953804134.jpg
    106.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom