Hii Mada aliipost jamaa Fulani kwenye group la what's app nikamuelimisha mwisho alinielewa nashangaa amekuja tena kupost huku.!!
Twende kwenye facts, Liverpool ni team iliyo kwenye kiwango bora kwa sasa maana kwa msimu uliopita ilimaliza ligi na points 97 point moja nyuma ya aliyekuwa bingwa man cty ambaye alikuwa na point 98.!
Msimu huo wa 2018/2019 Liverpool ilitwaa mataji matatu makubwa duniani yani
CL
Super cup na
FIFA World Club champions
Hakuna team inayotamani kucheza na Liverpool kwa sasa duniani.
Wachambuzi uchwara walisema kwa Liverpool ile kushindwa kutwaa epl msimu wa 2018/19 basi hawatatwaa tena kwa miaka ya karibuni Leo wapo wapi??
Wachambuzi uchwara walisema ngoja ifike Dec,na katikati ya Jan Liverpool watachemsha Leo wako wapi??
Wachambuzi uchwara walisema man cty ina kikosi kipana unaweza ukatoa vikosi vitatu Leo wako wapi??wachambuzi uchwara walisema ngoja Mane aumie team itapoteana Mane kaumia na bado team inashinda sasa wamekuja na epl ni ligi mbovu na sio ngumu Kama tunavyoaminishwa!!
Leo hii mashabiki wa man u, Chelsea,arsenal wanaacha kuangalia ubovu wa team zao wanakuja na propaganda wa ligi sio ngumu je isingekuwa ngumu wao wangekuwa na point 30?????????
Acheni uchambuzi uchwara Liverpool ipo kwenye kiwango bora sana kwa sasa na Hakuna team inayotamani kukutana nao kwa sasa Messi na barca yake walipigwa INE pale anfield
Sent using
Jamii Forums mobile app