Hakuna Kitu chochote ninachokipenda au kukishabikia kisiwe Kizuri. Akhsanteni sana Wachezaji wangu wa Liverpool na mwana Liverpool yoyote popote pale ulipo hebu jipongeze na furahi kwani leo tumecheza Soka la aina yake japo mwisho mwisho tulikuwa tunabana sana ' Mambupu ' yetu ili Magoli yote yasirudi kwani Manchester City walikuwa wakifanya come back za hatari. Sasa kwa hiki Kipigo tulichowapa Manchester City kuna uwezekano mkubwa tukijitahidi na kujiimarisha hasa sehemu yetu ya Ulinzi Liverpool FC tunaweza kuishia kuwa nafasi Tatu bora kabisa na juu. Mara nyingi sana Liverpool huwa inafungwa pale tu ikivalia ile Jezi ' Gundu ' ya Njano ila ikicheza mechi zake na kuvalia Jezi Nyekundu huwa na ' baraka ' mno na Timu huwa inashinda halafu magoli mengi tu.