Liverpool FC yainyuka Manchester City 4-3 na kuvunja mwiko

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411


ENGLAND: Mchezo umemalizika kwa Liverpool FC kuinyuka Manchester City kwa mabao 4 kwa 3 na kuvunja mwiko wa kutofungwa uliowekwa na Manchester City tangu ligi ya msimu huu 2017/18 ianze.

> Magoli ya Liverpool FC yamefungwa na Alexander Oxlade-Chamberlain dakika ya 9, Firmino dakika ya 59, Sadio Manè dakika ya 62, na Mohamed Salah dakika ya 68.

> Huku magoli ya Manchester City yamefungwa na Leroy Sanè dakika ya 41, Bernardo Silva dakika ya 85 na Ilkay Gündoğan dakika ya 90+1.
 
Mungu mkubwa, sasa kazi imebaki kwa man u kesho na yeye kushusha kipigo apunguze gap!!
 
Hatimaye.....hata gemu yao ya kwanza upepo ulianza kugeuka....thanks to red card PG akatoboa kwa ushindi mnono.

Game ijayo angepandwa tena Ingependeza Zaidi..
 
Atleast solution imepatikana. City ni kuwaatack tu. Ukipark meli kama anavyofanyaga Mourinho, lazima wakudukue. The best way of defence is to attack...
Nakumbuka el classical ya mwisho kwa gadiola, mou alipaki basi mpaka gadiola akadata, enzi hizo defense ya madrid inaongozwa na pepe na ramos!!! yan barca wakipanda tu, madrid wote wanashuka kulinda goli hahahahaa baada ya hiyo gemu gardiola akatangaza kuamia buyern!!
 

Hakuna Kitu chochote ninachokipenda au kukishabikia kisiwe Kizuri. Akhsanteni sana Wachezaji wangu wa Liverpool na mwana Liverpool yoyote popote pale ulipo hebu jipongeze na furahi kwani leo tumecheza Soka la aina yake japo mwisho mwisho tulikuwa tunabana sana ' Mambupu ' yetu ili Magoli yote yasirudi kwani Manchester City walikuwa wakifanya come back za hatari. Sasa kwa hiki Kipigo tulichowapa Manchester City kuna uwezekano mkubwa tukijitahidi na kujiimarisha hasa sehemu yetu ya Ulinzi Liverpool FC tunaweza kuishia kuwa nafasi Tatu bora kabisa na juu. Mara nyingi sana Liverpool huwa inafungwa pale tu ikivalia ile Jezi ' Gundu ' ya Njano ila ikicheza mechi zake na kuvalia Jezi Nyekundu huwa na ' baraka ' mno na Timu huwa inashinda halafu magoli mengi tu.
 
Kwakweli nimefurahi sana kwa mahasimu wangu wa liverpool kuwafanya vibaya guardiola na wanawe .
Ilikuwa ni shida kwakweli kila aliekuja mbele alikuwa anakaa ila liver mmetukomboa big to all livpool's fans
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…