Liverpool imeiumbua E.P.L , sio ligi ngumu kama tulivyoaminishwa

Liverpool imeiumbua E.P.L , sio ligi ngumu kama tulivyoaminishwa

Inshot timu za uingereza zenye uwezo wa kuchukua UEFA ni nyingi kuriko ligi yoyote ile, leo timu kama Man U anaweza shindana na PSG au Bayern ila sio Valencia na Bayern


Sent from my iPhone using JamiiForums
una kichaa, Man u ishindane na bayern ? au Bayern gongo la mboto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ligi ya kweli, ngumu na yenye msisimko kwa sasa ni EPL, zilizobaki ni ovyo tu.
Kuingiza timu 4 robo finali ya UCL siyo jambo dogo.
Timu nne za ligi moja kucheza fainali zote mbili za Ulaya msimu uliopita si jambo la kupuuzwa.
Hata hivyo kuchagua upande wa kupenda kama ulivyofanya mleta mada ni jambo la kawaida kwa kila kibinadamu
unachosema La liga walikuwa wanafanya daily...

Unakumbuka Real madrid kachukua uefa mara 3 mfululizo juzi hapa...

Ingekuwa ni timu ya uingereza imefanya hivyo mngeipamba kwa kila aina ya mapambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado epl ni ligi bora,hata kwa kutazama tu mechi zake una-enjoy,juzi nilikuwa natazama mechi kati ya newcastle na everton aaah ilikuwa bonge la mechi yan

Sasa nenda kajaribu kutazama mechi ya espanyol na sevilla kama hujazima tv..yaani ni heri uangalie mechi ya serie A labda lazio na hellas verona unaweza kupata burudani
 
Liverpool, kamati yao ya ufundi ina kila sababu ya kupongezwa.
 
EPL ukitaka iite kwa kirefu ENGLISH PREMIER LEAGUE.

Ukitaka kujua ni ligi ngumu nitajie mabingwa wa ligi 5 kubwa ulaya ktk misimu 10 alaf majibu baki nayo. Ligi bora haipimwi kwa msimu mmoja.
 
Mwenye kichaa ni ww apo
Man u kamtoa PSG akiwa mbovu kwenye ligi mwaka jana, PSG huyohuyo anamtoa kirahisi au ni tim ngumu kwa Bayern,
Kwa kifupi we ndo kichwa asiejijua


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hata Chelsea ya 2012 ilikuwa mbovu kwenye ligi ikachukua uefa ikizifunga Barca na Bayern zilizokamilika huyo jamaa hajui mpira
 
Kuna hii ngonjera na propaganda ambayo imetawala vichwa vingi vya mashabiki wa mpira kuwa E.P.L ndiyo ligi ngumu zaidi duniani.

Kila siku huwa tunawapa facts huku kuwa England sio ligi ngumu bali timu zake zinakaribiana viwango watu wanakuwa wabishi hata unapowapa facts.

Bahati nzuri huu mwaka Timu ya Liverpool imekuwa katika kiwango bora na cha juu kushinda timu nyingine zote ndio tunaona sasa ukweli kuwa hii ligi huwa sio ngumu bali timu zinafanana viwango.

Tokea umeanza kushabikia mpira wa miguu ni mwaka gani ambao umeona katika Ligi 3 kubwa za ulaya ( La liga, Bundes liga na E.P.L )timu inayoongoza kwa pointi inaipita timu inayofuata kwa zaidi ya pointi 20 !!! Hata kule Serie A ambapo juve anachukua kwa miaka kama 7 mfululizo hili jambo ni nadra kutokea hata kwenye zile farmers leagues .

Je , hii Liverpool ndiyo timu bora kuwahi kutokea ulaya?

Jibu ni Hapana, Timu bora kuwahi kutokea ulaya katika karne ya 21, kwa maoni ya wengi ni ile Barcelona ya Pep Guardiola (2008-2011) ambayo ilisomba makombe yote unayojua ndani ya msimu mmoja, Hii timu na ubora wake wote haikuwahi kuongoza kwa pointi 20+ ...

Mashabiki wengi wa soka wakawa wanatoa kejeli eti Barcelona ile Pep ingepata tabu England, mi nikawa najiuliza kama Liverpool tuu hii ya kina Henderson, Wijnaldum , Milner inawatesa hivi ingekuja Barca ya ile ya kina Xavi na iniesta si isingefungwa kabisa hata misimu 3, maana katika timu hii ya Liverpool inayotesa sahizi ni wachezaji wawili tuu wangeweza kucheza ile Barcelona na wenyewe ni beki kisiki VVD na kipa wao Allison baasi, wengine kama captain wao Henderson hata benchi asingekaa.

Sasa iweje Liverpool ambayo tunaambiwa iko kwenye ligi ngumu zaidi ulaya iongoze kwa pointi 20+ kitu ambacho hata hakitokeagi kwenye ligi ya ureno ?

Mashabiki wa England sijui mtakuja na utetezi gani !!

Yaani tofauti ya pointi kati ya wa 1 na wa 4 ni pointi 32[emoji23][emoji23][emoji23], Halafu unaambiwa hiyo ndiyo ligi ngumu zaidi Duniani

Liverpool imeiumbua E.P.L....aibuuuuu

View attachment 1344079View attachment 1344081View attachment 1344086

Sent using Jamii Forums mobile app
. Ok , Hivi ni mwaka gani vile Barca walibebwa against Chelsea , Chelsea walinyimwa penalties nne za halali , then drogba akamtukana mwamuzi yule mnorway ? Then ineasta akafunga bao zuri
 
umetumia perfomance ya msimu mmoja?

unajua katika kipindi cha miaka 10 iliyopita hao E.P.L wamechukua Uefa mara ngapi ?

kama hujui basi ujue kuwa wamechukua mara 2, Germany mara 1, Serie A mara 1 na La liga mara 6...

Kwa kipimo chako ligi bora ni La liga

Sent using Jamii Forums mobile app
Iko sio kipimo sahihi kwani Barca na Madrid wanapendelewa , kumbuka Ramos alivyomuumiza Mo salah bila ya kuchukuliwa hatua yoyote , Chelsea walinyimwa penalties nne halali , Kuna mechi nyingine refarii a kitushiwa kuuwawa na mashabiki wa Chelsea hii ilikuwa na Barca , etc
 
Back
Top Bottom