Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
ENGLAND: Mchezo umemalizika kwa Liverpool FC kuinyuka Manchester City kwa mabao 4 kwa 3 na kuvunja mwiko wa kutofungwa uliowekwa na Manchester City tangu ligi ya msimu huu 2017/18 ianze.
> Magoli ya Liverpool FC yamefungwa na Alexander Oxlade-Chamberlain dakika ya 9, Firmino dakika ya 59, Sadio Manè dakika ya 62, na Mohamed Salah dakika ya 68.
> Huku magoli ya Manchester City yamefungwa na Leroy Sanè dakika ya 41, Bernardo Silva dakika ya 85 na Ilkay Gündoğan dakika ya 90+1.